Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!


Unakaza sana ubongo. Relax usijekufa na pressure bure
 
Kwahiyo anaweza kubadili hizo sheria na mfumo ndani ya siku moja ??
 
Baadhi ya Watanzania wenzetu ni wagumu sana kuelewa
 
Sawa lakini itakuwa ni tofauti na mtangulizi wake, Mtangulizi wake alitawala kwa ubabe sana watu wameumizwa kwasababu za kijinga kabisa
 
Itachukua muda kupeleka sheria mpya bungeni kubadilisha sheria mbovu zilizopo ila ukipewa mkono wa amani ni vizuri kuupokea kabla mazungumzo hayajaanza. Alichofanya kwa sasa ni kutoa mkono wa salamu wa amani, tuupokee huo kwanza kabla ya kukaa chini kwa mazungumzo rasmi.
 
maneno matamu bila vitendo haisaidii maneno mazuri bila katiba mpya ni yaleyale
 
Usemayo ni sahihi ila ameonyesha nia njema ya kulipa taifa haki na usawa kulingana hata na zile sheria mbovu ambazo zilikuwa hazizingati miezi miwili nyuma.
Tuikubali kwanza hatua hii ya mwazo wakati tunasubiri kuoana atafanya nini kuhusu katiba mpya.
 
Hakina mama amejua kutufuraisha
 
Kwahiyo anaweza kubadili hizo sheria na mfumo ndani ya siku moja ??
Wapi nimesema kuwa abadili sheria kwa siku moja?Nilichomaanisha mimi ni kwamba kumsifia Samia au kuwa na matumaini nae kwa sababu ya maneno yake matamu siyo sahihi kwa sababu hata Hitler alihadhaa watu kwa maneno yake matamu na watu wakamuunga mkono katika kumfanya kuwa waziri mkuu wa German kumbe moyoni alikuwa na agenda nyingine.Mtaji wa wanasiasa ni maneno yao matamu.Hatupaswi kabisa kuwaamini wanasiasa katika maneno yao matamu bali tunapaswa kuwaamini katika sheria wanazosimamia.
 
Kwa hyo ulitaka hayo yote ayafanye ndani ya siku 18?
 
Kwahiyo tukasirike from Day Zero kuonesha kuwa huko mbele atapuyanga ??
 
Unakaza sana ubongo. Relax usijekufa na pressure bure
Utakuja kufa kwa presha wewe ambae unaamini na kufurahia maneno matamu ya Samia wakati mambo yatakuja kuwa ndivyo sivyo kwa sababu yeye anaongoza nchi kwa mujibu wa sheria ambazo ni gandamizi na onevu!Maneno matamu na yanayotia matumaini huwa hayaongozi nchi,kinachoongoza nchi ni sheria.
 
Amesema atapita kwenye kila sekta... Hivyo atapokea lawama na malalamiko ambayo atayafanyia kazi
 
Hivi nyie mnaotaka apewe muda kubadilisha sheria mnataka huo muda apewe mpaka lini? mbona wao wakitunga sheria zao mbovu mbovu za kutukandamiza huwa wanaitisha vikao vya bunge vya dharura kwa ajili ya kupitisha mambo yao kwa manufaa yao, kwanini kwa spidi hiyo hiyo wasirekebishe hizo sheria? nini kilichomshinda leo kutamka hayo maneno atahakikisha sheria kandamizi zinafutwa? au hajui kama zipo wakati naye alikuwa sehemu ya utawala uliopita?

Mnampa muda wa kurekebisha hizo sheria matokeo yake itafika 2025 october bado mnasubiri tu, sheria za kijinga kama za kuzuia nakala za matokeo kwa wagombea ubunge mnataka zisubiri tu mpaka atakapojisikia kuzifuta? au nguvu alizopewa msajili kufuta vyama vyama siasa? anyway endeleeni kushangilia tu, najua mtu akiwa amelala akiota ndoto nzuri ukimshtua usingizini anaweza kukupiga ngumi, nawatakia usingizi mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…