Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Hebu orodhesha hapa sheria za kipindi cha Magufuli ambazo unadai Kuwa ni kandamizi.
 
Huo ni mwanzo tu, huwezi futa sheria hizo ndani ya siku 18 !!!
Sijasema sheria zifutwe ndani ya siku 18!Mimi namlaumu sana mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu ila alikuja kuwaua kama Kuku!
 
Mkuu mbona umeumia sana? Au ulitaka atoe vitisho kama magu?
 
Hayati alikuwa na maadui wengi,toka amefariki zile story za baadhi ya watu kwamba watu wengi wanakufa kwa corona TZ hakuna tena...hii inaonesha wazi kwamba tatizo halikuwa corona bali hayati.
Corona ipo na inaua. Imemuua mpaka Magu mwenyewe na uongozi wa juu, bado mmekaza kichwa tu.

Akili za mizoga hizi.
 
My friend kwani wewe hupendi maneno matamu. Tena yakitoka kwa jinsia Ke[emoji6][emoji6]
 
Kwahiyo tukasirike from Day Zero kuonesha kuwa huko mbele atapuyanga ??
Tuwe neutral mpaka pale atakapofuta sheria zote gandamizi ambazo alizitunga yeye pamoja na Magufuli kwa sababu nchi huongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu na yanayotia matumaini.Maneno matamu na yanayotia matumaini huwa ni mitaji ya wanasiasa katika kuhadhaa watu ili watimize malengo yao.
 
Mkuu, tukasajiri Chama chetu tuingie mzigoni
 


Je, hakuna tofauti ya kiuongozi kati ya Mwendazake na Mama??
 
Kwa hyo ulitaka hayo yote ayafanye ndani ya siku 18?
Sijamaanisha kuwa hayo yote afanye ndani ya siku 18.Mimi namlaumu sana Mama na sikubaliani nae kwa maneno yake matamu kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Hilo ndilo ambalo lingetupa matumaini.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu ili watimize malengo yao ovu.Hata Hitler aliwapa maneno matamu wananchi wa Ujerumani hadi wakamuamini na kumpa uwaziri mkuu kisha akaanza kuwaua kama Kuku.
 
Anyway:

1- Wananchi tuna mahitaji yetu na

2- Wanasiasa pia wana mahitaji yao.

Ultimate goal ya mwanasiasa ni siku akipewa madaraka, halafu na yeye atatumia sheria hizo hizo kuumiza watu

Na sisi wananchi tunahitaji tu, ubora wa maisha yetu. Maana hakuna mwanasiasa anahangaika kupata kula.
 
We nawe unachosha bwana
Huna jema.
Mama Samia ndiye hana jema kwa sababu Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa sheria na wala siyo kwa mujibu wa maneno matamu.Yeye leo alipaswa atoe ahadi kuwa atafuta sheria zote kandamizi ambazo alitunga yeye mwenyewe pamoja na magufuli ila hakufanya hivyo.Maneno yake matamu hayana faida yoyote kwetu kwa sababu siku zote maneno matamu huwa ni mtaji wa wanasiasa katika kuhadaa watu ili watimize malengo yao ovu.Ni punguani peke yake ndiye anaweza kushobokea maneno matamu ya wanasiasa.
 
Wewe mwananchi huwezi kuwa na maisha bora kama unaongozwa kwa sheria ambazo hazina nia ya kukupatia muongozo sahihi katika kujitafutia maisha bora.
 
Je, hakuna tofauti ya kiuongozi kati ya Mwendazake na Mama??
Kumpima Mama ndani ya wiki hizi mbili siyo sahihi kwa sababu hata Magufuli,Hitler,Mussolin na kadhalika ndani ya wiki mbili za mwanzo walianza vizuri sana.Magufuli ndani ya wiki mbili za uongozi wake alikuwa ni role model leader huko Ulaya,Marekani,South Afrika na kadhalika ila baadae alikuja kuwa kituko kinachovutia hadi utalii!
 
Hebu orodhesha hapa sheria za kipindi cha Magufuli ambazo unadai Kuwa ni kandamizi.
1.Sheria ya Mitandao ya mwaka 2015.

2.Kanuni za Mawasiliano ya Kieletroniki na ya Posta (Maudhui ya Mtandaoni) zilizopitishwa mwaka 2018 zinamtaka kila anaemiliki blogu au tovuti kulipa ada ya leseni hadi shilingi za kitanzania milioni 2.1 (zaidi ya Dola za Marekani 900). Sheria hii pia inadhibiti maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa mitandao bila usimamizi wa mahakama.

3.Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti binafsi na upatikanaji wa taarifa za takwimu kwa umma kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, ambayo inawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa huru zilizothibitishwa. Wakati marekebisho ya sheria hii yaliyoletwa mwaka 2019 yameondoa dhima ya jinai kwa kuchapisha takwimu zisizo rasmi, mamlaka bado inadhibiti nani anayeweza kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu na kuamua kipi ni sahihi au sio sahihi.

4.Januari 2019, Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuweka vikwazo vingi zaidi vya haki ya uhuru wa kushiriki na kukusanyika kwa amani. Marekebisho haya yalimpa Msajili wa Vyama vya Siasa nguvu ya kufuta vyama vya siasa, kuitisha taarifa kutoka vyama vya siasa na kusimamisha wanachama. Pia ilianzisha hitaji la mashirika na watu binafsi kupata kibali kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo ambalo linazuia haki ya mwananchi kupata taarifa.
 
Utu vs vitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…