Ndiyo kusema Tanzania imejiunga kwenye Umoja wa Nchi za Kiarabu kimya kimya?

Zanzibar iko mbioni kuanzisha mfuko maalum wa kusaidia wanaoenda Saudia kila mwaka kuhiji. Hayo ni maneno ya Mhe. Husein Ally Mwili, Rais wa Kisiwa hicho.
Hadi hapo Unahitaji majibu gani zaidi mleta mada?
Hata waarabu wakristo wa Lebanon na kwineko kote duniani maandishi wanayotumia ni ya kiarabu !! Mpaka biblia yao imeandikwa kwa maandishi ya kiarabu !! Na ibada kanisani huwa inaendeshwa kiarabu !! Na majina yao mengi ni haya haya unayoyasikia kwa waarabu wakiitwa !! Kwa mfano aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Iraqi alikuwa anaitwa Tariq Aziz alikuwa ni Mkristo !! Huko Lebanon nusu ni wakristo na nusu ni waislam na wote ni waarabu na lugha wanayotumia ni kiarabu. !!
 
Hata mimi ni Mgalilaya lakini naitwa Ishmael Taib Erdogan Malughu
 
Hoja nzuri.

Baada ya mwigu Kutoa hoja mjengoni ya kurekebisha tozo,

Alionekana baada ya siku kadhaa Kwa TV akiwa na waarabu na akasema wanapitia mikataba waliingia Ili warekebishe Ili bidhaa zisitozwe mara mbili.

Nimejiuliza Pana mahusiano Gani ya kimkataba ya nchi yetu na Nchi za waarabu kibiashara??

Tutapata majibu soon.
 
Hili ni jambo la Siri ila wenye maarifa hujua
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana.... kuna bidhaa zina maandishi ya kifaransa basi tutakuwa tumejiunga na ufaransa kimyakimya.
Siyo uwezo mdogo wa kufikiri,kabugizwa chuki dhidi ya uislam kwenye jumuiya za dini yake shuleni mpaka chuoni(Kama kajaaliwa kufika),huwa Wana hofu na waislam,baraghashia,kanzu,hijab vinawatatiza Sana kuliko dhambi zao
 
Zanzibar iko mbioni kuanzisha mfuko maalum wa kusaidia wanaoenda Saudia kila mwaka kuhiji. Hayo ni maneno ya Mhe. Husein Ally Mwili, Rais wa Kisiwa hicho.
Hadi hapo Unahitaji majibu gani zaidi mleta mada?
Serikali Bara zamani ilikua ikigharimia wafanyakazi wake kwenda hijja
 
Iq yako ni below zero,kuweka kiarabu(lugha yoyote) kwenye bidhaa maana yake bidhaa imeingia kwenye soko la hiyo lugha
 
Wewe huwezi kuelezea Jambo lolote ukaeleweka...sababu akili huna
 
Mada inachekesha Sana hii!

Imani Ndio uhalisia wa mtu na anaoshirikiana nao!!

Hatuwezi kuepuka NGUVU yake kwenye inner self ya mtu,itajionyesha tu!!

Tulijenge Taifa letu!!
 
Udini ndo unaokutesa..
Kuna nchi imepitia mauaji ya kutisha kushinda Rwanda??!!
Tena yalichochewa na Mapadri wa Katoliki.
Mauaji ya Liberia je?
Yanayoendelea DRC je?
Huko nako ni Waislamu?

Rwanda sababu ya mauaji yao wa catholic wala hawakuchochea ( unawasingizia tu)

Sababu ya mauaji ya rwanda ilikuwa nj chuki ya kikabila.. mhutu anamuua mtutsi na mtutsi anamua mhutu.

Padri wa ki catholic akiwa mhutu hawezi kutetea watutsi maana ni adui zake kikabila.

U catholic haukuwa sababu bali ni Uhutu na Ututsi ndio sababu
 
Hakuna cha typing error hapo ni umekosea kabisa hilo neno. Siku nyingine andika comment yako kwa kiswahili tu. Hayo maono yako ni ya kipumbavu na ya kibaguzi. Nchi kibao zinatuuzia bidhaa na zimeandikwa kwa lugha mbalimbali na maisha yanasonga ila ikiandikwa kiarabu ndo inakuwa shida? Ishauri nchi ijenge viwanda vyake au iweke sharti kwamba bidhaa zote zinazoingia TZ ziwe na maandishi ya kiswahili. Wewe ni mtu mpumbavu na mbaguzi sana.
 
Mwarabu akuletee maendeleo? una akili kweli?

Hili ndiyo watu wanakosea huwezi kuletewa maendeleo na mtu au watu wengine!. kitu ambacho tunaweza kunafaika ni uwekezaji na mitaji lakini maendeleo ni kitu kingine. Kuna uwezekano kabisa kukawa na uwekezaji kama Mwadui lakini hatuoni wala kupata chochote na sio ubaguzi wa mwekezaji katoka wapi ni mikataba mibaya ambayo inafanywa na watu wetu wenyewe. Angalia kwa mfano Botswana wanavyo nufaika na Almasi. Tusiingize eti muonekano wa mtu na kujidanganya ndiyo maendeleo!
 
Kwamba miradi Kama ya migodi,kiwanda Cha transformers nk havileti maendeleo Bali kilimo Cha kufa na kupona!?
Kwani miradi ni lazima tuitegemee yote kutoka nje?
Kazi ya kuleta maendeleo Tanzania ni yetu sisi wenyewe kwa shughuli mbalimbali tunazoweza kuzifanya, na siyo kilimo peke yake, ingawa sehemu kubwa ya wananchi wetu wanashughulika na kazi hiyo. Wengi wao wakiifanikisha kazi hiyo, Tanzania itakuwa inapiga hatua kubwa za maendeleo.
Kwa nini tusifanye kila juhudi ili tufanikishe kazi zao kwa maendeleo ya nchi yetu!
 
Umenena Kweli kabisa !!
 
Miaka 61 tangu uhuru,hakuna schemes za maana umwagiliaji,hatujitoshelezi mbolea..zaidi ya porojo siasa ni kilimo,kilimo Cha kufa na kupona nk...tumeshindwa,tunahitaji pesa toka nje(fdi) ili kujongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…