Kwa hiyo FDI ndiyo itakayoleta maendeleo? Hivi huelewi kwamba miaka yote tumekuwa tukipata hizo zinazoitwa fdi, sasa nionyeshe maendeleo tuliyoyapata kutoka na hizo!
Katika 'statement' yako hapo juu, hivi huoni tatizo linapoanzia na kuishia?
Kweli hujui kwa nini katika miaka yote 61 hatujaweza kubadili kwa kiasi kikubwa hali zetu za maisha, hujui; ila unasubiri FDI kwa matumaini makubwa ya kuwaletea maendeleo waTanzania?
Ninajua mara nyingi tunagonganisha vichwa hapa JF, kati yako na mimi, lakini kama hata hili huwezi kujuwa matatizo yetu yapo wapi, nitakushangaa sana.