Ndoa hazivunjiki kwasababu ya kuoa mke bikira ila kwa kuchunguzana au kupelelezana period

Ndoa hazivunjiki kwasababu ya kuoa mke bikira ila kwa kuchunguzana au kupelelezana period

Mwisho kwa wale ambao huwa hatuna huo ujinga wa kuchunguzana we are strong enough kujua kwamba mwanamke au mwanaume hachunguzwi kwakuwa anajua anachofanya,na akiamua kufanya jambo lake anafanya hata humchunguze vipi

Kikubwa tunapenda heshima itawale ndani ya nyumba,mwenza wako asikuonyeshe dalili zozote za kutokuwa mwaminifu,kama mwenza wako anakuheshimu na anakutii basi huna haja haja ya kutafuta mchawi,furahia ndoa yako na muishi kwa furaha na amani

Siku zote naamini uaminifu ni jukumu la mwenza husika,yeye ndio anawajibika kujitunza na kujiheshimu lakini sio wewe kufanya jukumu hilo kwa kumfuatilia na kumchunguza katu hutofanikiwa kamwe! weka hii akilini mwako

Mwisho huwa naamini siku zote bad news hutufikia haraka sana,kama kuna sintofahamu yoyote utaijua tu ila usiitafute


ASANTE
 
Umeandika jambo zuri na kubwa sana.
Nje ya mada: Kama si bikra oa lakini ujue kuwa umepokonya mke wa mtu .
Pili oa hata kama hana bikra ila usitoe mahari
 
Hata Serikali yenyewe inachunguza raia wake kivipi Mume ashauriwe asimchunguze mkewe au vice versa ?

Kama mtu unamlisha unamtunza mnalala wote kitanda kimoja kivipi usimfatilie ? Je kama anampango wa kukuua

Hii dunia usiamini yoyote... nitolee mfano tu, Wa Samson wa kwenye biblia kama angemchunguza Delila basi yamkini yasingemkuta yaliyomkuta.
Yes. Mwanamke ishi naye kijeshi.
La sivyo utakufa mapema umwache aendelee kula vyuku.
 
Usaliti ndio unasababisha ndoa nyingi kuvunjika,hili lipo wazi kabsa
 
Sawa, ndio maana wanawake wengi siku hizi wanakimbia ndoa pia sababu kizazi cha wanaume wa sasa hawajui wajibu wa baba kwenye familia 😃 Hawana mifano mizuri ya wanaume wenye kuuvaa ubaba inavyopaswa. Na wale wenye ndoa nzuri wametulia zao wanakula mema ya nchi huku akina nyie mnalia mitandaoni.
Hao wanawake waokimbia ndoa zao sababu ya waume zao kutovaa majukumu ya ubaba acha wazikimbie tu, kwa sababu leo hii hata mwanaume akiyavaa hayo majukumu ya ubaba ipasavyo Bado tu mwisho wa siku atakuja kuambulia maumivu kutoka kwa huyo mke wake.

Mimi huwa nasema kama Kuna kizazi Cha wanawake ambacho hakistahili kabisa sacrifice zetu sisi wanaume basi hiki kizazi chenu Cha Sasa, kwanza ninaanzaje kuvaa majukumu ya ubaba ilihali wewe mwenyewe hauko tayari kuvaa majukumu ya umama??

Nyie wanawake wa siku hizi kufanya majukumu yenu ambayo kitamaduni ni ya kike huwa mnaita ni utumwa, Sasa kivipi Mimi nifanye majukumu yangu ya kiume??? acha tuishi hivyo hivyo.

Yaani You are not ready to play traditional feminine roles on account that they are slavery roles but you expect me to play traditional masculine duties?...Apparently you ain't ready to be my slave but you highly expect me to slave for you??? How ridiculous it is

Leo mwanaume akiwaoeni nyinyi modern women anakukuta tayari una kazi yako, wote mnakuwa mnafanya kazi kwa kipindi chote Cha ndoa yenu ila hela yako wewe haionekani ndani pesa inayotumika kwenye ujenzi wa familia ni ya kwake kwa mwamvuli wa kwamba eti kuhudumia familia ni jukumu la mwanaume na pesa ya mwanamke huwa haiguswi.....

Haya siku mmevunja ndoa, mnagawana Mali zote kwa 50-50 ambazo kimsingi asilimia kubwa ya pesa iliyotumika kununua Mali hizo ni ya mwanaume, wewe mwanamke pesa yako ulikuwa unapeleka kwenu huko kufanya miradi ya Siri na kuwasaidia ndugu zako....... SASA SI NI USSENGE HUO???

Aisee mtawashika hao hao masimps ambao Bado hawajashtukia huu utapeli mkubwa uliopo kwenye ndoa unaofanywa na nyie modern women Tena kirahisi sana.

Na pia hapa ndani hatulalamiki Bali tunasanuana, kwa mwelevu atayafanyia kazi haya tunayoyandika hapa ila kwa Yale masimps hayataelewa chochote na mtazidi kuyapiga sana kwa kivuli Cha ndoa.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi huu. Nadhani kinamna unaona ninapoelekea. Uwepo wa baba ni muhimu kwa ustawi wa familia. Au kwa kesi ambazo ametangulia mbele za haki, ni muhimu kukawa na mtu wa kiume (yaweza kuwa babu, baba mkubwa, mjomba) ambaye mtoto anamtazamia kuwa mfano wa namna mwanamme au baba anavyopaswa kuwa
Ukizungumzia kesi ya Hakimi na yule mtalaka wake mpaka anafikia hatua ya kudai talaka na kutaka wagawane Mali ni kwamba yule mwanamke alikuwa ameshapanga siku nyingi sana.

Mara kadhaa hata huko nyuma walikuwa wakiitilafiana kidogo sana, yule mwanamke alikuwa anamtishia kwamba atamfilisi na kurudisha nyuma kimaendeleo... Na hapo ndipo Hakimi akapata wazo la kuamisha Mali zake zote kwenye umiliki wa mama yake kwa Siri.

Mwaka Jana mwezi wa pili Kuna mwanamke alimtuhumu Hakimi kwamba amembaka, siku iliyofuata tu mke wake akakimbia mahakamani kwenda kudai talaka..... Mind you hapo Hakimi ndio ametuhumiwa tu Wala haijathibitika bado, lakini mke wake tayari akawa ameshaanza process za kumuacha.

Baadae ikaja kubainika kwamba yule mwanamke alikuwa ni muongo na Wala hakuna ubakaji wowote aliofanyiwa na Hakimi maana alikataa kuonesha ushirikiano kwa waendesha mashtaka.

Hivyo ni wazi kwamba yule ex-wife wa Hakimi alikuwa anasubiri itokee excuse ya kuachana na Hakimi ambapo ndio hiyo ya tuhuma ya ubakaji na ndio maana hata hakusubiri hili aone kama tuhuma za kweli, yeye akakimbilia kuvunja ndoa tu.

Sasa imagine mke wako anakuacha ukiwa kwenye matatizo una kesi nzito inayotishia ustawi wa maisha yako, wakati ndio kipindi ambacho anatakiwa awe karibu na wewe na Tena achukue nusu ya Mali zako.... Hivi kweli mwanamke kama huyo ana roho ya kibinadamu kweli??? Aisee Moja ya siku ambayo nilifurahi sana ni ile siku nilivyoskia kwamba yule yule tapeli haambulii kitu chochote kutoka kwa Hakimi na badala yake yeye ndio anatakiwa amlipe Hakimi.
 
Ewe kijana, chaguzi sahihi ni muhimu. Unaoa mtu anayeona kuwa na trako ndio kila kitu halafu unakuja kulia akisepa na pesa zako. Huyo ndio unayetarajia awe mama wa watoto wako. Mnapanda mbegu sehemu sehemu za ovyo zisizo na rutuba mkitegemea kuvuna mema. Ndoa yenu ni batili toka mwanzo halafu mnategemea mle mema ya ndoa hiyo wakati msingi wa ndoa yako umejenga juu ya mchanga wa bahari
Maneno yenye hekima sana haya

Nyash zimeharibu future za ndoa na familia nyingi sana
 
Siku utakapoanza utakapoacha kumchunga mpenzi wako au mke wako kwa nyakati hizi basi ndio umeanza kuchimba shimo la kaburi lako..........
 
Katika Uislam;
Ndoa ya Kiislamu hukamilika kwa kutekelezwa taratibu zake zote kama ifuatavyo;
a) Kuchagua Mchumba
- Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa, Mtume (s.a.w) amesema:
“Mwanamke anaolewa kwa vitu vinne; kwa Utajiri wake, Hadhi yake, Uzuri wake wa sura na kwa dini yake. Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa dini” (Bukhari na Muslim) - Kwa mujibu wa Hadith hii, Dini ndio sifa ya msingi kuzingatia katika kutafuta mchumba kisha sifa zingine kama elimu, umbo, sura, ukoo, n.k zinafuata. Rejea Qur’an (5:5), (2:221), n.k
- Ni haramu kwa Muislamu kuoa au kuolewa na asiye kuwa muislamu kama kafiri, mshirikina, mkristo, n.k na hata kushiriki katika ndoa na ibada zao pia. Rejea Qur’an (24:26), (9:71), (24:3), n.k

- Si ruhusa kuwaoa Ahlul-Kitaab (Mayahudi na Wakristo) wa zama hizi kwani walikuwa ni wale tu walioamini haki na kuifuata kabla ya kuja Uislamu. Rejea Qur’an (5:5)

- Wachumba wanaruhusiwa kuonana kabla ya kuoana (ndoa) ila katika mipaka ya Uislamu ili kujuana na kuridhiana.

b) Maharimu
- Ni wanaume na wanawake walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur’an na Sunnah.
Wanawake walioharamishwa kuolewa kama walivyobainishwa katika Qur’an (4:22-24) ni hawa ifuatavyo;
1. Mwanamke aliyewahi kuolewa na baba yako.(Babu yako, baba wa baba yako wa kuumeni na kikeni)
2. Mama (mzazi) aliyekuzaa.(Bibi aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa,…)
3. Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa), binti wa kunyonya na mwanao (na kizazi chake)
4. Dada yako khaalisa au wa kwa baba au wa kwa mama
5. Shangazi yako; (dada wa baba yako, na dada wa babu yako).
6. Mama mdogo; (ndugu wa mama yako, au ndugu wa bibi yako).
7. Binti wa ndugu yako mwanamume, khaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa na yeye).
8. Binti wa baba yako khaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
9. Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
10. Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na mama yako au mama yake alikunyonyesha).
11. Mama yake mkeo wa kumzaa (mama mkwe) au wa kunyonyesha (na bibi yake wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha). Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani, mama mdogo wake au shangazi yake (dada yake mkeo) wa kuzaliwa au kunyonya, unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12. Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake).
13. Mke aliyewahi kuolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake), si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.
14. Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Ama akifa mkeo au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake au shangazi yake au mama yake mdogo.
15. Mke wa mtu aliye katika ndoa ni haramu.
Wanawake hawa wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni pia.
Kuna wanawake na wanaodhaniwa ni maharimu lakini si maharimu (si haramu kuwaoa) kisheria. Hawa ni pamoja na mtoto wa baba mdogo, mama mdogo, shangazi, mjomba. Kwa ushahidi wa aya ifuatayo; “……Na (tumekuhalalishia kuwaoa) mabinti wa ami zako na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa dada za mama zako … (Qur'an 33:50).

c) Mahari
Ni kiasi cha mali au kitu anachotoa muoaji kumpa muolewaji kama zawadi (hidaya) kutoka kwa Allah (s.w). Rejea Qur’an (4:4), (5:5). Mahari haina kiwango maalum na ni uhuru wa mwanamke anayeolewa kutoza kiasi apendacho bali, kisiwe kikubwa au kidogo mno. Rejea Qur’an (4:20, 24)

d) Khutuba ya Ndoa
Ni sunnah kusoma khutuba ya ndoa kabla ya kufunga ndoa kama ukumbusho wa kutii maamrisho ya Allah (s.w) kwa wanaooana na waumini kwa ujumla.

Khutuba ya ndoa ina sehemu kuu mbili zifuatazo;
1. Kumhimidi Allah (s.w) kwa sifa zake (maamkizi mema). ii. Shahada zote mbili.
Rejea Qur’an (3:102), (4:1), (33:70-71).

e) Kufunga Ndoa
Ndoa ya Kiislamu hufungika kwa kutekelezwa mambo yafuatayo;

1. Muoaji atekeleze masharti ya kuoa
2. Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa.
3. Pawe na walii au idhini yake.
4. Pawe na mashahidi wawili au zaidi.
5. Pawe na idhini (ridhaa) ya muolewaji.
6. Pawe na Ijabu na Kabuli.

Masharti ya Kufunga Ndoa ya Kiislamu
a) Muoaji atekeleze masharti ya kuoa kama ifuatavyo:-
1. Mke anayemuoa alzima awe muislamu mwema.
2. Awe anaoa kwa hiari yake.
3. Asiwe maharimu wa mke anayetaka kumuoa.
4. Awe amebaleghe na mwenye akili timamu.
5. Asiwe katika Ihramu ya Hija.
6. Asiwe katika ndoa ya wake wanne anaoishi nao katika ndoa.

b) Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa kama ifuatavyo:-
1. Mume anayetaka kumuoa ni lazima awe muislamu mwema.
2. Asiwe katika ndoa ya mume mwingine.
3. Asiwe katika eda ya mume mwingine.
4. Asiwe maharimu wa mume anayetaka kumuoa.
5. Awe muislamu mwema mwenye akili timamu.
6. Asiwe katika Ihramu ya Hija.
7. Awe anaolewa kwa hiari yake.


c) Pawe na Walii au Idhini yake:-
Ndoa ya Kiislamu haswihi mpaka awepo Walii wa binti anayeolewa kwani ndiye mfungishaji wa ndoa au kutoa idhini kwa mtu mwingine mjuzi. Binti hana idhini ya kujiozesha mwenyewe.

Mawalii wanaoweza kuozesha katika Uislamu ni hawa wafuatao;

1. Baba mzazi wa mwanamke anayeolewa.
2. Babu mzaa baba yake.
3. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
4. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.
5. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja (mpwa wake).
6. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.
7. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja na mama mmoja.
8. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja tu.
9. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja na mama mmoja.
10. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja tu.
11. Serikali ya Kiislamu (Hakimu au Kadhi) katika nchi za Kiislamu.
Walii wa daraja ya chini hana ruhusa ya kuozesha kama wa juu yake yupo mpaka apewe idhini.

Masharti na Sifa za Walii ili aozeshe
1. Awe muislamu mwanamume.
2. Asiwe mtumwa (sio watumwa).
3. Awe mwema na mwenye akili timamu.
4. Awe anaozesha baada ya kupatikana idhini ya muolewaji.
5. Awe mwadilifu.

d) Pawe na Mashahidi wawili au zaidi wenye sifa zifuatazo:
1. Wawe watu wazima waliobaleghe, (watoto hawawezi kuwa mashahidi).
2. Wawe na akili timamu.
3. Wawe waislamu wema wanaume.
4. Wawe waadilifu.
5. Wawe waungwana, sio watumwa.

e) Pawe na Ridhaa au Idhini ya mwenye kuolewa
Ndoa ya Kiislamu haiswihi bila idhini ya muolewaji kupatikana. Na idhini yake hupatikana kwa kuwa kimya (kunyamaza kimya). Akikataa ndoa haiswihi.

f) Pawe na Ijabu na Kabuli
- Ijabu; ni maneno anayesema Walii (Muozeshaji) kumwambia mume anayeoa.
Mfano: “Nimekuoza/nimekuozesha Aisha binti Salimu…….”

- Kabuli; ni maneno ya mume anayeoa kukubali kumuoa binti.
Mfano: “Nimekubali kumuoa Aisha binti Salimu……”

- Hivyo, Ijabu ni kauli rasmi anayotoa Walii (muozeshaji) na Kabuli ni kauli rasmi anayotoa mume anayeoa.

Yatakiwa ikiwa mume ameoa na akaona kuwa mkewe si bikira na hali aliuliza au alijulishwa kuwa mwanamke anayo bikira, basi anaweza kuzungumza naye kutaka kujua ukweli wa kupoteza kwake ubikira na anapaswa kumwamini analolisema na kuendelea na ndoa. Vinginevyo anaweza kuamua kukataa kuishi naye kwa sababu anaona atakuwa na wasiwasi kila mara na kumshuku mkewe. Kwa njia hiyo itabidi mume arudishiwe mahari yake. Haya yote ni kwa mujibu wa Uislamu.

Nyie mnaoendelea kulilia bikra endeleeni, tabia ya mke katika ndoa haijengwi na bikra uliyomkuta nayo na bikra ni kitu cha muda tu.

Kwa mantiki hiyo unataka kusema hawa wanawake wenye sifa miongoni mwa sifa za mwanamke kuolewa kwa kupoteza kwao ubikra wasiolewe?
Mashaallah al akhy

Umetukumbusha mambo muhimu sana hapa,shukrani sana.
 
Kinachofanya ndoa ivunjike ni uaminifu,na tabia za mwanamke katika ndoa yenyewe basi, hayo ya bikra hayahusiani kabisa wazee walioa bikra lakin tabia za wake zao ziliwashinda wakawapa talaka.

Ndio maana wakaimba uzuri wa mwanamke sio urembooo ni tabiaaa, hawakuimba uzuri wa mwanamke ni bikiraaaa kwa sababu zamani suala la bikira lilikuwa sio issue mabikira walikuwepo wa kumwaga shida iko kwenye tabia, utaona mwanamke bikra lakini ni mchawi, mchafu, ana matusi hiyo ndoa itadumu???
Hiyo tabiaaa, Ina mchango katika kusababisha Binti mmoja awe na bikira na mwingine asiwe nayo.
 
Hiyo tabiaaa, Ina mchango katika kusababisha Binti mmoja awe na bikira na mwingine asiwe nayo.
Hapana, wengine bikira zao zimetolewa katika mazingira ambayo hawakuruhusu wao, walilazimishwa, kuna dada alitoa ushuhuda humu alibakwa na mjomba wake na kuahidiwa kusomeshwa
 
kuna harakati inasambaa sana mitandaoni siku hizi, inaitwa red pill

ni mambo ya wazungu wazungu

vijana wa kiume wanafundishwa kuchukia wanawake, wanashawishiwa kwamba chanzo kikubwa cha matatizo yao ni wanawake

tuseme ni kama feminism, lakini kwa wanaume

sasa vijana wengi wanatizama haya maudhui kwenye simu janja zao

nadhani ndo chanzo cha kero unayoizungumzia vijana humu kuwa walalamishi sana
Nadhani hii ndo ile KATAA NDOA inapoanzia. Japo sometimes kuna uhalisia wanawake wanazingua sanaa.

Yaani stress niliyopata jana nlitamani nirudi tu nikalale ofisini hizi ndoa za siku hizi kuna mahali wanawake hawafundishwi ndo maana vijana wanaona miyeyusho. Hata umpe 1M kila wiki still atakuzingua tu.
 
Thamani ya mwanamke ni bikra
kwanza kuna asilimia kubwa ya kuridhika na wewe sababu hana reference point bikra ni zawadi kwa mwanaume kutoka kwa mwanamke
bikra ina thamani kubwa sana Oa mwanamke bikra utapata Amani ya nafsi huyo atakua Mali yako wewe
 
Bikira zetu bado mtupangie matumizi,, aaaaaarrrrrrgggghh tuacheni hukoooo
 
Huu uzi naundika mahususi kwa kwasababu ya mdau mmoja ambaye anatupigia sana makelele hapa jukwaani kuhusiana na mwanamke bikira,kwa mtazamo wake anaona mwanamke bikira ndio sababu ya utengamano wa ndoa kitu ambacho si kweli kwa asilimia mia moja

Kwanza ieleweke sio kwamba hatupendi wanawake wajitunze mpaka siku ya ndoa laa! Tunapenda sana na kila mzazi angependa mabinti zake waolewe katika hali hiyo na hii inawezekana kama jamii ikiweka sana mkazo katika elimu ya dini na mila na desturi zikilindwa.

Mfano Lesotho sasa hivi kila mwaka wanafanya sherehe za kuwatunuku vyeti mabinti ambao wako bikira ambao wametimiza miaka 25,wanapimwa na kupewa vyeti rasmi,kwahiyo kumbe haya yakifanywa katika jamii inawezekana kabisa

Sasa tuje upande wa pili wa shilingi,kuoa mwanamke bikra hakukupi asilimia mia moja kwamba huyo mwenza wako atakuwa mwaminifu kwa asilimia mia,na hii ni kutokana na mfumo wa maisha ambao tunao sasa,hii sayansi na tekinolojia imekuja na faida na hasara zake

Vishawishi ni vingi mno huko mitandaoni,mambo ya chumbani sasa hivi yapo mitandaoni kwahiyo watu hupenda kujaribu mambo mapya,kwahiyo hata huyo bikira wako nae hajapona juu ya hili,maana naye anashawishiwa kula muogo wa shamba moja kila siku huchoki ebu jaribu bwana muhogo wa jang'ombe,je hapo hajaliwa?

Huko nyuma sio kwamba mababu zetu pamoja na kuoa mabikira sio kwamba hawaja chapiwa laa! Ila hakukuwa na nyenzo za kuchunguzana na kukamatana haraka kwakuwa mpaka umjue mgoni wako basi ufanye kazi kweli

Istoshe wazee wetu walijua haya mambo yapo lkn walijitahidi kadri ya uwezo wao kuepusha ndoa kuvunjika,wazee wakirudi nyumbani kutoka safari,basi hawaendi makwao moja kwa moja ila watatuma mtoto wa jirani apeleke koti nyumbani ikiwa na ishara kwamba amerudi,hivyo kama hapo kwake kuna sintofaahamu yoyote basi asiikute,naam ndio maana waliishi kwa amani na starehe

Sisi karne hii hizi simu ndio mvunjaji wa kwanza wa ndoa zetu,siku hizi tunafumaniana kupitia meseji,halafu cha ajabu eti meseji ndio inavunja ndoa,hivi tupo serious kweli? Yaan umetumia gharama kubwa kuoa,kumchagua mchumba,kumhudumia halafu siku moja tu inaingia meseji halafu ndoa inakuwa hakuna tena,ni aibu kubwa

Hivi kama tukiacha kuchunguzana katika simu unafikiri ndoa hazitadumu? Kwa maono yangu kuna sababu nyingi sana za watu kuchepuka,ukosefu wa mapenzi,kutopeana mda kumfanya mwenzio kuwa mpweke na hakuna kitu kibaya kama kuwa mpweke katika ndoa,kutokuwepo kwa maelewano na ugomvi kila mara,kutopeana haki ya tendo la ndoa na mambo kadha wa kadha

Kwahiyo tusijidanganye kuchepuka kutakuwepo tu iwe umeoa bikra au sio bikra,na bikra mzuri ni yule ambaye amejitunza mpaka ndoa,kama ulimtoa bikra kabla ya ndoa wala usijisifu kwakuwa sio mcha mungu,ni mcha mungu pekee ndio ana nafasi kubwa ya kutochepuka kwakuwa ana hofu ya Mungu,lakini bikra yake sio dhamana ya uaminifu wake,ingawa kidogo ana uhafadhali

Ukitaka kudumu katika ndoa mheshimiane yaani msitengenezeane mazingira ya kuwa na mashaka,muaminiane hiyo ndio silaha kubwa sana,mkiaminiana hata kuwekeana soft ware za kuchunguzana hamtafanya,ila mkitaka kuachana fasta endekezeni kupekuana simu zenu na kuwekeana hizo soft ware zenu nipo pale nawazoom mtaendelea kulialia mpaka kiama

Ni hayo tu!
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom