Katika Uislam;
Ndoa ya Kiislamu hukamilika kwa kutekelezwa taratibu zake zote kama ifuatavyo;
a) Kuchagua Mchumba
- Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa, Mtume (s.a.w) amesema:
“Mwanamke anaolewa kwa vitu vinne; kwa Utajiri wake, Hadhi yake, Uzuri wake wa sura na kwa dini yake. Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa dini” (Bukhari na Muslim) - Kwa mujibu wa Hadith hii, Dini ndio sifa ya msingi kuzingatia katika kutafuta mchumba kisha sifa zingine kama elimu, umbo, sura, ukoo, n.k zinafuata. Rejea Qur’an (5:5), (2:221), n.k
- Ni haramu kwa Muislamu kuoa au kuolewa na asiye kuwa muislamu kama kafiri, mshirikina, mkristo, n.k na hata kushiriki katika ndoa na ibada zao pia. Rejea Qur’an (24:26), (9:71), (24:3), n.k
- Si ruhusa kuwaoa Ahlul-Kitaab (Mayahudi na Wakristo) wa zama hizi kwani walikuwa ni wale tu walioamini haki na kuifuata kabla ya kuja Uislamu. Rejea Qur’an (5:5)
- Wachumba wanaruhusiwa kuonana kabla ya kuoana (ndoa) ila katika mipaka ya Uislamu ili kujuana na kuridhiana.
b) Maharimu
- Ni wanaume na wanawake walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur’an na Sunnah.
Wanawake walioharamishwa kuolewa kama walivyobainishwa katika Qur’an (4:22-24) ni hawa ifuatavyo;
1. Mwanamke aliyewahi kuolewa na baba yako.(Babu yako, baba wa baba yako wa kuumeni na kikeni)
2. Mama (mzazi) aliyekuzaa.(Bibi aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa,…)
3. Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa), binti wa kunyonya na mwanao (na kizazi chake)
4. Dada yako khaalisa au wa kwa baba au wa kwa mama
5. Shangazi yako; (dada wa baba yako, na dada wa babu yako).
6. Mama mdogo; (ndugu wa mama yako, au ndugu wa bibi yako).
7. Binti wa ndugu yako mwanamume, khaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa na yeye).
8. Binti wa baba yako khaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
9. Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
10. Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na mama yako au mama yake alikunyonyesha).
11. Mama yake mkeo wa kumzaa (mama mkwe) au wa kunyonyesha (na bibi yake wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha). Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani, mama mdogo wake au shangazi yake (dada yake mkeo) wa kuzaliwa au kunyonya, unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12. Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake).
13. Mke aliyewahi kuolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake), si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.
14. Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Ama akifa mkeo au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake au shangazi yake au mama yake mdogo.
15. Mke wa mtu aliye katika ndoa ni haramu.
Wanawake hawa wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni pia.
Kuna wanawake na wanaodhaniwa ni maharimu lakini si maharimu (si haramu kuwaoa) kisheria. Hawa ni pamoja na mtoto wa baba mdogo, mama mdogo, shangazi, mjomba. Kwa ushahidi wa aya ifuatayo; “……Na (tumekuhalalishia kuwaoa) mabinti wa ami zako na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa dada za mama zako … (Qur'an 33:50).
c) Mahari
Ni kiasi cha mali au kitu anachotoa muoaji kumpa muolewaji kama zawadi (hidaya) kutoka kwa Allah (s.w). Rejea Qur’an (4:4), (5:5). Mahari haina kiwango maalum na ni uhuru wa mwanamke anayeolewa kutoza kiasi apendacho bali, kisiwe kikubwa au kidogo mno. Rejea Qur’an (4:20, 24)
d) Khutuba ya Ndoa
Ni sunnah kusoma khutuba ya ndoa kabla ya kufunga ndoa kama ukumbusho wa kutii maamrisho ya Allah (s.w) kwa wanaooana na waumini kwa ujumla.
Khutuba ya ndoa ina sehemu kuu mbili zifuatazo;
1. Kumhimidi Allah (s.w) kwa sifa zake (maamkizi mema). ii. Shahada zote mbili.
Rejea Qur’an (3:102), (4:1), (33:70-71).
e) Kufunga Ndoa
Ndoa ya Kiislamu hufungika kwa kutekelezwa mambo yafuatayo;
1. Muoaji atekeleze masharti ya kuoa
2. Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa.
3. Pawe na walii au idhini yake.
4. Pawe na mashahidi wawili au zaidi.
5. Pawe na idhini (ridhaa) ya muolewaji.
6. Pawe na Ijabu na Kabuli.
Masharti ya Kufunga Ndoa ya Kiislamu
a) Muoaji atekeleze masharti ya kuoa kama ifuatavyo:-
1. Mke anayemuoa alzima awe muislamu mwema.
2. Awe anaoa kwa hiari yake.
3. Asiwe maharimu wa mke anayetaka kumuoa.
4. Awe amebaleghe na mwenye akili timamu.
5. Asiwe katika Ihramu ya Hija.
6. Asiwe katika ndoa ya wake wanne anaoishi nao katika ndoa.
b) Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa kama ifuatavyo:-
1. Mume anayetaka kumuoa ni lazima awe muislamu mwema.
2. Asiwe katika ndoa ya mume mwingine.
3. Asiwe katika eda ya mume mwingine.
4. Asiwe maharimu wa mume anayetaka kumuoa.
5. Awe muislamu mwema mwenye akili timamu.
6. Asiwe katika Ihramu ya Hija.
7. Awe anaolewa kwa hiari yake.
c) Pawe na Walii au Idhini yake:-
Ndoa ya Kiislamu haswihi mpaka awepo Walii wa binti anayeolewa kwani ndiye mfungishaji wa ndoa au kutoa idhini kwa mtu mwingine mjuzi. Binti hana idhini ya kujiozesha mwenyewe.
Mawalii wanaoweza kuozesha katika Uislamu ni hawa wafuatao;
1. Baba mzazi wa mwanamke anayeolewa.
2. Babu mzaa baba yake.
3. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
4. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.
5. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja (mpwa wake).
6. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.
7. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja na mama mmoja.
8. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja tu.
9. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja na mama mmoja.
10. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja tu.
11. Serikali ya Kiislamu (Hakimu au Kadhi) katika nchi za Kiislamu.
Walii wa daraja ya chini hana ruhusa ya kuozesha kama wa juu yake yupo mpaka apewe idhini.
Masharti na Sifa za Walii ili aozeshe
1. Awe muislamu mwanamume.
2. Asiwe mtumwa (sio watumwa).
3. Awe mwema na mwenye akili timamu.
4. Awe anaozesha baada ya kupatikana idhini ya muolewaji.
5. Awe mwadilifu.
d) Pawe na Mashahidi wawili au zaidi wenye sifa zifuatazo:
1. Wawe watu wazima waliobaleghe, (watoto hawawezi kuwa mashahidi).
2. Wawe na akili timamu.
3. Wawe waislamu wema wanaume.
4. Wawe waadilifu.
5. Wawe waungwana, sio watumwa.
e) Pawe na Ridhaa au Idhini ya mwenye kuolewa
Ndoa ya Kiislamu haiswihi bila idhini ya muolewaji kupatikana. Na idhini yake hupatikana kwa kuwa kimya (kunyamaza kimya). Akikataa ndoa haiswihi.
f) Pawe na Ijabu na Kabuli
- Ijabu; ni maneno anayesema Walii (Muozeshaji) kumwambia mume anayeoa.
Mfano: “Nimekuoza/nimekuozesha Aisha binti Salimu…….”
- Kabuli; ni maneno ya mume anayeoa kukubali kumuoa binti.
Mfano: “Nimekubali kumuoa Aisha binti Salimu……”
- Hivyo, Ijabu ni kauli rasmi anayotoa Walii (muozeshaji) na Kabuli ni kauli rasmi anayotoa mume anayeoa.
Yatakiwa ikiwa mume ameoa na akaona kuwa mkewe si bikira na hali aliuliza au alijulishwa kuwa mwanamke anayo bikira, basi anaweza kuzungumza naye kutaka kujua ukweli wa kupoteza kwake ubikira na anapaswa kumwamini analolisema na kuendelea na ndoa. Vinginevyo anaweza kuamua kukataa kuishi naye kwa sababu anaona atakuwa na wasiwasi kila mara na kumshuku mkewe. Kwa njia hiyo itabidi mume arudishiwe mahari yake. Haya yote ni kwa mujibu wa Uislamu.
Nyie mnaoendelea kulilia bikra endeleeni, tabia ya mke katika ndoa haijengwi na bikra uliyomkuta nayo na bikra ni kitu cha muda tu.
Kwa mantiki hiyo unataka kusema hawa wanawake wenye sifa miongoni mwa sifa za mwanamke kuolewa kwa kupoteza kwao ubikra wasiolewe?