Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
pia kwenye ndoa nimejifunza kwamba, ukighafirika kwa lolote, pambana jua lisichwe na uchungu moyoni mwako. fanya juu chini, kama kutubu kwa mwenzako tubu, mwambie nisamehe, na wewe ukiombwa msamaha samehe haraka ili uchungu uondoke mioyoni mwenu. Neno msamaha ni nguzo kwenye ndoa, na Yesu mwenyewe ambaye ndiye msingi wenu anatuhitaji tusameheane. why? kwenye ndoa mkigombana sasaivi, kadiri dakika na masaa yanavyozidi kuendelea, hasira na visasi huwa vinazidi kuongezeka, shetani huwa amekaa pembeni anachochea kuni. hivyo madhara ya ugomvi wa masaa machache ni madogo kuliko madhara ya ugomvi wa siku moja mbili na kuendelea. na mwisho wa siku mtakuja kupatana na mnashangaa kwanini tumeraruana namna hii si tungepatana tu palepale dakika zilezile ili madhara haya yasifikia kiwangu hiki?
WAEFESO 4:26 INASEMA: we na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 wala msimpe Ibilisi nafasi.
WAGALATIA 6:1 - 10 INASEMA: 1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. 3 Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. 4 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. 5 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.
6 Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote. 7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. 9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. 10Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.