Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

wakuu msaada juu ya hili
jana nilifanya kitu ambacho ni chukizo kwa mungu sasa kila siku kabla ya kulala huwa nasoma neno na kusikiliza gospel songs ila jana sikufanya sala kabisa sababu nilifanya chukizo
kabla sijalala nilijiwekea kauli kichwani nataka kutafakari juu ya kile nilichokifanya na pia nifanye maamuz na mustakabali wangu
badae nilipitiwa na usingizi , niliota ndoto nipo safarini nikafika mahali nipumzike kwenye mji wa watu nikapokewa vizuri tu na nikaishi nao vizuri tu wenyeji wangu walikuwa vijana wa rika langu baadae nikaanza safari ya kuelkea huko niendako wakati wananisindikiza nikajipapasa sina simu na suruali ambayo nilihifadhia iyo simu haikuwamo kwenye begi langu la mgongoni na wao wakawa wananishangaa nilojiona mzembe fikra zangu zikawa zinaniambia nguo iko mahali fulani ila namna ya kuipata siwezi nilishtuka toka usingizini nikawa naitafakari juu ya hii ndoto naomba mnisaidie juu ya hili
 
Jamani msiunganishe uzi huu nina maana yangu.

Habari ndugu zangu.

Nimeota ndoto kuwa nipo safarini kwenye basi ambapo kulikuwa na abiria mbalimbali. Baada ya muda nikaota nipo ndani ya gari kama Land cruiser nyeupe tupo wengi ndani na tunavuka mto wenye daraja la mbao. Daraja lilikuwa jembamba dereva akawa anakosa balance na baada ya muda likaenda pembeni na kudumbukia mtoni.. nilitoka salama na sikuwa na wasiwasi wowote.

Kuna baadhi ya matukio nimeyasahau lakini mambo ya msingi ninayoyakumbuka katika ndoto ni hayo.

Naombeni tafsiri ya ndoto hii kwa wenye uwezo huo wa kutafsiri..

Nawakaribisha pia Mla panya na Freedom tomorrow na Divine
 
Kwanini unataka tafsiri Mkuu, Bible yenyewe inasema MTU huota Yale anayowaza na kuchangia na uchovu!
 
serious ndugu zangu nikaribishieni wanaofahamu tafsiri
 
Ndoto ubakia ni ndoto. Mpaka pale itakapotokea kweli. Ndo itakuwa sio ndoto.
Acha uoga. Muda uamue.
 
Kwanini unataka tafsiri Mkuu, Bible yenyewe inasema MTU huota Yale anayowaza na kuchangia na uchovu!

Umesema ni BIBLE imesema uliyoyasema.....je, kama mtu si muumini wa hizi dini (Uislam, Ukristo) tulizoletewa na watawala wetu?
 
Hapo Mkuu kwakweli sijui! Ila nimesema hicho kitabu maana ndo muumini wacho! Kama mtu siyo wa hivyo vitabu vya dini aende kwenye science aone inasema nini kuhusiana na ndoto!
 
Hakuna kitu ni matukio ya ajali iliyotokea singida na moshi juzi, inaonekana uliyatafakali sana ubongo ukaweka kumbukumbu.
Ndoto ni njia ya kusafisha ubongo kwa baadhi ya matukio tuliyoyashuhudia au kusimuliwa.
 
hebu kumbuka hayo mengine uliyosahau ili tukupe tafsiri halisi ya ndoto yako tusije tafsiri nusu.
 
unakumbuka ile ndoto ya yule mbunge ilivyomletea taabu ? naogopa kuota !!!!
 
Haya mambo ni magumu sana....mimi nimefikisha ndoto zipatazo kumi ambazi kila nikiota hiwa nakosa maana yake alafu ndani ya wiki husika linakuja kutokea tukio lenye uhusiano na ndoto niliyoiota....mwezi uliopita niliota nimeokota kito cha thamani baada ya siku kadhaa nikaja kugundua kimepotea hazikuoita siku tatu nikakutana na jamaa wawili wakiwa wameruhusiwa kutoka hosp. mmoja wapo akiwa amefanyiwa upasuasi wa mshipa wa ngiri wakaniita kwa upole na kunieleza maswaibu yao ambapo walikua hawana ndugu wala jamaa mji huu hivyo hawakua na pakuelekea nikawachukua mpaka kwangu tukakaa siku mbili siku ya tatu mgonjwa hali ikabadirika ghafla kumrudisha hosp. kesho yake mchana akafariki dunia. Kwa nilicho kishuhudia usije ukarogwa/jaribu kuchukua mtoto wa mtu kwao eti mkatafute maisha ni zaidi ya hatari
 
Jamani msiunganishe uzi huu nina maana yangu.

Habari ndugu zangu.

Nimeota ndoto kuwa nipo safarini kwenye basi ambapo kulikuwa na abiria mbalimbali. Baada ya muda nikaota nipo ndani ya gari kama Land cruiser nyeupe tupo wengi ndani na tunavuka mto wenye daraja la mbao. Daraja lilikuwa jembamba dereva akawa anakosa balance na baada ya muda likaenda pembeni na kudumbukia mtoni.. nilitoka salama na sikuwa na wasiwasi wowote.

Kuna baadhi ya matukio nimeyasahau lakini mambo ya msingi ninayoyakumbuka katika ndoto ni hayo.

Naombeni tafsiri ya ndoto hii kwa wenye uwezo huo wa kutafsiri..

Nawakaribisha pia Mla panya na Freedom tomorrow na Divine
Tafsiri yake ni kwamba mwanamke wako anatembea na jirani bodaboda ila huyo kijana hana ukimwi ndio maana ulipona. Mtoto atakaezaliwa ni wa huyo bodaboda. Huyo bodaboda ni mweupe na anapenda usafi sana kibaya tu hatumii kondom
 
Mkuu;
Japo hukuniweka kwa hao wataalam wako ila nakusaidia ki hivi:
Gari ni chombo cha huduma. Hivyo ulivyoota kuwa uliingia kwenye hayo magari ni kuwa; Upo kwenye huduma flani kubwa (Bus) lakini katika hiyo safari ukajikuta mmeingia landcruiser (huduma ikapunguzwa). Mkaendelea mbele kumbe daraja sio imara na sio la kutegemea. Mkatumbukia kwenye maji.
Kutokana na huduma unayoifanya, mbele na muda sio mrefu, mtapunguzwa wengi japo utabaki lakini mda sio mrefu hata wewe utakosa kazi. Tena bila malipo
 
Nashukuru ndugu kwa tafsiri yako
 
Haya mambo ni magumu sana....mimi nimefikisha ndoto zipatazo kumi ambazi kila nikiota hiwa nakosa maana yake alafu ndani ya wiki husika linakuja kutokea tukio lenye uhusiano na ndoto niliyoiota....mwezi uliopita niliota nimeokota kito cha thamani baada ya siku kadhaa nikaja kugundua kimepotea hazikuoita siku tatu nikakutana na jamaa wawili wakiwa wameruhusiwa kutoka hosp. mmoja wapo akiwa amefanyiwa upasuasi wa mshipa wa ngiri wakaniita kwa upole na kunieleza maswaibu yao ambapo walikua hawana ndugu wala jamaa mji huu hivyo hawakua na pakuelekea nikawachukua mpaka kwangu tukakaa siku mbili siku ya tatu mgonjwa hali ikabadirika ghafla kumrudisha hosp. kesho yake mchana akafariki dunia. Kwa nilicho kishuhudia usije ukarogwa/jaribu kuchukua mtoto wa mtu kwao eti mkatafute maisha ni zaidi ya hatari
Ndoto za kusafiri ndani ya basi zimekuwa nyingi mno kiasi nashindwa kuelewa kwa nini
 
gari ni tz, dereva unamjua, weupe wa gari ni utajiri wa tz, daraja ni changamoto inazopitia tz kwa sasa, abiria ni watz, kupinduka kwa gari ni future mbaya kwa dereva, wewe kutoka salama kwenye mpinduko ni mambo hayo hayataathiri maisha ya kawaida. (NIMETANIA TU)
 
Wakuuu poleni na majukumu
Ninayo ndoto ambayo imejirudia mara ya tatu sasa kwa vipindi tofauti.

Ninaota nimepotea njia na njia ni ileile.

Imefikia mda nmetafakari nimeshindwa kuelewa, mwaweza nisaidia kuielewa.

Ahsanteni
 
Back
Top Bottom