Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Mgombea wa ccm anatumia kilugha kuomba kura na pia ameishia wapiga kura kwamba atawashughulikia, atowaletea maendeleo wasipomchagulia awatakao hapa tume inasemaje kwa mgombea mbaguzi Kama huyu
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC Online
Tume wamepewa maelekezo sasa naona yanawatokea puani. CCM maskini wanazidi kujichanganya hakuna kosa kubwa kama hili walilolifanya la kumita Lissu wanazidi kumpaisha aisee akili za kuambiwa changanya na za kwako..
 
Wananchi tulikubali kuwa tuwe na tume ya uchaguzi sasa tume ikifanya kazi yake ipasavyo mnakuja kulialia kuwa wananchi hamheshimiwi. Basi hakuna haja ya kuwepo kwa tume uchaguzi uongozwe kwa matakwa ya chadema.

Isiwepo na uchaguzi wenyewe pia usiwepo. Hiyo ni bora zaidi kuliko kutufanyia kiini macho cha demokrasia.
 
Umeona watu wanatumia Precision kama ilivyokuwa fast jest? Kwani kodi walisema hawalipi au ni nyie figisu zenu ili ndege zenu zisikose wateja. Mbaya zaidi na msivyoweza kuwaza wao wameondoka na nyie bado mmekosa wateja wao maana gharama zenu ni kubwa sana. Bila shaka hilo shirika litakufa kama ilivyokufa uda na mwendo kasi unapoelekea sasa hivi. Hiyo SGR subiri tuone kama haitakuwa majanga
Kwaiyo mkuu unafurahi kweli kweli kuona ndege zilizonunuliwa kwa kodi yako zinakosa wateja? Kuwa mzalendo comrade
 
Km ina double standard kwann mnashiriki uchaguzi?
Acheni ufala!
Kwa sababu ni haki ya kikatiba,but mtachezea kichapo na tume yenu, Hakuna kura hata moja itakayoibiwa this time.
Uzuri polisi mliwatelekeza miaka 5 awapo upande wenu
 
Wanafiki ninyi msionadi sera za chadema mnaowashamulia wagombea wengine kwa majina kinyume na maadili ya uchaguzi
Unafiki unao wewe msaka uteuzi uliyejitoa fahamu mpaka kutokuona kuwa polepole kawaita wapinzani misukule lakini NECCCM Tumeccm ha watathubutu kumhoji
 
Fafanua vizuri comrade.
Ina maana wagombea wa upinzani pekee ndo awajui kujaza formu,yule mgombea wa ccm mbona anatumia kilugha na pia kutisha wapiga kura wasipowachagua anaowataka atawashughulikia, hapa tume imekuwa kiziwi mbona.
 
Wangejua wanampa kiki sana.

Haijawahi kutokea tangu kuwepo vyama vingi tume kuita mgombea urais eti kwa kutoa lugha mbaya dhidi ya wagombea wengine.

Jambo hili kwa wananchi wa kawaida hawataelewa maana yake ni nini hasa wakikumbuka jinsi Mzee Lowasa alivyodhalilishwa mwaka 2015 kisa alikuwa upinzani.

Any way,naona kama uchaguzi huu mwamuzi ni Mungu
 
Lisu asijaribu kuwaamini watu hawa, kama kuna mwanachadema humu mfikishieni taarifa aongeze ulinzi wake binafsi,msije kusema hamkuambiwa.Kuna watu nasikia wamekasirika kiasi cha kuwatoa watu maofisini kuja kujibu hoja za Lisu,watu hao ni. OR tamisemi,polepole,msemaji wa serikali, mahera wa NEC wametolewa kuja kujibu hoja zinazoitwa za kichochezi za mgombea urais Chadema
 
Back
Top Bottom