Next on Straight Talk Africa: Tundu Lissu alongside Professor Lumumba - PLO


Kwa angle hii nimekuelewa. Acha tusubiri mjadale wenyewe,pengine tutapata picha halisi ya unachokiongea hapa.
 
mtumeni chakubanga au kheri james kwa nafasi la Lumumba
 
Hata ningekuwa mimi ningechafua tu, li nchi lililonipiga risasi 16 bado niendelee kulipaka rangi nzuri? Nehi. Ila nikwambie kitu msipende kuona ukweli ni kuchafua nchi mi nasubiri kusikiliza ya ukweli natabeba ya uongo natupa kule, kwa mfano watu waliaminishana hakuna korona wakati watu wanadondoka kwa wingi watawala wanajificha kwenye changamoto ya upumuaji
 
Nini maana ya kuchafua nchi ?
 
Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu sana. Kesho tutajua kama mama atafagilia uhuru huo ataendeleza uminywaji wa uhuru huo.
Mimi ninacho amini ,hata kama mama atakuwa na madhaifu namna gani,lakini kamwe hata kaa amfikie Jiwe kwa ukatilia aliotutenda.Kunaweza kuwa na mapungufu lakini hayawezi kufikia mapungufu ya regime iliyopita;Watu kuuwawa,watu kupotezwa,watu kupigwa risasi ,watu kutekwa,watu kubambikiwa kesi.Hayo yote yamefanyika bila hata uchunguzi wa kimagumashi kufanyika.Upendeleo wa waziwazi 'double standard',Ukabila na ukanda.Yaani maovu ya Jiwe ni mengi sana.Jiwe hajawahi kufuata hii katiba ya JMT wala sheria za nchi hata kwa asilimia 20% pamoja na mapungufu yote yaliyoko kwenye hiyo katiba.Kiufupi Jiwe alikuwa 'above the law'.Alikuwa juu ya mihimili yote mitatu!
 
Tunakumbushana tu na wala isiwe nongwa.

Taifa liko kwenye Maombolezo ya siku 21 hivyo ni vema tukajikita kwenye maombolezo na kumuombea mwendazake.

Sitashangaa kama mh Dr Diallo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na Waziri mstaafu atazuia kurushwa kwa mahojiano hayo ya akina Tundu Lisu yatakayokuwa mubashara.

Ki zama na kitabu chake

Maendeleo hayana vyama!
 
atazuia dstv?
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Kama Radioni tu, wanakata hata visehemu vya taarifa ya habari ambayo walikuwa hawajui kitasemwa nini, sembuse hicho kipindi ambacho wanajua kitakacho ongelewa!
 
Mwanadamu huwa anajiandalia makao yake ya baadaye angali hai. Sasa kusubiri kuombewa baada ya kufariki, hilo ni tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…