mmmh! Mm nina digrii ya nutrition,nisome hyo ya nursing? Naona hata kaz zake ziko za kumwaga! Mana nahangaika kutafuta kaz sipati
Afande Narubongo,lol. Hata mimi mpaka leo sijaamini kwamba kweli naenda huko...but I have this feeling that something has got to change in our country's system. I want to be a part of that change..I wanted to join the education system but sijui kwa nini nimevutiwa (kwa sasa) na polisi. Maybe, sitabadilisha kitu..but untill that happens, nitaenda and see for myself!
Karibu mkuu..it is our country, sote tukikata tamaa..tutaiuza nchi!??
safi sana kaka maana hata mimi sasa hivi nikiona mtu amevaa gwanda za polisi huwa moyo unaniruka na pia nikifikiria sana ni kwamba pale polisi na kwa degree yangu ndio mahala pake, hatuwezi kwenda UK kutafuta mtu aliyesambaza email chafu wakati sisi tupo na fani zetu tumezidivert kwa kuendekeza fedha kwenye mashirika ya wazungu, nilisikia mchakato wa degree holder huwa unaapply direct makao makuu. Nimeanza kukusanya nyaraka za muhimu kabla ya kupata baraka za wazazi
Yep..kwa degree holder kuendelea unaaply makao makuu..hawa wengine ni mikoani.
Kwa kweli hata mimi sikuwa nawapenda hii ni kutokana na ukweli kwamba polisi na ualimu wanaenda waliofeli...mimi nataka kubadili hili.
Na kama kweli ni hivyo basi hawa tukiwatoa watapunguza undezi tunaouona huko!
Kuhusu babraka za wazazi; mpaka sasa baba ananiambia hana amani..ila kadri siku zinavyozidi kwenda anaelewa mtazamo wangu!!!
asante mkuu nimekupata sawaasawaa!......TGS A hadi C ni kiwango cha watumisha kwa watumishi wa serikali wanaoanza kazi bila kuwa na shahada. Hiyo TGS D ndo wale wanaoitwa maafisa pindi wanapoanza kazi ingawa hata wasiokuwa na shahada wanaweza panda toka A hadi G ambayo huwa ndio kiwango chao cha mwisho hawawezi kupanda zaidi ya hapo labda wawe wamepewa madaraka (sio cheo).
Kwa government system, mshahara wa TGD D huanzia around 470,000/= kwa mwezi na kwa TGD E huanzia 600,000. Hii haiwahusu walimu na madaktari. Kwa engineers wote including ARDHI degrees wao wanapoanza kazi huanzia na TGS E na kwa degree nyingine zote huwa wanaanza na mshahara wa TGS D upon first employment na Government. kwa wenye degree mshahara ya hupanda hadi kufikia TGS H amabapo ili kwenda TGS I, ni lazima upate cheo cha madaraka (i.e uwe mkuu wa idara, mkurugenzi etc, hii haiwahusu wakurugenzi wa mashirika ya umma yanayojitegemea kama tanesco, TBS, TANAPA, Ngorongoro TRA etc. wao wana mifumo yao ya mishahara ambayo ni mikubwa kuliko ya watumishi wa wizara za serikali na halmashauri ambao ndiyo wanaotumia mfumo wa TGS)
Unapokuja kwenye TGS I, hivyo ni viwango vya mishahara vinavotokana na madaraka km ukiwa mkuu wa idara serikalini basi mshahara wako ndo utaanzia na TGS I au ukiwa na cheo cha Principal, mshahara wako walau utaanzia na TGS I. Hao unaowasikia wakuu wa idara za wizara wote mishahara yao huanzia hapa ambao ni around 1,400,000/=.
Hope mpaka hapa utakuwa umepata mwanga kidogo.