TGS A hadi C ni kiwango cha watumisha kwa watumishi wa serikali wanaoanza kazi bila kuwa na shahada. Hiyo TGS D ndo wale wanaoitwa maafisa pindi wanapoanza kazi ingawa hata wasiokuwa na shahada wanaweza panda toka A hadi G ambayo huwa ndio kiwango chao cha mwisho hawawezi kupanda zaidi ya hapo labda wawe wamepewa madaraka (sio cheo).
Kwa government system, mshahara wa TGD D huanzia around 470,000/= kwa mwezi na kwa TGD E huanzia 600,000. Hii haiwahusu walimu na madaktari. Kwa engineers wote including ARDHI degrees wao wanapoanza kazi huanzia na TGS E na kwa degree nyingine zote huwa wanaanza na mshahara wa TGS D upon first employment na Government. kwa wenye degree mshahara ya hupanda hadi kufikia TGS H amabapo ili kwenda TGS I, ni lazima upate cheo cha madaraka (i.e uwe mkuu wa idara, mkurugenzi etc, hii haiwahusu wakurugenzi wa mashirika ya umma yanayojitegemea kama tanesco, TBS, TANAPA, Ngorongoro TRA etc. wao wana mifumo yao ya mishahara ambayo ni mikubwa kuliko ya watumishi wa wizara za serikali na halmashauri ambao ndiyo wanaotumia mfumo wa TGS)
Unapokuja kwenye TGS I, hivyo ni viwango vya mishahara vinavotokana na madaraka km ukiwa mkuu wa idara serikalini basi mshahara wako ndo utaanzia na TGS I au ukiwa na cheo cha Principal, mshahara wako walau utaanzia na TGS I. Hao unaowasikia wakuu wa idara za wizara wote mishahara yao huanzia hapa ambao ni around 1,400,000/=.
Hope mpaka hapa utakuwa umepata mwanga kidogo.