Tangu kuanzishwa kwa JamiiForums mwaka 2006 hadi ilipobadilishwa kuwa JamiiAfrica 2025, nguvu kubwa ya mtandao huu ipo kwenye usiri wa utambulisho wa members(anonymity).
Uchangiaji unakuwa bora zaidi maana members tunakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yetu, kukosoa,kukejeli, kupinga, kupongeza n.k inasadifu slogan ya
where we talk openly.
Kama kwa namna yoyote ile u-anonymity huu utaondolewa kwa kuleta mfumo wa kuweka jina halisi, picha, eneo mhusika alipo n.k wengi nadhani tutaikimbia JamiiAfrica ama italazimika tujipange upya!
Mshangazi dot com aliwahi kusema
"JF unaweza kubishana hata na babamkwe na ukamshinda bila nyie kujuana..."
Heshima mbele wakuu,
Nawasilisha.