Ni chakula gani watu wanakipenda lakini wewe hujawahi kukielewa kabisa?

Naheshimu vyakula vyote maake ndo vilivyo wakuz wengi wetu humu

Mimi nakula ama napenda zaidi

Ugali nyama/ samaki/ dagaa/ mboga za majani tuseme karibu zote nakula japo kisamvu nyumbn hakijawah pikwa , mlenda hapana kwakweli kula bamia ilinichukua muda kidg

Chapati hata tano namaliza,

Pilau aseeh sitaki kusema

Ndizi nyama, ama maharage plus viazi,

Wali siupendi kivile,


Sasa ukija vyakula sijui pizza Baga, biryani chips aseeh sijawahi vielewa hivi vyakula
 
Mpaka sasa nimetafta ambae amesema hapendi wali maharage sijamuona!!! Wali maharage oyeeee... hii kitu usichezee.
 
Napenda vyakula vyote isipo kuwa makande tu , siwezi kupenda chakula kinachopendwa na wapare aseeπŸ€”
 
Katika mboga za majani yenye ufanisi katika afya ya binadamu ni hiyo sasa.

Kama ladha yake haipandi, inashauriwa ichanganywe kwenye nyama etc kukata shombo.
Kabeji haina kirutubisho chochote mwilini,,,kama kipo kitaje !
 
Katika mboga za majani yenye ufanisi katika afya ya binadamu ni hiyo sasa.

Kama ladha yake haipandi, inashauriwa ichanganywe kwenye nyama etc kukata shombo.
Kabichi ipo na vitamini gani tuambie
 
Niliingia cafeteria Moja hapo mtaa wa Lumbumba jirani kabisa na Ofisi ya CCM Mkoa, nikaagiza ugali kuku.... Sasa wakaleta ugali na nyama ya kuku imechanganywa na majani ya maboga na ikawa haijaungwa..... Pumbavu kabisa Ile menyu hovyo sana.... Niliichukia sana.... Nilikula Sababu ya njaa.....πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Chipsi aiseee!!!, kitu kinaitwa chipsi sidhani kama nitakuja kula hata kwa bahati mbaya!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…