Ni chakula gani watu wanakipenda lakini wewe hujawahi kukielewa kabisa?

Ni chakula gani watu wanakipenda lakini wewe hujawahi kukielewa kabisa?

Ndio hivyo ila mimi sijawah kuzipenda mkuu, zikitiwa kwenye dagaa huwa nakula dagaa tu.

Kuna watu wanakula mbichi kabisaa na chumvi tu.
Hata mimi zamani nilikuwa sizipendi ...nilianza kuzila kwa kuzisikilizia ndiyo nikagundua kuwa ni nzuri tu
 
Hizo mboga ulizo tsja unslia chakula gani ugali ? Uchungu wa mchunga unachujwa vizuri na kubaki kidogo ule uchungu ndiyo unanogesha hiyo mboga nikama pilipili au ndimu kwenye mboga
Hiyo ni biringanya nalia ugali, wali, n.k.
 
Mkuu kwenye ndizi nakubaliana na wewe ingawa natokea unyakyusani kwenye ndizi nyingi, ila kuna ndizi kwetu wanaita ndizi uganda zile ukipikia supu ya nyama ni zaidi ya utamu.

Kitu nilichogundua Afrika tumebarikiwa kuwa na vyakula vingi vitamu, mavyakula ya kimagharibi na asia(isipokuwa India na China)mengi chenga. Sijui Shawarma,Pizza,Burger,Biryani ni utapeli mtupu
Birian hata kuionja tu siwezi Huwa nikiona tu najua hapa hakuna chakula Bali Kuna mapambo
 
Hivi Kuna mtu anapenda kabichi si tunalia(ga) shida tu jamani..😔ila hii mboga iheshimiwe inatusaidia(ga) nyakati za shida hasa misibani😊
Wapo wanakula tena bila kutia samaki wala nyama kabichi tupu
 
Kuna baadhi ya watu lazima wanywe chai ya rangi mara 4 au 5 Kwa siku..
Asubuhi,mchana,jioni, usiku,

Na asipopata kikombe Cha chai kichwa kinauma au anakuwa hayupo sawa..

Inamaana wametoa sana madini ya chuma tumboni sio?
Ndy maana akikosa chai ya rangi kichwa kinauma?
Au chai huleta uraibu?
Hapo Kwa red ndio ukweli
 
Kwahyo wale ambao bila kunywa chai ya rangi kichwa lazima kiume, anakuwa amekosa madini gn?
Au amezidisha kuondoa madini ya chuma?

Chai ya rangi zaidi ya kuleta joto mwilini haina maana yeyote..
Inaleta Alostoo!!
Mimi ilikuwa nikiacha kutumia siku inakuwa ndefu kwa maumivu ya kichwa so nikaipiga chini kiubishi 2007 ile mpaka leo sitii pua kwenye majani ya chai.
iwe ya rangi au maziwa hapana, now napiga tangawizi na green tea (mchai chai) hata nisipokunywa mwezi nakuwa fresh tu.
 
Sinywi kitu kinaitwa chai,
Iwe ya maziwa au ya rangi.

Asubuhi always nakunywa soup au juice mwaka wa 30 huu...
Kama mini asee huwa napiga tangawizi tu, ikikosekana basi choochote ila sio TATEPA, CHAI JABA Hata Kahawa hapana
 
Kama mini asee huwa napiga tangawizi tu, ikikosekana basi choochote ila sio TATEPA, CHAI JABA Hata Kahawa hapana
Tangawizi,majani ya mchai chai kidogo yanashawishi ila pia sishughuliki nayo zaidi ya soup au juice.

Ila TATEPA hayana faida mwilini zaidi ya kutia joto
 
Inaleta Alostoo!!
Mimi ilikuwa nikiacha kutumia siku inakuwa ndefu kwa maumivu ya kichwa so nikaipiga chini kiubishi 2007 ile mpaka leo sitii pua kwenye majani ya chai.
iwe ya rangi au maziwa hapana, now napiga tangawizi na green tea (mchai chai) hata nisipokunywa mwezi nakuwa fresh tu.
Hyo mchai chai na tangawizi ndy mpango mzima,
Ila hizo TATEPA,,hamna kitu inaleta zaidi ya kuongeza majasho mwilini,,na arosto
 
Back
Top Bottom