Acha uongo.
HAKUNA aliposema anawasihi mataifa tajiri yatambue na kutumia fursa zilizopo Africa.
Ametumia risala hiyo kuomba misaada na kusema dunia sio fair, Afrika tuna njaa na utapiamloa, magonjwa, ni masikini wa kutupwa, hatuna mashine za kilimo, wala mbolea, wala utafiti, na tuna madeni, na ushindani wa dunia ni mkali sana.
Halafu akasema bado tunasubiri ahadi ya mafanikio itakayoletwa na globalization.
Hivi nchi tajiri zilituahidi kwamba globalization itatutoa ???
Na zilitusukuma tuingie kwenye globalization ?
Waingereza ndio waliwaambia Waafrika wakafuate mataka taka kama ma ndala na ma vikombe ya plastiki CHINA badala ya kujifunza kuvizalisha nyumbani kuokoa foreign currency ???
Watu wanakula, sisi tunapita na bakuli kutangaza umasikini. Angeenda na ndege ya kulipia tiketi daraja la tatu, sio luxury class na ndege yake mwenyewe, too expensive! Wangemuelewa na wangemheshimu zaidi.