Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hebu kwanza!

Tukiangalia upande wa pili wa shilingi (sarafu) ambayo haipo tena)!

Hivi mipango ya aina hii haiwezi kutumika kuwafunga zaidi wanaotafuta kujitenga huko visiwani?

Nina maana ya kwamba, mipango kama hii iwe ndiyo sababu ya kuufanya Muungano uwe karibu zaidi; hizi zikiwa hatua za kutupeleka kwenye "serikali moja" kwa mfano!

Sina maana ya kusema hapa kwamba hawa viongozi wanaofanya haya wanayafanya kwa nia hiyo; lakini haya yanaweza kuzalisha kitu ambacho hawakukitegemea kabisa, kukiwa na kiongozi mwenye ushawishi wa kustawisha muungano.

Ni wazo tu.
 
Philipo 'prospects' zake zilikuwa nzuri sana, lakini hii tabia aliyoanza kuionyesha akiwa mgonjwa wa UVIKO imejitokeza kuwa 'liability' kubwa sana kwake.
Mtu huwezi kuwa kama 'robot' lililo'programiwa' na kutumiwa na mwenye program zake bila kusita.
 
Kwa mtazamo wangu Kalamu ni kwamba suluhu ya Muungano wetu ni ama tuwe na serikali kuu moja ikiwa na majimbo (Federal Government) au serikali mbili ya Tanganyika na Zanzibar chini ya serikali moja ya Muungano (Union Government) au tuwe na serikali moja kamilifu (Unitary Government) na Zanzibar ikiwa ni mmojawapo wa mikoa ya serikali hiyo.

Ili tufike huko ni lazima tuwe na viongozi jasiri, viongozi ambao kwa sasa hatuna.
 
It's too much! Mtanganyika anamenyeka sana kwa kupeleka resource eneo lisiolo na tija kwasababu ukienda BoT utaona mchango wa Simiyu na si Zanzibar
Lakini kwenye mgao wao wako mbele kwa kasi ya mshale. Mgao wa nini kama watu wao wanahudumiwa kwa kila kitu na Watanganyika? Iko siku watataka na Rais wao ajengewe Ikulu Dodoma. Shika maneno yangu.
 
Tatizo letu huwa tunachagua watu tu, bila ya kuwa na adhari kwamba watu hao tunawapa mamlaka gani dhidi yetu. Inasikitisha kwamba wanasiasa wetu wa Tanganyika wako kimya kama vile hakuna kinachotokea.

wako Bize kusema "Mama anaupiga mwingi"
 
Huo mstari wa mwisho ndio kila kitu kwa hali iliyopo sasa.

Lakini naomba pia tulitilie maanani hili la sasa, kwamba, bila ya kujuwa wala kutegemea, inawezekana kabisa haya yanayofanyika sasa hivi (ya kuinufaisha zaidi Zazibar), matokeo yake yakawa ndiyo ndoana ya kutupeleka kwenye serikali moja kirahisi.
Sijui, lakini ni dhana ambayo siwezi kamwe kuidharau, pakiwepo na mazingira mazuri na uongozi wenye maono kutupeleka huko.

Wazanzibar wakijaa hapa, na kunufaika kiasi cha kuona uzanzibari wao hauna maslahi zaidi ya uTanzania wao kutokana na manufaa wanayoyapata, bila shaka watapenda kuwa waTanzania zaidi.
 
Kama mission ya SSH ni kuua muungano, lengo lake litatimia haraka sana, haya hayakubaliki

Tubebe gharama kwa mambo yasiyo na maana kama ha
Mkuu 'Nguruvi3', pamoja na maumivu yote haya, binafsi naanza kuwa na imani na nadharia hii mpya. Hata sijui itafika wapi, lakini ni wazo tu, kwamba anayofanya Samia ndiyo iwe kamba ya kuufumba Muungano wenyewe kiasi kwamba hauwezi kuvunjika tena.

Hapana. Wazo la kuvunja Muungano binafsi silioni na wala silitetei. Lililopo ni kuyashughulikia madhaifu yake na kuuimarisha Muungano zaidi.
 
Hapana. Wazo la kuvunja Muungano binafsi silioni na wala silitetei. Lililopo ni kuyashughulikia madhaifu yake na kuuimarisha Muungano zaidi.
Hakuna mwenye akili timamu anayewaza kuwa Muungano huu unastahili kuvunjwa. Kwanza ni jambo lisilowezekana lakini pia athari zake kama taifa hatuwezi kuzihimili.
 
Hakuna mwenye akili timamu anayewaza kuwa Muungano huu unastahili kuvunjwa. Kwanza ni jambo lisilowezekana lakini pia athari zake kama taifa hatuwezi kuzihimili.
Sina tatizo na muungano kuwepo

Hebu nifahamishe kuna athari gani kwa Taifa?
 
Sina tatizo na muungano kuwepo

Hebu nifahamishe kuna athari gani kwa Taifa?
Muungano ukivunjika ni lazima kuna athari hasi na chanya. Bahati mbaya sana zile hasi kama taifa hatuwezi kuzihimili. Na ndiyo maana kwenye mabandiko yangu ya awali nilisema sitamani yale mambo ya Pakistan na India kuhusu Kashimir yatokee hapa Tanzania.

Huu Muungano ukivunjika athari hasi zake hakuna wa kuweza kuzihimili, lazima tutasambaratika tu.
 
Hii si sawa kabisa kwa sababu hata mwanamke mtaalam aliyeolewa na Mzanzibari wakirudi Zanzibar hawezi kuruhusiwa kufanya kazi huko, badala yake mume ataendelea na kazi na mke atalazimika kurudi Tanganyika ili aendelee na ajira yake!
 
Ni athari gani?

Mwaka 1967 Nyerere alisema '' Wazanzibar wakiukataa muungano sitwapiga mabomu''

Nauliza athari gani?
 
Ni athari zipi?
Ninayoiona haraka haraka bila hata kufikiri ni hii ya "kuwaudhi, kuwakasirisha waTanganyika", kuona kwamba wenzao ndani ya Muungano wanafaidika zaidi ya wao.
Hizi hasira zinaweza kuwa kichocheo kikubwa kwa wananchi wa eneo moja kuukataa muungano moja kwa moja; hasa pakitokea kuwepo na kiongozi mwenye ushawishi wa kutaka iwe hivyo.
 
Ni athari gani?

Mwaka 1967 Nyerere alisema '' Wazanzibar wakiukataa muungano sitwapiga mabomu''

Nauliza athari gani?
1967 tulikuwa hatujaenda mbali sana kuliko tulivyo sasa. Wakati ule ungevunjika wala kusingekuwa na tatizo.
 
Sio muda naweka hathari hasi na chanya zitakazotokea pindi Muungano ukivunjika.
 
Zamani ilikuwa wazanzinari ndio waliokuwa wanalalamikia huu muungano sasa hivi imekuwa watanganyika ndio wanalalamika 😅😅 ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Farao Wazenji wametulia kimyaa !! Wanasemaga waswahili Kutesa kwa zamu. !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…