Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Kwa Mfano , mimi wa kutoka Kajunjumele Kyela ninaweza kukubaliwa kugombea Ubunge Chake chake , Mchambawima au kisiwandui kama Husein Mwinyi alivyogombea Mkuranga ?
Inategemea umeishi muda gani huko, kama umekidhi vigezo vya kupata kitambulisho cha ukaazi una haki ya kugombea
 
Hii ni mojawapo ya kero kubwa ya Muungano, ambapo kuna wazanzibari wameanza kujazwa kwenye nafasi na vyeo kwa Wizara na Taasisi zisizo za mungano. Capo Wakuu wa Wilaya, Ma RAS, DAS na DED. Mfano Mkuu wa Wilaya Mkuranga yule dada ni mzanzibari mtoto wa Rafiki yake Kiongozi wa Juu wa nchi. Haki za Wabara zinazulumiwa sana awamu hii.
 
Kila jambo linamuda wake zamu yao imefika na itapita vumilia tu mkuu hata jiwe alisemwa anapendelea Skuma Gang[emoji23][emoji2].
 
Huu muungano umekuwa mithili ya ndoa yenye migongano. Mke na mume washaamua kuachana lakini wazazi wana kazi ya kuwalazimisha waendelee kujaribu tu labda suluhishi itapatikana.

Huu Muungano ni bora uvunjwe tu, tubaki na Tanganyika yetu na wao wabaki na Zanzibar yao na wabebe wazanzibari wao wote pia.
 
Back
Top Bottom