Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 11,786
- 18,562
Ujue nipo Kajunjumele hapa...Kwa Mfano , mimi wa kutoka Kajunjumele Kyela ninaweza kukubaliwa kugombea Ubunge Chake chake , Mchambawima au kisiwandui kama Husein Mwinyi alivyogombea Mkuranga ?
Kama wote ni Watanzania kwanini Mtanganyika haruhusiwi kununua ardhi Zanzibar ?????Ni halali kwa sababu hatuna utabganyika wala tanganyika, tuna tanzania!
EeeenHeeeee!,Muundo wa muungano utazamwe upya ili kuondoa hii mikanganyiko iliyopo.
Kalamu Nguruvi3 zitto junior JokaKuu brazaj
Maswali magumu kwa wakati huu lakini siku atakapoondoka haya yote majibu yake utayaona jinsi yalivyo; kwa sasa dola inalinda hata kisicho halali kuwepo kwa sababu ya mhimili fulani kuteka mihili mingine, ukithubutu kupanua kinywa chako na kutoa sauti ya maneno kuhusu hili utakapoishia ni wewe pekee na wao ndio mnaojua. State capture at work................ Tanzania is a hybrid state with sovereignty status in the record at the international level as opposed to Zanzibar which is a ceremonial state with limited borders. The United Republic of Tanzania constitution and the Zanzibar Revolutionary constitution conflict with each other.....................URT constitution provides that Zanzibar is not a state whilst the converse asserts Zanzibar is a full state with its own government............................ This is an ironic mockery of the people of Tanzania whose constitution's inconsistency needs to be immediately amended to meet the people's will.Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?
Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?
Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?
Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?
Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?
Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?
Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
Zanzibar ni Zanzibar ila Tanganyika ni Tanzania bara. KWA NINI??
Ndoa hazijawa tatizo, watu wanaoa popote duniani na haiwezi kuwa hojaKuoa na kuolewa inakuaje
Masuala ya Ardhi kununua na kuuza, je watu wa bara tunaruhusiwa kwenda kurundikana na kununua mashamba na Ardhi uko Zenjibar na kujenga majumba, maviwanda na mahotel makubwa?
Masuala ya Biashara kodi na makato, ukinunua kitu Zanzibar Kodi inakuaje na makato yanaenda wapi na ukinunua kitu bara Kodi inaenda wapi na makato yanakuaje
Masuala ya usafiri kuingia na kutoka je kuna live permit au unaingia km unaingia uwani na kutoka
Emu gusia na hapo inakuaje mkuu
Kwa sababu baba wa taifa alisema moja na moja ni mbili, na akawakejeli waumini wa moja na moja ni tatu.Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ipo ni kwa nini Tanganyika isiwepo.
Kwa nini kuwepo kwa Tanzania kuipoteze Tanganyika lakini Zanzibar iendelee kuwepo?
Wenyewe (WaZanzibari) watakwambia mambo yao yote yanaamuliwa na CCM. Kwamba viongozi wao wote ni CCM.Leo hii tuna rais Mzanzibari anawaamulia Watanganyika mambo mengine ambayo wala siyo ya Muungano. Sasa hii inakuwaje?
Hakuna Mtanganyika mwenye power ya kuwaamulia Wazanzibari mambo yao ya ndani yasiyo ya muungano!
Kmkm ni jeshi la ovyo zaidi hata ya jeshi letu la mgambo wanaoshinda daily wakikimbizana na mama ntilie wa tandale.Hivi wale askari wa kmkm mafunzo yao wanapata bara au Zanzibar, vipi mtanganyika anaweza kujiunga na hilo jeshi..?
Dodoma ni eneo tu, lakini Wazanzibari wenyewe wanashiriki kikamilifu ndani ya CCM. Kwani hujui kuwa CCM ni TANU na ASP?.Wenyewe (WaZanzibari) watakwambia mambo yao yote yanaamuliwa na CCM. Kwamba viongozi wao wote ni CCM.
CCM ambayo imekuwa ikiendeshwa toka Dodoma, ndiyo inayoamua mambo ya Zanzibar (isipokuwa kwa awamu hii ya Samia).
Pengine huu ndio utakuwa mwanzo wa kulegeza makucha ya CCM kutoka Dodoma yakiwafinya waZanzibari.
Nafasi yao muhimu ipo hapa kujikwamua, wakishindwa safari hii ndiyo basi tena!
Dont worry. You just deal with the Articles of Union and the Act of the Union. These are the foundations of the Union.Maswali magumu kwa wakati huu lakini siku atakapoondoka haya yote majibu yake utayaona jinsi yalivyo; kwa sasa dola inalinda hata kisicho halali kuwepo kwa sababu ya mhimili fulani kuteka mihili mingine, ukithubutu kupanua kinywa chako na kutoa sauti ya maneno kuhusu hili utakapoishia ni wewe pekee na wao ndio mnaojua. State capture at work................ Tanzania is a hybrid state with sovereignty status in the record at the international level as opposed to Zanzibar which is a ceremonial state with limited borders. The United Republic of Tanzania constitution and the Zanzibar Revolutionary constitution conflict with each other.....................URT constitution provides that Zanzibar is not a state whilst the converse asserts Zanzibar is a full state with its own government............................ This is an ironic mockery of the people of Tanzania whose constitution's inconsistency needs to be immediately amended to meet the people's will.
UshapanikTumia elimu yako vizuri mbona huwa nakuona Kama mtu wa maana!ata Kama ni vyeo havitafutwi Kwa namna hiyo na nyeupe itabaki kuwa nyeupe tu na kinyume chake ni sahihi
Hakuna anayebaguliwa pia soma kinachozungumziwa uelewe kabla ya kujibu.Watanzania bara wengi sana ndugu na jamaa zangu nawafahamu wamekimbilia Zanzibar kufanya kazi mbalimbali hasa sekta ya utalii. Hoja hizi za uzanzibar na utanganyika ni za kibaguzi. Mwalimu Nyerere alikuwa sawa kusema tunauona uzanzibar wao na utanganyika wetu Kwa kuwa tuko ndani ya Muungano. Muungano ukivunjika hakutakuwepo na utanganyika tena Bali tutahamia kwenye usukuma na uchaga
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwa Mfano , mimi wa kutoka Kajunjumele Kyela ninaweza kukubaliwa kugombea Ubunge Chake chake , Mchambawima au kisiwandui kama Husein Mwinyi alivyogombea Mkuranga ?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Chao chao, chetu chao!
Nyerere huyo kwa ujuaji mwingi aliwauza Watanganyika kwa sababu ya personal ambitions za kutaka kutawala eneo kubwa, na kujionyesha kimataifa kuwa yeye ni "Uniter"
Unachukua 25% ya ajira unawapa watu wasiofika milioni mbili, halafu hata zile 75% zilizobaki bado wana haki ya kuziomba vilevile kwa hoja kuwa ni za watanzania wote bila kubagua mtu katoka wapi.
Haka ka muungano kanaifanya Tanganyika kuwa Kubwa Jinga na Zanzibar kuwa dogo Janja
Mkuu Allen Kilewella , kwanza kazi ni kazi, hakuna kazi ya mtu, hivyo hakuna kazi za Mtanzania wala kazi ya Mzamzobari, kazi ni ya wote. Pili hiki ulichokileta ni ubaguzi wa kutaka kuwabagua Wazanzibari!. Mwalimu Nyerere alisema hii ni dhambi!. Kiukweli somo la uraia linahitajika sana Tanzania kwa watu kama wewe!. Tanzania ni nchi moja, ya JMT, yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki sawa na haki zote za raia wa Tanzania.
Ndani ya uraia wa Tanzania kuna uraia mmoja tuu wa Mtanzania.
Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna sehemu moja ya Zanzibar ina utawala wake wa ndani ambao Wazanzibari licha ya kwanza kuwa ni raia wa JMT wenye haki zote za uraia wa JMT, hawa wamepewa haki za ziada za ukaazi wa Zanzibar. Kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar sio kitambulisho cha uraia, hakuna uraia wa Zanzibar kuna uraia mmoja tuu wa JMT na ziada ya ukaazi wa Zanzibar.
Hivyo Wanzanzibari wana haki zote za uraia wa Tanzania na ziada ya haki za ikaazi wa Zanzibar.
Lile jambo langu likitimia, nafungua darasa la bure la Haki, kuwaelimisha Watanzania haki zao mbalimbali zikiwemo haki za uraia.
P