Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Mm naishi Zanzibar kiukwel ni ngumu sana kuajiriwa SMZ sharti lazima uwe na kitambulisho cha mzanzibar mkaazi, Sasa kukipata hicho kitambulisho ni mtihani sana utazungushwa mpaka ukate tamaa, ajabu kuna ajira mfano ualimu, afya wazanzibar wako free kuomba na wanaajiriwa vizur tu ili mradi awe na leseni ya bara.

Hili ni tatizo kubwa watanganyika tunanyonywa sana ktk huu muungano .
 
Muundo wa muungano utazamwe upya ili kuondoa hii mikanganyiko iliyopo.
Kalamu Nguruvi3 zitto junior JokaKuu brazaj
EeeenHeeeee!,

Mkuu 'Proved', sijui unataka niseme nini hapa!

Muungano uliowekwa na waasisi haukuwa na lengo la haya yanayofanyika leo.

Ukiangalia kwa makini utaona kwamba yanayofanyika leo yana lengo moja tu; nalo ni kuuvunja Muungano wenyewe. Haya yanafanywa na hao hao viongozi wenyewe waliopo kwenye madaraka.
Lengo lao ni kuwakera waTanganyika, na wakikereka vya kutosha, wanavunja Muungano. Hili ndilo wanalolitafuta hawa viongozi wetu sasa hivi.
 
Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?

Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?

Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?

Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?

Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?

Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?

Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
Maswali magumu kwa wakati huu lakini siku atakapoondoka haya yote majibu yake utayaona jinsi yalivyo; kwa sasa dola inalinda hata kisicho halali kuwepo kwa sababu ya mhimili fulani kuteka mihili mingine, ukithubutu kupanua kinywa chako na kutoa sauti ya maneno kuhusu hili utakapoishia ni wewe pekee na wao ndio mnaojua. State capture at work................ Tanzania is a hybrid state with sovereignty status in the record at the international level as opposed to Zanzibar which is a ceremonial state with limited borders. The United Republic of Tanzania constitution and the Zanzibar Revolutionary constitution conflict with each other.....................URT constitution provides that Zanzibar is not a state whilst the converse asserts Zanzibar is a full state with its own government............................ This is an ironic mockery of the people of Tanzania whose constitution's inconsistency needs to be immediately amended to meet the people's will.
 
Kuoa na kuolewa inakuaje

Masuala ya Ardhi kununua na kuuza, je watu wa bara tunaruhusiwa kwenda kurundikana na kununua mashamba na Ardhi uko Zenjibar na kujenga majumba, maviwanda na mahotel makubwa?

Masuala ya Biashara kodi na makato, ukinunua kitu Zanzibar Kodi inakuaje na makato yanaenda wapi na ukinunua kitu bara Kodi inaenda wapi na makato yanakuaje

Masuala ya usafiri kuingia na kutoka je kuna live permit au unaingia km unaingia uwani na kutoka

Emu gusia na hapo inakuaje mkuu
Ndoa hazijawa tatizo, watu wanaoa popote duniani na haiwezi kuwa hoja

Ardhi: Wazanzibar huru kujimegea mapande bara. Rais Mwinyi kasema Mtanganyika kupata ardhi Zanzibar atafikiriwa kama mgeni mwingine, yaani kama Mfilipino, Mnigeria au Mbrazili.

Biashara na kodi: Biashara ilileta tatizo, Magufuli alikataa uchochoro wa kupitishia bidhaa Zanzibar kwasababu kule hawachukui kodi. Mfano, kontena moja inayolipiwa milioni 1 Zanzibar bara ni milioni 10. Wafanyabiashara wa Zanzibar wakachukua uchochoro huo. JPM akaona ni ujinga kutoza watu wake kodi kwa uzembe wa Zanzibar akaweka kodi kwa bishaa.

Kodi: Hakuna VAT inayovuka bahari kuja bara wala kodi yoyote ya Zanzibar inayoingia hazina
 
Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ipo ni kwa nini Tanganyika isiwepo.

Kwa nini kuwepo kwa Tanzania kuipoteze Tanganyika lakini Zanzibar iendelee kuwepo?
Kwa sababu baba wa taifa alisema moja na moja ni mbili, na akawakejeli waumini wa moja na moja ni tatu.
 
Leo hii tuna rais Mzanzibari anawaamulia Watanganyika mambo mengine ambayo wala siyo ya Muungano. Sasa hii inakuwaje?
Hakuna Mtanganyika mwenye power ya kuwaamulia Wazanzibari mambo yao ya ndani yasiyo ya muungano!
Wenyewe (WaZanzibari) watakwambia mambo yao yote yanaamuliwa na CCM. Kwamba viongozi wao wote ni CCM.

CCM ambayo imekuwa ikiendeshwa toka Dodoma, ndiyo inayoamua mambo ya Zanzibar (isipokuwa kwa awamu hii ya Samia).

Pengine huu ndio utakuwa mwanzo wa kulegeza makucha ya CCM kutoka Dodoma yakiwafinya waZanzibari.

Nafasi yao muhimu ipo hapa kujikwamua, wakishindwa safari hii ndiyo basi tena!
 
Hivi wale askari wa kmkm mafunzo yao wanapata bara au Zanzibar, vipi mtanganyika anaweza kujiunga na hilo jeshi..?
Kmkm ni jeshi la ovyo zaidi hata ya jeshi letu la mgambo wanaoshinda daily wakikimbizana na mama ntilie wa tandale.
Kutamani kuwa askari wa kmkm ni kujidhalilisha, zanzibar waoneeni huruma ndio maana wanakuja bara hata kuwa walimu lkn wabara hatuvutiwi kuufuata ualimu wa Uko zanzibar
 
Wenyewe (WaZanzibari) watakwambia mambo yao yote yanaamuliwa na CCM. Kwamba viongozi wao wote ni CCM.

CCM ambayo imekuwa ikiendeshwa toka Dodoma, ndiyo inayoamua mambo ya Zanzibar (isipokuwa kwa awamu hii ya Samia).

Pengine huu ndio utakuwa mwanzo wa kulegeza makucha ya CCM kutoka Dodoma yakiwafinya waZanzibari.

Nafasi yao muhimu ipo hapa kujikwamua, wakishindwa safari hii ndiyo basi tena!
Dodoma ni eneo tu, lakini Wazanzibari wenyewe wanashiriki kikamilifu ndani ya CCM. Kwani hujui kuwa CCM ni TANU na ASP?.
 
Maswali magumu kwa wakati huu lakini siku atakapoondoka haya yote majibu yake utayaona jinsi yalivyo; kwa sasa dola inalinda hata kisicho halali kuwepo kwa sababu ya mhimili fulani kuteka mihili mingine, ukithubutu kupanua kinywa chako na kutoa sauti ya maneno kuhusu hili utakapoishia ni wewe pekee na wao ndio mnaojua. State capture at work................ Tanzania is a hybrid state with sovereignty status in the record at the international level as opposed to Zanzibar which is a ceremonial state with limited borders. The United Republic of Tanzania constitution and the Zanzibar Revolutionary constitution conflict with each other.....................URT constitution provides that Zanzibar is not a state whilst the converse asserts Zanzibar is a full state with its own government............................ This is an ironic mockery of the people of Tanzania whose constitution's inconsistency needs to be immediately amended to meet the people's will.
Dont worry. You just deal with the Articles of Union and the Act of the Union. These are the foundations of the Union.
 
Watanzania bara wengi sana ndugu na jamaa zangu nawafahamu wamekimbilia Zanzibar kufanya kazi mbalimbali hasa sekta ya utalii. Hoja hizi za uzanzibar na utanganyika ni za kibaguzi. Mwalimu Nyerere alikuwa sawa kusema tunauona uzanzibar wao na utanganyika wetu Kwa kuwa tuko ndani ya Muungano. Muungano ukivunjika hakutakuwepo na utanganyika tena Bali tutahamia kwenye usukuma na uchaga
 
Hakuna anayebaguliwa pia soma kinachozungumziwa uelewe kabla ya kujibu.
 
Chao chao, chetu chao!

Nyerere huyo kwa ujuaji mwingi aliwauza Watanganyika kwa sababu ya personal ambitions za kutaka kutawala eneo kubwa, na kujionyesha kimataifa kuwa yeye ni "Uniter"

Unachukua 25% ya ajira unawapa watu wasiofika milioni mbili, halafu hata zile 75% zilizobaki bado wana haki ya kuziomba vilevile kwa hoja kuwa ni za watanzania wote bila kubagua mtu katoka wapi.

Haka ka muungano kanaifanya Tanganyika kuwa Kubwa Jinga na Zanzibar kuwa dogo Janja
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Huu muungano una magumash mengi sana
Mkuu Allen Kilewella , kwanza kazi ni kazi, hakuna kazi ya mtu, hivyo hakuna kazi za Mtanzania wala kazi ya Mzamzobari, kazi ni ya wote. Pili hiki ulichokileta ni ubaguzi wa kutaka kuwabagua Wazanzibari!. Mwalimu Nyerere alisema hii ni dhambi!. Kiukweli somo la uraia linahitajika sana Tanzania kwa watu kama wewe!. Tanzania ni nchi moja, ya JMT, yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki sawa na haki zote za raia wa Tanzania.

Ndani ya uraia wa Tanzania kuna uraia mmoja tuu wa Mtanzania.

Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna sehemu moja ya Zanzibar ina utawala wake wa ndani ambao Wazanzibari licha ya kwanza kuwa ni raia wa JMT wenye haki zote za uraia wa JMT, hawa wamepewa haki za ziada za ukaazi wa Zanzibar. Kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar sio kitambulisho cha uraia, hakuna uraia wa Zanzibar kuna uraia mmoja tuu wa JMT na ziada ya ukaazi wa Zanzibar.

Hivyo Wanzanzibari wana haki zote za uraia wa Tanzania na ziada ya haki za ikaazi wa Zanzibar.

Lile jambo langu likitimia, nafungua darasa la bure la Haki, kuwaelimisha Watanzania haki zao mbalimbali zikiwemo haki za uraia.
P
 
Back
Top Bottom