Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hii ni mojawapo ya kero kubwa ya Muungano, ambapo kuna wazanzibari wameanza kujazwa kwenye nafasi na vyeo kwa Wizara na Taasisi zisizo za mungano. Capo Wakuu wa Wilaya, Ma RAS, DAS na DED. Mfano Mkuu wa Wilaya Mkuranga yule dada ni mzanzibari mtoto wa Rafiki yake Kiongozi wa Juu wa nchi. Haki za Wabara zinazulumiwa sana awamu hii.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii unaelewaje? Mtu kutoka Zanzibar sio mmoja wa mwananchi ya Jamhuri ya Muungano.
 
Ni halali kwa sababu hatuna utabganyika wala tanganyika, tuna tanzania!
Sasa ni muungano gani huo ambao moja ya mwana muunganl hajabadili jina lake na badoba ajiendesha kama nchi halafu huyu mwingine kaachana na jina lake anatumia jina la muungano?
 
Mbarawa alikuwa waziri enzi ya JPM akacha akaenda zanzibar, akachukua fomu kugombea Urais huko, akapigwa chini na mwinyi, akageuka akarudishwa bara akapewa uwaziri sasa anauza bandari.

So ukiwa Mzanzibari unacheza na akili za watanganyika utakavyo.

Ni Nani anayeweza kucheza huo Mchezo wa Mbarawa kama Wewe Sio Mzanzibari?

Tunachezewa sana hutadhani bara kuna watu 200,000!!
 
koti hili limetubana wa Tanganyika , NI muda Sasa eitha kulivua , au tuliwekee viraka Tena!!
 
Kuna picha Za mama mmoja zimebandika Tanzania bara yote kila mkoa kila wilaya zina maanisha nini?

Mbona ule upande mwingine hazijawekwa ?
 
Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?

Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?

Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?

Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?

Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?

Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?

Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
Afya siyo ya Muungano. Lakini kuna watumishi wengi tu wazanzibar wapo huku Bara na wanafanya kazi. Lakini sisi watanganyika haturuhusiwi kukaa na kufanya kazi Zanzibar. Hii siyo sawa kabisa

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
 
KATIBA IHESHIMIWE
 
Watanganyika wamekuwa kama watoto waliomkana Baba yao sasa laana inaanza kuwatafuna.
Mrejeeni Baba yenu mjoinusuru na hii ghadhabu ya laana.
 
Hii ndio hoja ya msingi ya serikali tatu, rais wa muungano na wa Zanzibar wote ni wazanzibari, nani anatetea maslahi ya Bara ndani ya Muungano? Bara inaporwa tu hakuna wa kuitetea, waliopigania Uhuru wa Tanganyika wanadhihakiwa mno
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?

Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?

Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?

Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?

Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?

Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?

Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
The Age of Enlightenment or the Enlightenment, also known as the Age of Reason

Hapa kwetu Tz 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 🇹🇿 pengine imechelewa sana.....

Ila ulaya miaka Mingi iliyo pita walipitia Enlightenment age................
 
Tatizo linakuja pale penye kikao chochote cha maamuzi Kuhusu muungano wa.zenj lazima waiwakilishe Zenj na Tz!=wawakilishi.2
M-Tg ikiwa bahati atakuwa na uwakilishi wa mjumbe mmoja
 
Hao jamaa ni waumini wakubwa wa ile kitu inayoitwa changu changu, chako changu. Na kama huamini, basi jaribu kufuatilia kwa kina! Halafu utaniambia.
CHAKO CHETU SOTE , Hi Tanganyika yetu sote. Ndo maana Serka li ya Tanga Nyika ni yetu soto kwa jina La Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
CHANGU CHANGU PEKE YANGU-Hi Zanzibar yetu peke yetu Wazanzibari, ndo maana Tuna serikali yetu peke yetu
 
Kwa Mfano , mimi wa kutoka Kajunjumele Kyela ninaweza kukubaliwa kugombea Ubunge Chake chake , Mchambawima au kisiwandui kama Husein Mwinyi alivyogombea Mkuranga ?
Aliyekuwa, Wakili wa Mahakama Kuu Msomi, Tundu A. Lissu.Akifafanua kitu.
‘’Nimefadhaishwa kidogo na baadhi ya michango ya humu ndani kuhusu masuala mbali mbali yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’’

Inaelekea tuna tatizo kubwa sana la uelewa wa historia yetu ya kisiasa na kikatiba. Kinachofundishwa kwa watoto wetu mashuleni kama 'historia' au 'civics' ni propaganda za kisiasa, if not outright fabrications.

Matokeo yake ni kwamba wengi wetu hatujielewi hata hapa tulipo, na tumefikaje hapa tulipo.

Kwa sababu hiyo, nawaombeni radhi kwa kuwachosha na hiki nitakachoandika kuhusu 'Nchi yetu.'

Muungano wetu umeundwa kwa mfano wa Muungano wa Falme ya Britannia Kuu (ile inayoitwa kimakosa 'Uingereza'), kwa kifupi UK.

Sheria ya Mapatano ya Muungano Kati ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ya tarehe 22 Aprili, '64, ilikopiwa moja kwa moja kutoka kwenye Sheria ya Mapatano ya Muungano Kati ya Uingereza na Scotland ya 1703.

Hii ni kwa sababu mtunzi wa Sheria hiyo alikuwa Mwingereza Roland Brown, aliyekuwa Solicitor General wa Tanganyika mara baada ya Uhuru, na wakati wa Muungano. Brown alitumia mfano wa nchi yake mwenyewe katika kutengeneza Muungano wetu.

Muungano wa aina hii hauui nchi washirika wake. Ni Muungano katika baadhi ya mambo tu. UK inaundwa na nchi nne (Uingereza, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini) ambazo zimeendelea kuwepo zikiwa na mamlaka kamili katika mambo fulani fulani.

Ndivyo ilivyo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zanzibar ina mamlaka kamili katika mambo yote yasiyokuwa ya Muungano ya Zanzibar.

Kwa upande mwingine, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina mamlaka kamili katika mambo yote ya Muungano; na pia kwa mambo yote yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika.

Hapa ndipo lilipo tatizo la msingi la Muungano wetu, na chanzo kikuu cha ugomvi wetu na Wazanzibari. Na ndipo palipojaa propaganda za kisiasa.

Wanaosema Tanganyika 'ilipotea' kwa sababu ya Muungano hawako sahihi. Tanzania ndio Tanganyika. Kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiuhalisia ni Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika iliyonyakua madaraka ya Zanzibar katika yale yanayoitwa 'Mambo ya Muungano.'

Siku Muungano huu unazaliwa, yaani tarehe 26 Aprili, '64, Mwalimu Nyerere alitunga sheria mbili kwa amri ya Rais (decree).
Sheria moja iliekeza kwamba watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika, kuanzia siku hiyo watahesabika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Aidha, Mahakama Kuu ya Tanganyika itakuwa ndio Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Vile vile, kila mahali katika kila jambo na katika kila sheria za nchi panapotamkwa neno 'Tanganyika', patatamkwa maneno 'Jamhuri ya Muungano.'

Sheria ya pili ilielekeza kwamba Nembo za Taifa la Tanganyika, yaani 'Bibi na Bwana' na Bendera ya Taifa la Tanganyika, zitakuwa ndio Nembo za Taifa za Jamhuri ya Muungano.

Baadae kidogo Mwalimu Nyerere alitunga sheria nyingine iliyoigeuza Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa ndio Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano.

Kwa hiyo, tangu siku ya kwanza kabisa ya Muungano, Tanganyika ilivaa koti la Tanzania. Haijawahi kulivua tangu wakati huo.

Tatizo hili la Muungano lilitokana na uelewa tofauti wa aina ya Muungano wenyewe,kati ya waasisi wake, yaani Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume.

Kwa Mwalimu, Muungano huu ulikuwa njia ya muda tu ya kuelekea Serikali moja, i.e. Serikali ya Tanganyika iliyojifunika koti la 'Tanzania.'

Kwa Sheikh Karume, Muungano huu ulikuwa ni njia ya muda tu ya kuelekea Serikali tatu, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwalimu Nyerere na 'sisi' Watanganyika tumekuwa na agenda ya kuimeza Zanzibar tangu mwanzoni kabisa.

Kuna ushahidi mkubwa wa nyaraka unaoonyesha kwamba Mwalimu Nyerere alimlazimisha Sheikh Karume kuwa na Muungano. Kumbuka Jeshi la Tanganyika lilipelekwa Zanzibar siku tatu tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mara baada ya Muungano, Mwalimu Nyerere na watu wake walianza kazi ya kuimeza Zanzibar, kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Mifano ifuatayo inathibitisha kauli yangu.

Kwanza, muundo wa Serikali mbili, uliokuwa ni temporary arrangement tu kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano, ukafanywa ndio muundo wa kudumu chini ya Katiba ya Mpito ya mwaka '65, na baadae Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka '77 iliyopo sasa.

Pili, kuanzia mwaka '64 hadi '77, Katiba yetu iliendelea kutumia jina la 'Tanganyika' katika vifungu vyake kadhaa.

'Tanzania Bara' ilizaliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka '77. Katiba hii iliua pia jina la 'Zanzibar' na badala yake ikazaliwa 'Tanzania Visiwani.'

Tatu, mabadiliko ya orodha ya Mambo ya Muungano. Hati ya Mapatano ya Muungano ya mwaka '64 ilikuwa na mambo 9 tu ya Muungano. Sasa orodha ya Mambo ya Muungano kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano ina mambo 22.

Mwaka '83, NEC ya CCM ilisema kwamba lengo la kuwa na orodha ya Mambo ya Muungano lilikuwa na kufafanua masuala yaliyoko chini ya mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yatahamishiwa kwenye mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, i.e. Serikali ya Tanganyika.

Nne, kufuatia mgogoro mkubwa wa Muungano wa mwaka '83/'84, uliopelekea 'kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa'; na kungolewa madarakani kwa Rais wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe, mambo mawili yalitokea kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Moja, 'Tanzania Visiwani' iliuawa, na 'Tanzania Zanzibar' ikazaliwa. Hivyo, maneno 'Tanzania Zanzibar' yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ni ya mwaka '84.

Mbili, maneno ya ibara ya 1 ya Katiba ya sasa kwamba 'Tanzania ni nchi moja...' yaliingizwa. Maneno haya hayakuwepo tangu mwanzo wa Muungano huu, yaliingizwa mwaka '84, miaka 20 baada ya Muungano kuzaliwa.

Wazanzibari hawajawahi kukubali kupoteza nchi yao. Mifano ya kuthibitisha kauli hii ni mingi sana. Nitataja baadhi tu.

Moja, Zanzibar haikuwahi kutunga sheria ya kuridhia Mapatano ya Muungano, kama ilivyokuwa inatakiwa na Hati ya Mapatano ya Muungano.

Mbili, mgogoro juu ya kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania mwaka '66/67. Karume na Wazanzibari walitaka kuwa na Benki Kuu yao wenyewe, ili wawe na uhuru katika masuala ya fedha na uchumi. Badala ya Benki Kuu, waliishia kupata Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), benki ya kibiashara.

Tatu, kwa sababu ya kuongezwa kinyemela kwa mambo ya Muungano, kuna ushahidi kwamba Sheikh Karume alikuwa na mpango wa kuvunja Muungano muda mfupi kabla ya kuuawa kwake Aprili 7, '72.

Nne, kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa mwaka '84, na kung'olewa madarakani kwa Aboud Jumbe.

Kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wake, Bashir Ebassuah Kwaw Swanzy, Jumbe alipanga kuitisha Mahakama Maalum ya Jamhuri ya Muungano ili kupata ufumbuzi wa 'Kero za Muungano.'

Mwalimu Nyerere, kwa kutumia majasusi wake alimuwahi, na baadae akamlazimisha kujiuzulu. Aidha, Mwanasheria Mkuu Kwaw Swanzy, raia wa Ghana, alifukuzwa nchini; na Waziri Kiongozi Ramadhani Haji Faki alifukuzwa kazi.

Vile vile, Wazanzibari wengi, akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ya wakati wa Muungano, Wolfgang Dourado, waliwekwa kizuizini.

Tano, Katiba ya sasa ya Zanzibar ni 'Katiba ya Uhuru ya Zanzibar.' Maneno 'Zanzibar ni Nchi'; kutakuwa na 'Mzanzibari'; Rais wa Zanzibar ni 'Mkuu wa Nchi ya Zanzibar'; Rais wa Zanzibar ni 'Kamanda Mkuu wa vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar', n.k., ambayo yametapakaa katika Katiba hiyo ni uthibitisho kwamba Wazanzibari wanataka uhuru wao.

Sita, mjadala wa Katiba Mpya wa mwaka '11-'15 na mapendekezo ya Tume ya Warioba ni uthibitisho mwingine tosha kwamba Wazanzibari wanataka uhuru wao.

Sisi Watanganyika, kwa sababu ndio 'wafaidikaji' wakubwa wa Muungano huu, mara nyingi tumeshindwa kuelewa kilio hiki cha Wazanzibari na kukiunga mkono.

Kama ilivyo kawaida ya watu wanaotawala watu wa mataifa mengine, kumekuwa na fikra potofu kwamba, actually, tunawasaidia Wazanzibari, badala ya kuwakandamiza kisiasa na kuwanyonya kiuchumi.

Tunajiona 'tumepoteza' Tanganyika yetu, wakati ukweli ni kwamba tumeinyakua Zanzibar na tunaikalia kinyume na matakwa ya Wazanzibari walio wengi.

Kama sehemu ya mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiuchumi yanayohitajika Tanzania, suala la Muungano na Utaifa wa Zanzibar ni la umuhimu wa kipekee.

Ili kulitatua kwa njia ya maridhiano, sisi Watanganyika tunao wajibu mkubwa. Wajibu wetu wa kwanza ni kuifahamu historia yetu halisi, ili kuuelewa Muungano huu na kero zake na kuzitafutia dawa muafaka.

Tundu AM Lissu, MB.
Tienen, Belgium.
27 Aprili, 2019.
 
Juzi shirika la POSTA limetangaza kutenga Asilimia 25 ya AJIRA zake Kwa wazanzibar labda ndio wakati watu wenyewe hawazidi Asilimia moja ya watanzania wote
Kwani issue ya ajira si ni km free market, mwenye vigezo ndiyo anapata? Au mimi ndiyo sielewi mambo?!
 
Sasa ni muungano gani huo ambao moja ya mwana muunganl hajabadili jina lake na badoba ajiendesha kama nchi halafu huyu mwingine kaachana na jina lake anatumia jina la muungano?
Wanaosema Tanganyika 'ilipotea' kwa sababu ya Muungano hawako sahihi. Tanzania ndio Tanganyika. Kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiuhalisia ni Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika iliyonyakua madaraka ya Zanzibar katika yale yanayoitwa 'Mambo ya Muungano.'

Siku Muungano huu unazaliwa, yaani tarehe 26 Aprili, '64, Mwalimu Nyerere alitunga sheria mbili kwa amri ya Rais (decree).
Sheria moja iliekeza kwamba watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika, kuanzia siku hiyo watahesabika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Aidha, Mahakama Kuu ya Tanganyika itakuwa ndio Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Vile vile, kila mahali katika kila jambo na katika kila sheria za nchi panapotamkwa neno 'Tanganyika', patatamkwa maneno 'Jamhuri ya Muungano.'

Sheria ya pili ilielekeza kwamba Nembo za Taifa la Tanganyika, yaani 'Bibi na Bwana' na Bendera ya Taifa la Tanganyika, zitakuwa ndio Nembo za Taifa za Jamhuri ya Muungano.

Baadae kidogo Mwalimu Nyerere alitunga sheria nyingine iliyoigeuza Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa ndio Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano.

Kwa hiyo, tangu siku ya kwanza kabisa ya Muungano, Tanganyika ilivaa koti la Tanzania. Haijawahi kulivua tangu wakati huo.

Tatizo hili la Muungano lilitokana na uelewa tofauti wa aina ya Muungano wenyewe,kati ya waasisi wake, yaani Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume.
Kwa Mwalimu, Muungano huu ulikuwa njia ya muda tu ya kuelekea Serikali moja, i.e. Serikali ya Tanganyika iliyojifunika koti la 'Tanzania.'

Kwa Sheikh Karume, Muungano huu ulikuwa ni njia ya muda tu ya kuelekea Serikali tatu, yaani Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mwalimu Nyerere na 'sisi' Watanganyika tumekuwa na agenda ya kuimeza Zanzibar tangu mwanzoni kabisa Wanaosema Tanganyika 'ilipotea' kwa sababu ya Muungano hawako sahihi. Tanzania ndio Tanganyika. Kinachoitwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiuhalisia ni Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika iliyonyakua madaraka ya Zanzibar katika yale yanayoitwa 'Mambo ya Muungano.'

Siku Muungano huu unazaliwa, yaani tarehe 26 Aprili, '64, Mwalimu Nyerere alitunga sheria mbili kwa amri ya Rais (decree).
Sheria moja iliekeza kwamba watumishi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika, kuanzia siku hiyo watahesabika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Aidha, Mahakama Kuu ya Tanganyika itakuwa ndio Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano. Vile vile, kila mahali katika kila jambo na katika kila sheria za nchi panapotamkwa neno 'Tanganyika', patatamkwa maneno 'Jamhuri ya Muungano.'

Sheria ya pili ilielekeza kwamba Nembo za Taifa la Tanganyika, yaani 'Bibi na Bwana' na Bendera ya Taifa la Tanganyika, zitakuwa ndio Nembo za Taifa za Jamhuri ya Muungano.

Baadae kidogo Mwalimu Nyerere alitunga sheria nyingine iliyoigeuza Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa ndio Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano.

Kwa hiyo, tangu siku ya kwanza kabisa ya Muungano, Tanganyika ilivaa koti la Tanzania. Haijawahi kulivua tangu wakati huo.
 
Hapa tatizo ni muundo wa muungano, kwa aina hii iliyopo sasa ya serikali mbili ni vigumu sana kuweka mipaka baina ya Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wao wana serikali yao ndiyo maana identity yao bado inaonekana. Hivi fursa wanazipata kupitia kichaka cha kuwa Tanzania ni nchi moja. Sisi watanganyika pia tunajiona ndiyo Tanzania kwakuwa Tanganyika haipo. Tungekuwa na serikali 3 hili lingeweza kusimamiwa kwa umakini zaidi. Kama mchakato wa katiba mpya utafanikiwa suluhisho liwe ni kuwa na serikali 3, 1 au kila mtu apambana na hali yake irudi Tanganyika.
 
Back
Top Bottom