Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 31,913
- 65,514
Mbona una onyesha Kama umechoka au kukata tamaa. If you don't mind telling me. princess arianammh sawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona una onyesha Kama umechoka au kukata tamaa. If you don't mind telling me. princess arianammh sawa
Pole sana bro.......kuoa mwanamke anauekuzidi kipato... Brother....USIJARIBU.....
Wanadharau...masimango..Wabinafsi...
Najuta najuta..Najutia....most of them ni real... DEVIL [emoji49]..........
Kuitumikia dini badala ya kumtumikia MunguHabari zenu wananchi wa Taifa la JamiiForums, leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and downs nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo.
BINAFSI: Wakati nipo chuo mwaka wa tatu UDSM huko Tanzania nikipiga zangu Computer Science nilipata mchongo Nokia Siemens kuna mradi wa kusimika minara walikuwa wakifanya na walihitaji watu competent kwenye eneo la Network Systems nikapewa hiyo connection na nilipiga kazi kama mwaka hivi hela ilikuwa tamu ila bahati mbaya kuna rafiki yangu wa karibu sana (family friend) alipata majanga ya kifamilia kodi nyumbani ilimuishia, michongo alikuwa hana na mke wake alikuwa akiumwa sana aliniomba nimsaidie amalize suala lake la kodi nikamsaidia lakini baadae aliniomba nimkopeshe kama milioni 12 aende morogoro akafanye mishe za kilimo ila ndani ya miezi 7 atakuwa kasharejesha yote so kwasababu ya ukaribu wetu na jinsi nilivyomfahamu way back sikuwa na shaka na ombi lake.. dah niliingia benki nikamtolea milioni 12 akanishukuru akasepa yaani toka nimempa hiyo pesa sikuwahi kummwona tena maishani nilimtafuta sana baadae hata mke wake naye akawa hapatikani nilienda kwao kupeleka malalamiko yangu lakini ni kama walinipoza tu kwa maneno mwisho nikachoka na kuamua kupotezea ila iliniuma hii mistake.. usimuamini kiumbe anayeitwa mtu kupita kiasi..
Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha nyuma cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze ili wasikosee?
Hakika hili limetugusa wengi.Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.
Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.
Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.
Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
T☕️☕️☕️☕️☕️☕️☕️Nilipoenda na furushi langu la bangi Oysterbay Polisi, ili niwauzie FFU, maana niliwaona sehemu wakilipuliza, hivyo nikaona ni busara nikiwapelekea mzigo wa jumla
Inaitwa Handcap.Kuzaa kabla ya ndoa(Yaaaaani kuingia kwenye ndoa ukiwa na alama 3 mfukoni kabla ya mchezo kuanza).
duuu! PoleNajuta kuzaliwa afadhali nisingezaliwa mateso juu ya mateso
miaka 10 sasa naumwa ugonjwa usioeleweka sijui ni kansa ya ngozi ?
Nikienda hospitali madoctor wanasema siyo kansa napewa madawa tu siponi
namuomba Mungu achukue maisha yangu au aniponye lakini hakuna hata moja linalotokea
kweli dunia jalala
Ugonjwa wa ngozi ni tatizo dogo tu sababu baso unapumua ila kukata tamaa na kukosa shukrani huku ni kubaya zaidi, tatizo gani hilo mkuu linalokufanya uongee maneno mabaya namna hiyo, si useme tukusaidie? juu ya kila mwenye elimu pana mwenye elimu zaidi mkuu, salimia watu upate msaada.Najuta kuzaliwa afadhali nisingezaliwa mateso juu ya mateso
miaka 10 sasa naumwa ugonjwa usioeleweka sijui ni kansa ya ngozi ?
Nikienda hospitali madoctor wanasema siyo kansa napewa madawa tu siponi
namuomba Mungu achukue maisha yangu au aniponye lakini hakuna hata moja linalotokea
kweli dunia jalala
Lips cheilitis mkuu . Yani ngozi ya kwenye lips hubanduka na kutoka mdomo ote mwekundu nikila mbele ya watu wanaweza kutapika wote ngozi ikiguswa tu na maji inakuwa kama ukoko wa ugali just imagineUgonjwa wa ngozi ni tatizo dogo tu sababu baso unapumua ila kukata tamaa na kukosa shukrani huku ni kubaya zaidi, tatizo gani hilo mkuu linalokufanya uongee maneno mabaya namna hiyo, si useme tukusaidie? juu ya kila mwenye elimu pana mwenye elimu zaidi mkuu, salimia watu upate msaada.
Ni kama mambo ya London exhibition kwenye Industrial revolution wahuni USA,Japan, Belgium, Germany wakaiga, wakaboresha,wakamzidi aliyekuwa wakwanza kuundergo mapinduzi ya viwanda.Ahsante sana ...Niliwahi kukosea pia hapa nilikuwa talented kwenye fani fulani nikajindai kuonyesha hadharani na kila mtu alikuwa anajua finally kilichonipata najuta.
Hapa ndo ata mimi najutiaga ilifika hatua wanafunzi wenzangu walikuwa wananifuata kunipa ushauri niachane na makundi mabaya nipambane na kitabu daah nikaishia kuwashit leo najiona mjinga sana.Kuzembea kitabu, uwezo nilikua nao na ninao hata sasa lakini sikutendea haki muda niliokua nao hapo nyuma.
Najua upumbavu unaogandana na jina mwanafunzi hivyo sihangaiki kuambia toto la mtu lisome kwasababu najua halitanisikiliza
Ukiona hivyo kuna magonjwa ya kiroho, haya majonjwa hayawezi kukuacha kama wewe mwenyewe hujachukuwa hatua za kuacha tabia chafu/dhambi kama.Najuta kuzaliwa afadhali nisingezaliwa mateso juu ya mateso
miaka 10 sasa naumwa ugonjwa usioeleweka sijui ni kansa ya ngozi ?
Nikienda hospitali madoctor wanasema siyo kansa napewa madawa tu siponi
namuomba Mungu achukue maisha yangu au aniponye lakini hakuna hata moja linalotokea
kweli dunia jalala
100%Wasia wangu kwa vijana wenzangu, tumieni umri wenu vyema kila moyo wako unapopiga basi umeshapunguza idadi katika ile hesabu maalumu uliyoandikiwa, msihangaikie sana hii dunia kwani kwa namna yeyote hamuwezi kutoka hapa mkiwa hai.
Jambo la pili, mkitaka amani ya kudumu katika nyoyo zenu toeni viumbe wote na mumtie mola wenu aliyewaumba peke yake, hapo atawapatia wenza wazuri na wenye mapenzi kutoka kwake, atawapatia maisha mazuri na yenye kuwatosheleza, atawazidishia furaha na baraka katika maisha yenu, lakini mkirundika virus na bakteria wa kila aina humo ndani mtajuta na mtazidiwa na stress mpaka kupoteza muelekeo jumla.
Mwisho, ninajuta sana kuchelewa kugundua siri ya maisha ya furaha, nimetumia umri wangu kwa sehemu kubwa kuhangaika kuokota mawe kumbe pana mahali almasi zimejaa tele, kwa hasara hii kila mara nawaeleza watu wa karibu na ndugu jamaa na marafiki kuwa wasipate hasara kama niliyopata mimi wajiandae na siku yao ya kufa kwani hapo ndio mwanzo wa maisha ya kweli.