Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

1. Kutokupata kumaliza degree kwa muda maalum accordingly.
Nilipostpone Masomo kisa biashara. Na nilikua nimeshafika mwaka wa pili.
Nikarudi miaka miwili baadae , nilisoma kwa shida , nikamaliza kwa shida. kama una nafasi ya kusoma soma muda huo kijana usicheze na muda.

2. Ukiona unaweza kuzaa au kuzalisha. Zalisha mtu sahihi. Tuliza kichwa. Majuto yake ni hatari, haswa kama hujajipanga. Though upande wangu nilijuta kuzaa na mwanamke aliyekua wakupita tu. Nikaachana na chuma nilichokua mimekielewa na nilikua tayari nimeshawekeza maisha yangu, nilipoteza mwanamke na mali.
Nilianza upya maisha. kijana jitahidi sana hisia, kupunguza, jitahidi sana uzae ukiwa na mipango na maamuzi yako binafsi si ya rafiki wala mpenzi wako.

3. Ukipata hela miradi na mipango ni mingi usisubiri kwamba utaja pata mbeleni. Hicho ndicho chenyewe. Niliwahi pata hela nyingi sana nikiwa bado 20-25 nikachezea sana.
Nilipata shida sana kuzipata after miaka hiyo, bata la kila aina. Wanawake, roadtrips na marafika starehe za sinza zilinikoma. Kijana kua makini na starehe, fany huku unawekeza. Laki ni pesa kubwa sana.

4. Na mwisho, ujanja ujanja, umenicost sana, mbele ya wazazi ndugu na marafiki, kijana usiwe much know. Hii hupoteza sana muda, uwongo. Umenicost sana. Kijana jitahidi sana hapo.

Zaidi Threas tamu sana hii.
Huu ushauri mzuri sanaa
 
So sorry ila huezi jua, maybe ulikuwa unatengenezwa kuwa mtu safii princess ariana.
[emoji117]Fursa bado zipo , maana dunia ni Kama darasa Lina maajabu mengi.
Moja ya vitu ambavyo nilikuwa namlaumu mshua why hujawa kama mzee fulani, anakula rushwa ana pesa kedekede.
Akanijubu nimewawekea akiba ya jina. Baadaye mtapata faidaya jina. Sikuelewa.

Nipo kazini, kuna siku mmoja alikiwa kiongozi mkubwa ofisini kufanya ukaguzi, wakati akiwa mkutanoni kuna kujitambulisha, nilivyosema jina langu akasema namfahamu sana mzee wako ni mtu mwema sana. Mkurugenzj mtumie huyu jamaa vizuri kama anaishi kama baba yake ni faida kwenu.

Mungu si athumani nilihamishiwa kitengo kingine ambako kuna nafuu sana.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Kukimbilia kuwa na familia mapema kabla sijajiweka vyema kifedha.

Nimekwama mambo mengi ada unastruggle , chakula unastruggle, kodi unstruggle.

Huwezi kujilipua tena unakuwa na limit ya tyme in short ukishakuwa na familia maisha yanabadilika sana.

Bado napambana nije kuishi maisha ya ndoto yangu ingawa mpambano ni mkali sana.
Hapa huna Cha kujutia mzee Kuna watu walitamani kupata watt mapema kila unachoptia ndo ulichoandikiwa keep steel hustling buddy kila kitu kinawezekana
 
Kuamini watu kupita kiasi:
Naamini kabisa huwezi zungukwa na marafiki muda wote. Kuna wengine wanaokuzunguka si watu wazuri. Mfano watu ambao wanakusengenya na kukusemea mabaya. Watu ambao hawataki mafanikio yako.

Kuruhusu watu wajue mapungufu yako:
Wanafamilia au watu wa karibu pale wanapojua mapungufu yako wanayatumia kama fimbo ya kukuchapia. Angalia sana wa kumweleza mambo yako.
Hili nakubaliana na ww kw asilimia 200 hsa hapo kw ndgu
 
Kuna jamaa nilifanya naye Kazi... Tukatengeneza pesa ndefu Sana, na mgao wangu ulikuwa kama mil.17.... jamaa akanipiga zote...[emoji22][emoji22]..... Maninaaa! Jamaa sijawahi kuonana naye mpaka Leo... Yapata Miaka 8 Sasa....

Sijasahau.... Kila nikikumbuka nakwazika upya... Maninaaa![emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Habari zenu wananchi wa Taifa la JamiiForums, leo katika kutafakari kwangu nimewaza sana haya maisha kuna ups and downs nyingi sana ambazo zingine zina utata sana kutokana na makosa tuliyoyafanya huko way back na unatamani kuwasaidia wengine wasirudie makosa hayo.

Wakati nipo chuo mwaka wa tatu UDSM huko Tanzania nikipiga zangu Computer Science nilipata mchongo Nokia Siemens kuna mradi wa kusimika minara walikuwa wakifanya na walihitaji watu competent kwenye eneo la Network Systems nikapewa hiyo connection na nilipiga kazi kama mwaka hivi hela ilikuwa tamu ila bahati mbaya kuna rafiki yangu wa karibu sana (family friend) alipata majanga ya kifamilia kodi nyumbani ilimuishia.

Michongo alikuwa hana na mke wake alikuwa akiumwa sana aliniomba nimsaidie amalize suala lake la kodi nikamsaidia lakini baadae aliniomba nimkopeshe kama milioni 12 aende morogoro akafanye mishe za kilimo ila ndani ya miezi 7 atakuwa kasharejesha yote so kwasababu ya ukaribu wetu na jinsi nilivyomfahamu way back sikuwa na shaka na ombi lake..

Dah niliingia benki nikamtolea milioni 12 akanishukuru akasepa yaani toka nimempa hiyo pesa sikuwahi kummwona tena maishani nilimtafuta sana baadae hata mke wake naye akawa hapatikani nilienda kwao kupeleka malalamiko yangu lakini ni kama walinipoza tu kwa maneno mwisho nikachoka na kuamua kupotezea ila iliniuma hii mistake.. usimuamini kiumbe anayeitwa mtu kupita kiasi..

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kipindi cha nyuma cha maisha yako na ungependa wengine wajifunze ili wasikosee?
Kwenda advance badala ya Diploma.
Ndugu zangu advance ni kupoteza muda.
Over
 
Fanya mahusiano na soulmate wako, kuna watu roho zinaendana na kuna wengine hazitokaa ziendane, kuna watu ukifanya nao mahusiano ni sawa na ncha za sumaku zinazofanana, will always repel, wengine ni ncha zisizofanana, will always attract

Search for Billy Kimber
 
1. Kutokupata kumaliza degree kwa muda maalum accordingly.
Nilipostpone Masomo kisa biashara. Na nilikua nimeshafika mwaka wa pili.
Nikarudi miaka miwili baadae , nilisoma kwa shida , nikamaliza kwa shida. kama una nafasi ya kusoma soma muda huo kijana usicheze na muda.

2. Ukiona unaweza kuzaa au kuzalisha. Zalisha mtu sahihi. Tuliza kichwa. Majuto yake ni hatari, haswa kama hujajipanga. Though upande wangu nilijuta kuzaa na mwanamke aliyekua wakupita tu. Nikaachana na chuma nilichokua mimekielewa na nilikua tayari nimeshawekeza maisha yangu, nilipoteza mwanamke na mali.
Nilianza upya maisha. kijana jitahidi sana hisia, kupunguza, jitahidi sana uzae ukiwa na mipango na maamuzi yako binafsi si ya rafiki wala mpenzi wako.

3. Ukipata hela miradi na mipango ni mingi usisubiri kwamba utaja pata mbeleni. Hicho ndicho chenyewe. Niliwahi pata hela nyingi sana nikiwa bado 20-25 nikachezea sana.
Nilipata shida sana kuzipata after miaka hiyo, bata la kila aina. Wanawake, roadtrips na marafika starehe za sinza zilinikoma. Kijana kua makini na starehe, fany huku unawekeza. Laki ni pesa kubwa sana.

4. Na mwisho, ujanja ujanja, umenicost sana, mbele ya wazazi ndugu na marafiki, kijana usiwe much know. Hii hupoteza sana muda, uwongo. Umenicost sana. Kijana jitahidi sana hapo.

Zaidi Thread tamu sana hii.
Hii kitu imenikuta mwaka jana saivi naona life sio.. ila ni funzo ukikosea ni kupambana tu na changamoto
 
Back
Top Bottom