Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Kuchukua mkopo NMB wa miaka 7.wa 19500000kuja kupiga hesabu natakiwa kurudisha milioni 39 Ni aibu na kosa ambalo sitarudia maishani ninaishi kwa utumwa
Ulichukua ENZI hizo riba asilimia 22. Pole sana, kama halijaisha nenda kaliuze Crdb au pbz Wana asilimia 12 Sasa hivi, upunguze machungu hata ya milioni 2.
 
Kaza mkuu
 
Sinywi pombe,sivuti sigara, sivuti bange, sifatii la maisha ya watu, siyo mzinzi, sijawahi kumfitinisha mtu, kwenye ukoo wetu sina ambae nina ugomvi nae, sijawahi kuua,sijawahi kufanya mambo ya kishirikina, sijawahi kumtukana mzazi

Mimi sina lolote nalojutia katika dunia ni pesa tu sina ila nafuraha, sijihisi mwenye hatia yoyote
 
Mkuu ahsante kwa comment hii. japo sijaelewa hapo kwenye siri ya furaha. fafanua plz.
Naam mkuu, siri ya maisha ya furaha ipo kwenye kugundua malengo ya maisha na hili watu wengi wameshindwa kulielewa, ukijua umekuja kufanya nini hapa duniani basi utaelewa makusudio yangu.

Wanadamu wanakula, wanavaa, wanakunywa, wanaoana na wanafanya shughuli zao mambo haya yote ni ya njiani tu na ndio maana yana mwisho, hivyo lipo lengo kubwa sasa hapo ndio kwenye siri ya mafanikio.
 
Una matatizo makubwa sana kisaikolojia. Believe me
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…