Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani kubwa ulilifanya kwenye maisha yako na usingependa wengine walirudie?

Najuta kuzaliwa afadhali nisingezaliwa mateso juu ya mateso
miaka 10 sasa naumwa ugonjwa usioeleweka sijui ni kansa ya ngozi ?
Nikienda hospitali madoctor wanasema siyo kansa napewa madawa tu siponi
namuomba Mungu achukue maisha yangu au aniponye lakini hakuna hata moja linalotokea
kweli dunia jalala
 
Pole sana mkuu. Mkuu, usichoke kumuomba Mungu.
 
Wasia wangu kwa vijana wenzangu, tumieni umri wenu vyema kila moyo wako unapopiga basi umeshapunguza idadi katika ile hesabu maalumu uliyoandikiwa, msihangaikie sana hii dunia kwani kwa namna yeyote hamuwezi kutoka hapa mkiwa hai.

Jambo la pili, mkitaka amani ya kudumu katika nyoyo zenu toeni viumbe wote na mumtie mola wenu aliyewaumba peke yake, hapo atawapatia wenza wazuri na wenye mapenzi kutoka kwake, atawapatia maisha mazuri na yenye kuwatosheleza, atawazidishia furaha na baraka katika maisha yenu, lakini mkirundika virus na bakteria wa kila aina humo ndani mtajuta na mtazidiwa na stress mpaka kupoteza muelekeo jumla.

Mwisho, ninajuta sana kuchelewa kugundua siri ya maisha ya furaha, nimetumia umri wangu kwa sehemu kubwa kuhangaika kuokota mawe kumbe pana mahali almasi zimejaa tele, kwa hasara hii kila mara nawaeleza watu wa karibu na ndugu jamaa na marafiki kuwa wasipate hasara kama niliyopata mimi wajiandae na siku yao ya kufa kwani hapo ndio mwanzo wa maisha ya kweli.
kwa kweli vijana huwa tunajisahau mno kwenye maswala ya ibada,nakutenga muda mahususi kwaajili ya muumba wetu
 
Back
Top Bottom