Ni kwanini wilaya ya Kigamboni maendeleo yapo taratibu sana?

 
Kwanza mtazamo wa maendeleo kwa mtu. Inatofautiana mtu mmoja na mtu mwingine.

Kwa wale wanaoamini maendeleo ni watu kuwa wengi, mji kuchangamka, makelelele, vuruguvurugu, mara gari linapita, mara pikipiki zinakimbia, watu mara wana sherehe, vigoodoro wadada wanatikisa matako yao, mara huku bar, mara huku disko, mara singeli. Mtu ambaye kiufupi anaamini maendeleo ni amshaamsha, lazima atataka amshaamsha. Kuna wengine wanaaamini maendeleo ni huduma bora na utulivu pamoja na ukimya. Mara nyingi ni watu wenye pesa zao na wanapenda Sehemu ya kutulia na kurelax.


Sasa kwa uzoefu wangu ni kuwa bei ya viwanja ndio inaamua aina ya eneo, spidi ya kukua na kupangika. Maeneo ambayo bado watu wanauziana kwa kupima miguu na kiwanja ni bei nafuu lazima hilo eneo litakuwa na wateja wengi na kutachangamka ndani ya muda mfupi sana, ukilinganisha eneo ambalo kiwanja kimepimwa kitaalam na serikali, kwanza bei ni kwa square meters tena unaona square meter moja inacheza kuanzia 8000(porini) mpaka 30,000-50,000(sehemu iliyo na huduma) 55,000-85,000(sehemu iliyochangamka sana na yenye huduma zote na majirani wapo)

Maana yake kiwanja cha miguu 20x20 ambacho mtu anapata kwa 800,000 mpaka 1,600,000 ambayo ni bei hiyo watanzania wengi wa kawaida wanaimudu ndio kitanununulia haraka na kuendelea kwa haraka.

Ila 20x20 ikishakutana na wataalam wa ardhi waje waigeuze kuwa square meters zinakuwa 400sqm. Ambayo kwa bei ya kibosi itaanzia 4,000,000-8,000,000. Na sehemu yenye huduma itakuwa 12,000,000- 20,000,000. Sasa hizo bei za juu ndio bei za huko kigamboni. Sehemu iko porini mno ila bei milioni 20, na sasa Matajiri wao wanachukua maeneo makubwa tu kuanzia 10,000sqm mpaka 50,000sqm wengine mpaka 100,000sqm. Halafu wanakaa nayo wanatulia tena kwa bei ambazo ni highly overpriced mpaka 200m-500m. Maana yake huko kuja kuendelea bado sana. Mpaka hao Matajiri waanze kuja kuendeleza sio leo. Hawana njaa wala shida ya nyumba. Sanasana hao Matajiri wanatumia hizo hati ilikukopea hela benki ili kukuza biashara zao. Sanasana NMB na CRDB n.k.





Muda umefika serikali ikubali kupima ardhi na kuuza kwa bei nafuu kwa ajili ya wananchi wa kawaida bei ya square meters 1 iwe chini ya 2000. Masuala ya kuuza bei ya kiwanja bei juu kuanzia 10,000@sqm mpaka 50,000sqm hayasaidii wananchi.
 
Homboza sio dar ni kisarawe
 
Kwa io ujenzi holela ndio mji kuendelea si ndiyo?
 
Point of correction: Kuhusu gharama ya ardhi huwa wanauza ardhi kwa bei nafuu sana kusema ukweli.
Tafuta matangazo ya uuzwaji ardhi,utaona jinsi serikali ilivyokuwa ikiuza ardhi ya sqm 1 kwa 1,500 mpaka 2,000 pale Kigamboni.

Kwenye hiyo kiwanja cha 20×20, bei ya 800,000 mpaka 1,600,000 naomba utaje hiyo sehemu ambayo unaweza kupata kiwanja kwa bei hiyo...Dar hiii hiii.

Kigamboni ndiyo Wilaya yenye viwanja vya bei ya chini kuliko nyingine,viwe vimepimwa au havija pimwa...

Hayo maeneo ya ukanda wa Chanika, hebu mtutajie hizo Bar na Disco, zipo sehemu gani specifically.

Kubandana ovyo kwa nyumba haiwezi kuwa kipimo cha maendeleo.Kwa wastani nyumba moja ya Kimbiji, inajenga nyumba 5 pale Chanika.

Je,Mtatuambia Kunduchi Ununio hapaja endelea mana hakuna hamsha hamsha au Bunju B na Mabwe Pande yake au Mbopo nako.mana Kuna mchanganyiko wa majumba makubwa na mapori.
 

- Definition & meaning of development?

-Measures of development?

-Core value of Development?

-Objectives of Development?

-Level of Development?

-Indicator of development?

-Effects of development?
 
Umenipata hapo, Kuna maeneo meng sana yana mapori na kunajaa maji balaa sehem nying, kigambon eneo Dogo sana ndio limejengeka
Mnazungumzia Kujaa maji katika maeneo ya Dar.
Pale Boko,Kunduchi, Mikocheni,Mbezi Beach,Kariakoo,Kigogo.

Hivi huo ukanda wa Chanika mna ujua vizuri...mshafika Viwege (Majohe) nyie, mshafika maeneo ya ndani ya Buyuni,Zingiziwa kwenye majaruba ya Mpunga...
Huko njia ya maji hugeuka mito.
Yani kwenye hilo msi kurupuke na kukimbilia viwanja ,mtakuja lia.
 
Mkuu unataka watu wajenge katika mashamba ya mpunga yanayojaa maji seriously? Afu baadae waje waombe msaada serikalini kipindi cha mafuriko kweli? Hapa uzembe utakua wa nani?
Mpaka mwisho wa andiko sijaona kipi kifanyike ili kigamboni iendelee kama Chanika.....!
 
Wazaramo na wandengereko.
 
Sijajua ila nimekaa cheka... Naona freshi kabisa kabisa kwa wasiopenda fujo za dar...


Chanika nilienda 2017 kulikuwa kuna wazaramo tuu siku hizi unaweza potea...


Charles kilian toa neno kuhusi kigamboni yako
Hapa jamaa katukosea sana inabidi atuombe radhi au anaona kwa sababu wilaya yetu Ina mapori mengi😂😁🤣
 
Mkuu usitarajie kukajengeka ghafla kama utakavyo.
Maendeleo huenda hatua kwa hatua.
Asa unataka kote kujengeke haraka for which purpose??
 
Umenipata hapo, Kuna maeneo meng sana yana mapori na kunajaa maji balaa sehem nying, kigambon eneo Dogo sana ndio limejengeka
Kigamboni kubwa sana ndugu.
Je hata hiyo Sinza munayoisifia ilijengeka kwa muda mfupi????
Eneo huwa linaendelea kwa pull factors tofauti,haiwezekani tu kukurupuka eti Kigamboni yote ijengwe,kwa misingi ipi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…