Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Aangalie wabunge bungeni wanasema nini. Hao ndio wanawakilisha shida za wananchi.
Sijasema rais atembelee kijiji, bali nauliza atajuaje kuwa kama watumishi wake wanafanya kazi kiufasaha, mfano kama si kuingia mitandaoni asingejua kuwa huku mitaani vitendo vya ujambazi vimeudi.
 
Mlishakataa utawala wa majimbo huo ndio ungekuwa mfumo sahihi kwa nchi kubwa kama hii na sio huo wa kutaka Rais azurure vijijini akikagua kama shule zina vyoo au zahanati zina maji.

Tanzania in vijiji na mitaa zaidi ya 16,000 Hata Rais akiamua kila siku kufanya kazi ya kutembelea vijiji angalau 3 hawezi kuvimaliza kwa miaka 10 ya utawala wake.
Tanzania ni kubwa mkuu wangu ukikaa tu officen huwezi kupata yote kwa usahihi...
 
Mamaa mamaa mama huyo mamaa mama huyo mamaa mama.
Ye ni kuteua tu na kutumbuana sijui km kuna kazi zingine za kufanya.
 
Zile ziara za mwendazake zilikuwa za kujijenga kutawala zaidi ya miaka 10.
Na alishafaulu kuteka "wafuata mkumbo wengi pasipo kufikiria!" Genge la wapumbavu waliokaririshwa midundo wasioijua... wamecheza wee mwishowe wanataka kuingia kwenye mzinga wa nyuki na makelele yao....
 
wanyonge si mnyongwe tu
Ni jambo zuri Raisi kutembelea wananchi wake mikoani siku moja moja kukiwa na sababu ya msingi. Wakuu wa mikoa na wilaya ni wasaidizi wa raisi wa moja kwa moja ndio wenye wajibu wa kusikiliza na kutatua kero za kila siku zinazowakabili wananchi. Mhe. Raisi SASHA halazimiki kujihusika moja kwa moja kusikiliza na kutatua kazi zilizo chini ya wasaidizi wake!
 
Hapa ndipo mnapothibitisha kuwa ccm haifai, yaani kazi zote afanye rais hii nchi siyo duka la mangi.
 
Kwani huko alikoenda uganda na kenya hakuna mabalozi aje na huku kwetu dabaga tumwone kila siku tunamwona kwenye Tv tu
Swali kama hili akiuliza mtu ambaye ana uwezo wa kujisajili jamii forum, huwa sijibu.
Lakini angeuliza mwanangu junior ningejibu.
 
Kwahiyo Mama hatakiwi kwenda kwa wananchi? Ila ikifika wakati wa Uchaguzi Mkuu ndio aende sio? Washauri wa Mama Oyeeeeeeeee!!!!
Kuna kwenda kwa wananchi na kushinda kwa wananchi, mnachotaka wafuasi wa kichaa ni mama kushinda kwa wananchi, anunue mahindi,mapapai agawe laki tano tano.
Huyo atakuwa kiongozi au kichaa?

Kama kwenda kwa wananchi anaenda na ndiyo maana kaongea na wazee wa Dar es salaam kwa niaba ya wazee. Au unataka wananchi gani?
 
Kwamba unanambia rais anajua hayo yote akiwa barabarani kila siku akinunua mahindi na mapapai?
Dikteta anayetaka kutawala milele ndiyo huwa na hizo tabia ili kupata popularity.
Rais anayejielewa anakutana na wananchi lakini hawezi akawa anashinda barabarani kila siku kufanya propaganda.
 

Tuwe uchumi wa kati chini halafu tuendelee na tabia za banana republic? No taasisi; no watendaji; no mgawanyo wa madaraka? Rais anahudumia wanyonge wasiopungua milioni 40 moja kwa moja? Huo ni UONGO mkubwa.
 
Ule ulikuwa usanii tu. Wewe unaamini Rais anaweza kumaliza kero kwa kumsikiliza mtu mmoja mmoja kwenye mkutano wa hadhara?
It send a message. Kwamba Tltunawaangalia nyie wote, mkizingua, utatenguliwa.

Ni kitu kizuri alichoanzisha Magufuli. Uwajibikaji.
 
Mleta uzi nakuunga mkono.
Rais wa Tanzania lazima aijue Tanzania, ndani nje. Yeye si Rais wa dar au dom au zenj pekee.

Lazima akashuhudie changamoto za watu wake kwa kuwatembelea na kuongea nao. Huo ndio uongozi. Kuwa Rais wa nchi kubwa kama hii si kazi ya lelemama.

Msidanganye hapa kwamba asubirie dom au dar taarifa za wananchi wake. Hawezi kufika kila sehem lakin lazima awe na utaratibu wa kutembelea huko mawilayani. Lasivyo yale yaleee. Kwamba alikuwa Rais mzuri ila wasaidizi wake wamemuangusha
 
Kwaiyo ye akitaka kuja huku chini aje kuomba kura tu si ndiyo?
Mkuu, ndo wanavyotaka.

Ikikaribia uchaguzi au wakati wa kampeni ndo eti tuanze kumuona mara anaenda Sikonge, mara Liwale mara Songwe. Kwasasa hawataki. Wanataka wawe wanamlisha matango pori. Bosi kila kitu kiko shwari Rombo kumbe hamna lolote

Au wanamuonea huruma kuwa atakuwa anachoka?

Aende akashuhudie watu wake wanavyoishi hukoooo
 
Sina uhakika kama una uelewa na ulichochangia.
 
Mfumo wa uongozi uheshimiwe , Kila nafasi ina umuhimu wake, kama Kila Jambo tukimwachia rais atatue , tutalemaza viongozi wengine , watakosa ubunifu na uthubutu wa kufanya maamuzi yaliyo ndani ya uwezo.
Rais kama kocha kazi yake kubwa Ni kupanga timu yake vizuri, kuhakikisha nani anafaa kucheza namba fulani ,nani anazingua abadilishwe. So ukiona kocha anataka kuingia uwanjani anakuwa na tatizo, maana siyo majukumu yake na mwisho timu lazima imshinde,
Kuna majukumu mengi sana makubwa ya kitaifa ambayo rais anapaswa kuyatimiza.Hayo Ni mengine sio lazima kuyafanya
 
Tatizo ni kwamba watz sio waaminifu ndo sababu unaona mjuba alikuwa front!!! Hawa wateule wengi usipo wafatilia ni ujanja ujanja tu huko uraiani mkuu
Hapa ndipo mnapothibitisha kuwa ccm haifai, yaani kazi zote afanye rais hii nchi siyo duka la mangi.
 
Mambo gani makubwa unayodhani zaid ya kuwatumikia wananchi. Kuingia mikataba ya Gesi au? Rais ni Rais wa watu si Rais wakusafiri bila kuona tija ya safari zake. So unataka azurure mitaa ya Karen, Mombasa, Kasarani na si mitaa ya nchi yake! Ha ha ha!
We kenge kweli kuwatumikia wananchi ni kupi? Huko ikulu au kwenye ziara za nje anawatumikia mbwa au

Kazi ya Rais sio kufanya unavyotaka wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…