Kwa hiyo katiba mpya itakaa mlangoni kwa lissu kumlinda????
 
Hiyo namba 4 inaweza kuwa sawa...kuna watu sasa hivi ni maswahiba ndani ya chama tawala na upinzani
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.
Huu uzi na taarifa na muujiza wake utadumu kwa miaka 1000Mbele
 
Suspect namba moja ni wewe mtoa mada maana uchambuzi wote unaonyesha unavyotaka kupoteza ushahidi wakati ushahidi haufutiki.
 
Kat
Kwa hiyo katiba mpya itakaa mlangoni kwa lissu kumlinda????
Katiba Mpya itasimamia haki zote za watu na wanasiasa watoapo maoni yao hata kama ni mwiba kwa serikali iliyoshika hatamu!!

Hoja za kisiasa zitajibiwa kisiasa na sio kwa Risasi!

Pia Rais aliepo madarakani atapunguziwa madaraka hataweza kumziba mdomo yeyote kwa njia yeyote ile kama ilivyo Sasa!!

Nachelea tena:-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"!
 
Habari za ujenzi wa taifa wanajamvi.

Shambulizi la Tundu A. Lissu Lilitokea kipindi ambacho kulikuwa na mvutano baina ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Joseph Pombe Magufuri na mwanasiasa huyo Nguli Tundu Lissu.

Shambulizi hili lilitugawa watanzania mara mbili kama si mara tatu, yaani wanaokubali madai ya Tundu Lissu ambae ndiye aliyeshambuliwa (wote tunatambua madai yake) na wale wanaopinga kuhusika kwa aliyekuwa Rais wa JMT John Magufuri.

Binafsi kinachonifanya nipingangane na madai ya mshambuliwa ambae ametuhakikishia Watanzania kuwa JP Magufuri ndiye mhusika namba moja wa shambulizi hilo.

Sababu kuu ya kupinga hilo ni kuwa, Selikali ya awamu ya sita(6) chini ya Rais shupavu Samia Suluhu Hassan ilianisha uovu wote ambao ulifanywa na Rais aliyepita sasa hili la kushambuliwa kwa Tundu lissu mbona liwe gumu kusemwa hadharani ili watanzania tuujue ukweli na wahusika wa shambulio.

Namaanisha waliobeba silaha hatari na kwenda kumshambulia Mbunge asiye armed wala asiye na hatia wanyooshwe na mkono wa sheria kama ilivyofanyika kwa wahusika wa uovu mwingine, mfano aliyekuwa Dc wa Hai.

Mheshimiwa Tundu Lissu amejenga chuki kubwa sana na Hayati JPM akimfananisha na Nduli Idd Amin huku akidai Taifa la Tanzania lilipata ahueni baada ya kufariki kwa aliyekuwa Rais huyo, hayo yote ni kuamini kuwa washambulizi walitumwa na JPM jambo ambalo ni wrong100%.

NB: Mimi si sukuma gang.


Nawasilisha



Sent from my STK-L21 using JamiiForums mobile app
 
Mmemuuliza Mbowe vizuri? Mana Dr Slaa alisema Mbowe ana tabia ya kuteka na kuua watu wake. Interview ipo mitandaoni, akitolea mfano wa mwenyekiti wa CHADEMA wa Temeke alivyonusurika kuuawa na gaidi mbowe
 
Ungeweka na facts zinazofanya umkingie kifua dictator Jiwe ili zichambuliwe otherwise na wewe ni Sukuma gang mlinda 'legacy'.
Ushahidi wa mazingira unaonyesha ushiriki wa Jiwe kwenye mpango mzima wa jaribio lililofeli la kutaka kumuua nduli Jiwe, serikali(CCM) haina uhakika na reputations kama watalisanua hivyo wameamua bora waendeleze 'mute' iliyowekwa na utawala wa dictator Jiwe kuhusu hilo shambulio.
 
Bashite na cyprian msiba le mutuzi na wenzao ndiyo wanajua shambulio lote nenda kawaulize usitumie nguvu kuwasingizia chochote chadema
 
Hivi unahangaika nini wakati mwenyewe yupo?

Nenda kamuulize. Mnapenda kupoteza muda na nguvu kwa mambo ya kipuuzi.

Kwahiyo ukijua alietaka kumuua unapata nini?

Tafuta kujua namna ya kupiga pesa.
 
Hii issue haita kaa iishe....

Ila kuna siku wahisani wa kimataifa ambao wanatupa misaada wakisema jamani Serikali chukueni hatua za mwanzo.....

Basi itakuwa siku mbaya sana kwa Bashite... Ndiye atakuwa wakwanza kuhojiwa...
 
Kwakatibayetu mkuu wa kaya akiamua kukumaliza huchomoki.
Ukichomoka ujue hausiki kwa namna yoyote kwasababu anakila kitu kinacho hutajika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…