Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Dhana tu: Waliompiga risasi Tundu Lissu walikuwa na nio ovu ya kuhakikisha Taarifa ya Mh Rais Dr Magufuli kusafisha sekta ya madini esp Almasi na Tanzanite haiwi covered vya kutosha na vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi.

Hii ni dhana tu kwangu ila tuache vyombo vya uchunguzi viendelee na uchunguzi na upepelezi wao.
1. Kwani akisikia ye ni nani!!?
2. Kwani Taarifa hizo zimetolewa kwa ajili ya nani!?

Ifikie pahala tuache siasa za chuki na ubinafsi.

Hakuna mtu yeyote mwenye timamu aliyefurahishwa na kitendo cha kupigwa risasi Mh. Lissu. Kikubwa nikuweka maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu; Mh. apone haraka aweze kurejea katika shughuli zake za kila siku.
Huku vyombo vya usalama vifanye kazi yake kwa kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwawajibisha.
 
Dhana tu: Waliompiga risasi Tundu Lissu walikuwa na nio ovu ya kuhakikisha Taarifa ya Mh Rais Dr Magufuli kusafisha sekta ya madini esp Almasi na Tanzanite haiwi covered vya kutosha na vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi.

Hii ni dhana tu kwangu ila tuache vyombo vya uchunguzi viendelee na uchunguzi na upepelezi wao.
Mkuu, inaitwa
"To DIVERT ATTENTION" / KUJARIBU KUBADILI hali halisi ILI TUACHE hili la MADINI na WIZI/WEZI na TUJIKIMU kwenye kujadili JARIBIO la maisha ya Tundu Lissu.
Hawatafanikiwa
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.


1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.
wewe,eti unahuita ni uchambuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni nani adui namba moja wa Lissu aliyemfunga jela takribani mara 7?


Kwa haraka haraka watu watasema CCM inahusika, ila ukiangalia katika jicho la upelelezi unawezaona kuwa Lissu alitaka kuuliwa aidha na watu wenye mapenzi na nchi hii, chadema yenyewe ili kumfachua Magufuli, pamoja na baadhi ya maadui zake ambao pia yeye anadhani kuwa ni marafiki zake. Ujasusi ni kitu kinachotumia intelijensi sana ila kwa bahati mbaya watu hawafikirii au kuona mbali, matokeo yake wanakuja na hoja za kijinga kwa kunyoshea vidole wasio na hatia. My guess and knowledge inaniambia kwamba hapa CCM wala haiusiki.
 
Dhana tu: Waliompiga risasi Tundu Lissu walikuwa na nio ovu ya kuhakikisha Taarifa ya Mh Rais Dr Magufuli kusafisha sekta ya madini esp Almasi na Tanzanite haiwi covered vya kutosha na vyombo vya Habari vya ndani na nje ya nchi.

Hii ni dhana tu kwangu ila tuache vyombo vya uchunguzi viendelee na uchunguzi na upepelezi wao.
Hiyo sio dhana ni kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuntu. elite wamegawanyika Mkuu kuna beneficiaries na victims wa policy za Mkuu wa nchi.....kwa sasa pool za kila wizara zina victim wanaosubiri kupangiwa kazi...huwa najiuliza waliopunzishwa wakisubiri. so wanatia hasara tu. Kwa mini wasiende kufanyakaz za ujenz wa taifa hili....zipo nyingi tuuuuu.
Kweli mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi anafanya jambo la kizalendo, ila kuna watu labda wana tafsiri tofauti ya uzalendo kuhusu upinzani na ndo nacho kiona hapa
 
Najaribu kuwaza tu, meli iko baharini, na manahodha wetu na mabaharia wengine wako busy kutoboa meli,

Kuna wakati pia Hawa wemanahodha wetu unajenga shaka juu ya utimamu wa akili yao.

Jukumu LA kuwa na "nyundo na vifaa vya kar
akana" ni jukumu LA manahodha ndani ya meli, iweje meli itobolewe manahodha waseme hawajui?

Hii safari INA shaka, tulikotoka na tunakoenda si salama tena.
 
Wewe siyo siri n kutoka lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
Actually, mimi sina chama.

Namuunga mkono Magufuli kwa utekelezaji wake wa sera. Nawapinga CDM kwa sasa kwa ubabaishaji wao na kigugumizi chao kuhusu ufisadi na demokrasia ndani ya chama.

Tukipata utawala mwengine nitapima kuwaunga mkono au kuwapinga.

Hii ndio raha ya kutokuwa na chama. Huna ushabiki wa kinazi kama timu za mpira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inteligensia yao ya kufahamu matukio kabla ipo katika kugundua uhalifu utakao kwenye maandamano ya wapinzani tu! Nje ya hapo Inteligensia kapuni. Ajabu sana nchi hii!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabaharia hao hawajawahi kurejesha majibu.. Upepo ukipita na jambo linapita!
 
Back
Top Bottom