Ningependa nimjue mwanzisha mada kwanza, kabla ya kukomenti.
 
Sawa kabisa, wahenga wamenena ukitaka kumulika nyoka anzia miguuni. Lakini si lazima nyoka awe miguuni, maana yake ni kuwa ukianza kumulika mbali na kwa kutembea utamkanyaka nyoka na atakung'ata.
Kwa hiyo kama maadui wa Lissu wako CDM na ndiyo wanaomtibu akilala kitandani kwa matibabu itakuwa ndiyo kwaheri Baba wa CDM. Atakata kauli moja kwa moja.
 
Asante.Ni kama vile umeamua kujipofusha ila usione ukweli.Ata mwanangu wa chekechea anajua nani ni mtuhumiwa.
Ni kama vile Ronaldo apewe penati bila kipa golini alafu akaamua kupaisha.
Wahenga walisema "Common things occurs commonly".
 
Ujinga mtupu,nadharia haitakiwi kuonesha upande wako ila tu uhalisia wa nadharia yenyewe ili kila mtu achague mojawapo kati ya hizo na aweze kiwa muumini wa nadharia hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati mbaya watanzania hatuna muda wa kufikiri kutokana na chuki na kuichoka serikali yetu.

Jana nimemwambia jamaa yangu siamini kuwa serikali ilitaka kumuua Lissu, yani hadi urafiki umeisha..

Tatizo tuna jazba sana, na hatutulii katika maamuzi.

Siamini kabisa kwamba kama nina visa na Juma, na mtaa mzima wanajua, naweza kumuua, mana ntakuwa first suspect.

Icpokuwa, naamini kuwa kuna watu nlio na chuki nao wanaweza utumia uhusiano wetu mbovu to their advantages....

Ndo mana wahenga walisema mchawi mpe mwanao akulelee... Mana hata akilogwa na mwngne wote tutajua ni yeye tu... Hvyo lazima atamtibu...

<> semper fi <>
 
At the end of the day umeonesha unatetea upande gani na upo chama gani!! Ukweli kunasiku utajulikana tu na kuna watu wataaaibika!!
Kweli kabisa, sababu humo humo kwenye chama chao kuna "Power Struggle", ya chini chini, na wachunguzi walitegemea kitu sio kama hiki ila chepesi zaidi, naamini kabisa wanaohusika na na hili tukio ni wenyewe...
Mke au Mume akifa, uchunguzi waanza kwao, wanandugu na marafiki, simple...
 
MLETA MADA! Mimi binafsi najaribu kutafakari ili jambo/tukio na bado sijapata jawabu! Kuna chapisho flani nililisoma humuhumu JF, kama siku nne zimepita, kuhusiana na kambi mbili ndani ya chama ila nilibaki na wasiwasi kuhusu hilo chapisho na mtu aliyezungumziwa kuwa katika kambi inayokujaa juu au kupata umaarufu ndani ya chama ni huyu aliyeshambuliwa kwa risasi! Sasa, baada ya tukio la shambulio la jana, akili yangu imenifanya nikumbuke Kifo cha Marehemu CHACHA WANGWE kilichosababishwa na ajali ya gari, nimekumbuka tukio la Mh. ZITTO KABWE kuvuliwa uanachama, Beni saanane kupotea na mengine mengi hapa nchini. Haya matukio yanatokea baada ya kuonekana kuwepo kwa kambi moja kutaka kulinda maslahi yake dhidi ya kambi nyingine. Tunaliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili tupate ukweli wa ili jambo. Haiwezekani watu wetu ambao ndiyo tunaowategemea watusemee sisi wananchi ambao hatuna nafasi ya kusemea waumizwe na kuuwawa kiholela! Wahusika wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Kwani ambao wamempeleka mahabusu lissu mara saba hawajulikani???

Kwa nini asipelekwe mahabusu kama anahoja ya kujibu? hata mara mia anaweza kupelekwa. Hiyo sio hoja. Kuvaa kofia ya uwakili haina maana vyombo vya dola visimhoji kwa kosa analosemekana ametenda au anatenda. Tuache kuwa na mihemuko isiyo na tija. Tundu Lissu is a great man. hata mimi nampenda. Hicho kilichomtokea si sawa. Watu waliofanya hivyo watajulikana tu. Tuviamini vyombo vyetu. Vitafanyakazi. Vitaibua maovu hayo. Tuwe na subira.
 
Watu wanajitekenya na kucheka wenyewe
 
Ongezea Bashite...Jana alikuwa wapi na mbona hakupost kitu instagram... Acheni kuzunguka mbuyu...Nissan patrol nyeupe????hakuna MTU binafsi anatumia magari mabovu..chunguza mtaani kwako...Lissu anabounce back tutampa ulinzi magari hata kumi na atafukua siri zote hakuna kuacha kitu
 
Amlight umenichekesha. jana rafiki yangu nusura apewe talaka kwa kusema haamini serikali imemmiminia risasi Tundu.. Mimi mwenyewe siamini kabisa na wala sifichi hisia zangu. Umiminiaji wa risasi wa aina ile ni mtindo wa Zamadani. Serikali kama inania ya kumwondoa Lissu si kwa kumfatilia na gari mchana kweupe na kummiminia risasi! hivi masikio hayasikii na macho hayaoni? Lissu anaweza kuwa na maadui wengi tu kama wakili wa kujitegengemea. Mara ngapi tunasikia watu wanaua kwa vile wamenyimwa haki mahakamani? wameshindwa kesi "on technicalities ground"? sasa anayenyimwa haki akiwa na roho ndogo na stress ya ajabu anaweza kufanya nini? kuna scenario nyingi. Lakini No! No! No! hiyo sio kazi ya Serikali. Tuache kuipaka matope serikali jamani; Tumelogwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…