Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.
You are perhaps!
 
Hoja no.3 umetanguliza hisia zako Mbele zaidi kuliko kutafakari na kufikiri kwa Kina kwakua bdo ht km S/kali itakua imehusika ktk mchakato huo Uwezo wa CCM kuendelea kushikilia Dola ni mkubwa sanaa kwakua katiba bDo inampa Raisi nafasi kubwa zaidi(INAMLINDA)+Upinzani ht km utakua na Nafasi kubwa ya kushinDa na chama tawala kikachakachua matokeo hakutakuepo na suala la upinzani kukata rufaa ili uchaguzi urudiwe kwa kufuata Haki na Sheria,2005 mpk Raisi mstaafu anaapishwa mgombea mkuu wa Upinzani W.slaa alikua analalamika suala la kuibiwa kura zake na akafikia hata hatua ya kusema kwamba hamtambui Raisi mteule/aliyepo madarakani lkn baada ya Hapo hakikufanyika chochote So this is to reminD you that the first anD foremost key thing here is to change our Katiba,Halafu Issue ya kui neglect s/kali kwa hoja kwamba wtu wataionea huruma CDM ni kutoelewa kwamba hii Nchi illiteracy rate ni kubwa zaidi Maeneo ya Vijijini ambapo ukitembeza chumvi,kofia,fulana za rangi+Matamasha kadhaa n Lunch ya haja watu wanasahau shiDa na kurusha Mikono Juu so Chama tawala kina take Over,itizame hoja yko Vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii sinema ya Mbowe, anataka kuondoa ushindani maana jamaa amekuwa popular kumzidi yy, [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

Umesahau dhana nyingine wewe na watu wa namna yako mnaojipendekeza mpewe nafasi na serikali hii inayotaka kusifiwa tu. Uzuri wake mnatekeleza amri kutoka juu halafu mnakuwa wa kwanza kuanzisha thread JF.
 
Taifa liko katika mapito makali ya vita ya kiuchumi.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania yuko katika mapambano makali dhidi ya wezi na wahujumu uchumi,vita hivi ni ndani ya chama chake,ndani ya nchi yake,ndani ya washindani wa nchi za maziwa makuu na kwa upekee yupo kwenye vita na mabepari na wakoloni wa zamani na wakoloni mamboleo.

Wakati akipokea ripoti za wizi unaotokea kwenye makanikia mheshimiwa Rais alitahadharisha juu ya ugumu wa vita hii.

Ukiacha kutahadharisha juu ya usalama wa wajumbe wa kamati Mh Rais alitsahadharisha kuhusu usalama wake mwenyewe na of course usalama wa watanzania wazalendo.

Katika mapokeo ya tukio lililomkumba ndugu yetu na mtanzania mwenzetu ni vyema tukawa na mapokeo ya aina zote ambayo kati ya hayo moja tu ndio litakuwa sahihi baada ya uchunguzi.

Huu sio wakati wa kutukana,kuhemuka,kulaumu au kujiapiza bali ni wakati ambao watanzania wote bila kujali itikadi kutulia na kutafakari kwa kina sana.

Zipo conspirancy theiories kadhaa ambazo inatakiwa tuzimulike kabla ya kuja na misimamo mikali ambayo haitasaidia kujua ukweli wa jambo hili na hataonesha upendo au majonzi yetu ya dhati kwa Mh Lissu.

1-Tundu lissu alikuwa ni maarufu kwa kupinga sera za Rais Magufuli na CCM na ameingia kwenye migongano kadhaa iliyoko mahakamani dhidi ya Serikali ya CCM pengine hata kabla Magufuli hajaingia madarakani.

2-Tundu lissu alikuwa ni mwanaharakati wa mazingira haswa katika uharibufu wa mazingira katika maeneo ya migodini na ameandika articles nyingi dhidi ya wachimbaji wa madini wa kutoka ughaibuni.

3-Tundu lissu ni mwanasheria kitaaluma na amesaidia wengi katika kesi mbalimbali na amewaumiza wengi kwa maana hii katika kesi mbalimbali.

4-Tundu lissu kwa weledi wake katika sheria anaweza kuwa ni asset muhimu ya serikali kitaifa na kimataifa kama leo tulivyoelezwa na mheshimiwa Rais kuhusu professa Mruma.

5-Tundu lissu ni mwanaChadema 'asili' ambaye potentially angeweza kuwa mgombea urais 2015 au hata 2020.pia anaweza kuwa bado ni mkereketwa halisi wa vita dhidi ya ufisadi na aliyeamua kupingana na ufisadi ndani ya Chama chake.

6-Tundu lissu kwa weledi wake anaweza kuwa ni muajiriwa wa makampuni ya uwekezaji katika madini ambayo kwa sasa yapo kwenye mgogoro mkubwa na Serikali au pengine yako kwenye mgogoro au ushindani mkubwa kati yao wenyewe.

7-Tundu lissu ni mwanafamilia ambaye ana mke na watoto na hivyo huwezi kumuondoa kwenye migogoro ya kawaida ya kifamilia.

8-Tundu lissu ni mbunge ambaye kwa level za kibongo ni tajiri kwa kiasi chake kiasi cha kuvutia majambazi wanaoweza kuhotaji mali zake.

9-Tanzania ni nchi salama na thabiti kisiasa ambayo inaweza kuwa under attack ili tu ionekane hakuna amani nchini mwetu.

10-Tundu lissu sio exceptional kwa vichaa tu wenye hamu za kuchukua uhai wa watu hasa hasa watu maarufu kwa sababu za kuwapendezesha watu hao.

Kwa ufupi zipo theories nyingi zinazoweza kutujulusha kwa nini shambulio hili kwa mheshimiwa lissu limetokea .

Tujadili kitaalamu kwa kila mwanaJF na utaalamu wake wakati tukisubiri ripoti za vyombo vya ulinzi na usalama.

Mada hii ijadiliwe kwa weledi zaidi kuliko mohemuko au itikadi zetu za kisiasa
.....
......maji hayazoleki
 
Naanza na kutoa pole kwa watz wenzangu juu ya Mh.Lissu kwa janga lililomkuta..
Kwamfano Siku imetokea Mara Mungu amejaalia hao wahalifu wakakamatwa na IKIBAINIKA kua serikali haikuhusiana kabisa na matendo hayo..
HAO WENYE KUISHUTUMU SERIKALI YETU YA AWAMU YA 5,JE NYUSO ZAO WATAZIWEKA WAPI??

Sent from Calculator Phone vesion007
 
Kumekucha tena .naona mmeshaingia kazini .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naanza na kutoa pole kwa watz wenzangu juu ya Mh.Lissu kwa janga lililomkuta..
Kwamfano Siku imetokea Mara Mungu amejaalia hao wahalifu wakakamatwa na IKIBAINIKA kua serikali haikuhusiana kabisa na matendo hayo..
HAO WENYE KUISHUTUMU SERIKALI YETU YA AWAMU YA 5,JE NYUSO ZAO WATAZIWEKA WAPI??

Sent from Calculator Phone vesion007
Mbona mnajishuku si mkae kimya msubiri watu wafanye uchunguzi wao??:
 
Naanza na kutoa pole kwa watz wenzangu juu ya Mh.Lissu kwa janga lililomkuta..
Kwamfano Siku imetokea Mara Mungu amejaalia hao wahalifu wakakamatwa na IKIBAINIKA kua serikali haikuhusiana kabisa na matendo hayo..
HAO WENYE KUISHUTUMU SERIKALI YETU YA AWAMU YA 5,JE NYUSO ZAO WATAZIWEKA WAPI??

Sent from Calculator Phone vesion007
Acha Ujinga...mwombe mama yako nauli uende shule, au kojoa ukalale mtoto! Kwa akili yako kwanini isiwe serikali? Na kwa akili yako ndo umekaa hapo unasubiri Sirro amkamate Magufuli au Paul Makonda, au yeye mwenyewe Sirro na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wajikamate kuwa ndo walihusika kutaka kumwua Lissu? Acha ujinga dogo
 
Serikali haikwepi na wala hawana pa kutokea
Police ccm bashite wanahusika
 
Back
Top Bottom