Uchambuzi wako na hypothesis zako ni nzuri sana, ila umesahau kitu kimoja tu, je silaha zilizotumika kumshambulia ni za aina gani? Je hao raia wa kawaida wanaruhusiwa kua nazo? Je Lissu ni wa kwanza kua mwiba kwa serikali? Je umaarufu wake kwa kuisumbua serikali unazidi wa Mrema na Dr. Slaa?
 
Hii nchi ina viumbe wanafki sana.

Ni nchi hii watu wamevamia mkutano wa CUF na hakuna lolote lilitokea.

Mtu kavamia kituo cha redio na bunduki mpaka sasa yupo kazini.

Mtu kamtolea bastola Nape mbele ya waandishi wa habari na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Waliomteka Roma mpaka sasa hawajulikani. Kweli?

Ben Saanane mpaka sasa hajulikani halipo na waliompoteza hawajulikani.

Hizi analysis mnaandika bila kusema haya yote. Punguzeni unafki.
 
Tukio la leo la kujaribu kumuua Tundu Lisu, limetupaka matope kama Taifa, katika kipindi hiki ambapo tunatafakari jinsi ya kujenga uchumi wenye viwanda. Binafsi nina laani kitendo hicho. Ninakumbuka Jaji Mstaafu Warioba, alitaka tuunde katiba mpya yenye kusisitiza Tunu za Taifa, ingawa hatukufika mwisho wa mchakato huo, lakini ulikuwa unatupeleka katika kuenzi UTANZANIA.. UTAIFA kwanza.
 
Jaimee

Nikas Mahinda was my colleague. Mauwaji yake yalikuwa na uashiria wa ujambazi na business dealings. Sidhani kama yalikuwa ya kisiasa. Nisahihishe kama nimekosea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapo ambao lazima wawe maadui wa Lissu. Wa kwanza wasioheshimu katiba na sheria za nchi.
 
Lord knows.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…