Tokea mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni T Lisu apigwe risasi mchana kweupe kuna nadharia kadhaa zimeibuka kujaribu kuelezea huo upigwaji risasi wa Lisu.
Lisu mwenyewe alipotembelewa na makamu wa rais akiwa Nairobi alikiri wazi kuwa hawajui waliompiga risasi na kuviachia vyombo vya dola vifanye uchunguzi wake.
Ingawa hivi majuzi akiwa ubeligiji ameibuka na kuihusisha serikali na upigwaji wake risasi.
Nadharia nyingine inatokea ndani ya chama cha chadema ,gazeti la Jamvi la habari wameelezea A to Z kuwa Lisu alipigwa risasi baada ya kutishia uenyekiti wa Mbowe. Wameeleza siku chache kabla ya kupigwa risasi kulikuwa na vikao kadhaa vya wanachadema wakimtaka Lisu agombee uenyekiti.
Pia aliyekuwa mbunge wa Ukonga na mjumbe wa kamati kuu ya chadema naye alinogesha nadharia hii baada ya kuelezea namna watu wanavyopata misukosuko wakitangaza kugombea uenyekiti ndani ya chadema.
Waitara alihusisha kufa kwa Chacha Wangwe ,kutaka kulishwa sumu kwa Zito Kabwe ,kupigwa risasi kwa Lisu na yeye mwenyewe kutishiwa kushughulikiwa iwapo atagusa kiti cha mwenyekiti ndani ya chama..
Kama kweli Mbowe anasingiziwa kwenye tuhuma hizi za kuuwa watu wanaotaka kugombea uenyekiti ndani ya chama basi aende mahakamani kutaka kusafishwa na tuhuma hizi.
Mbowe akiendelea kukaa kimya bila kuwaburuta mahakamani wanaomtuhumu basi , mamilioni ya watanzania watajua ni kweli
View attachment 829281View attachment 829284