Ili kupata majibu rejea Katiba ya JMT. Huko, ukiwa na macho yanayoona utaona majibu kwa uwazi. Nilidhani watu wangedai na kuchukua za kuuvunja muungano, lkn hili hawalifanyi kwani wanatamani kuiona Zanzibar na Wazanzibari wakiwa ni watawaliwa wa Tanganyika asilimia mia moja lkn hawatofanikiwa.
Pale Mtanganyika kutoka Tanganyika isiyoonekana anapokuwa rais na kuwa na madaraka juu ya Zanzibar na Wazanzibari kwao sio Tatizo, ila Mzanzibari kutoka Zanzibar inayoonekana anapokuwa rais na kuwa na madaraka juu ya Tanganyika na Watanganyika, kwao ni tatizo. Huu ni ugonjwa. Mungu awaponye. Dawa ya hili ni kuuvunja huu muungano, kwahivyo, fanyeni hivyo ili hii fitna iondoke. Tuwache kulialia kiuongouongo.