Mkuu
Tlaatlaah Ngoja Nikusaidie maana huwezi kupata Unachotafuta kwa sababu..
Ukisoma vizuri mkataba wa Muungano utaona kuwa Waziri Mkuu ndiye Msaidizi wa Rais wa Muungano kwa masuala yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar ndiye Msaidizi wa Rais wa Muungano kwa masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar. Kama ilivyo Rais wa Zanzibar hana
mamlaka huku bara vile vile Waziri Mkuu hana mamlaka yeyote kule Zanzibar
Mkataba wa Muungano ndio rejea pekee la masuala ya muungano. Articles of the Union zimeanzisha Mamlaka 3, Mambo ya Muungano chini ya Rais wa Muungano, mambo yasiyo ya Muungano kwa Tanganyika chini ya msaidizi mkuu
wa Rais wa JMT ambaye 1964 alikuwa makamu wa pili wa Rais...
na mwisho ni mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar ambaye ni msaidizi mkuu wa Rais wa JMT ambaye 1964 alikuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa kwanza wa Rais. Waziri Mkuu wa Tanzania ndiye huyo makamu wa pili wa 1964.
Baadaye Ndo kikafutwa Cheo cha Makamu wa Pili wa Muungano Kikaanzishwa Cheo cha Waziri Mkuu na kikaanza kutiliwa Mkazo...