Swali linabaki kuwa, huko serikalini hawapo watu wenye capacity ya kumjibu TUNDU Lissu Kwa HOJA?
Jibu la hili swali ni jepesi sana.
Jibu sahihi ni HAKUNA.
Unataka nifafanue kidogo hilo jibu?
Ni hivi: Serikali unayoisema ni ya CCM. Watumishi wake wote, hata hao akina AG ni mali ya CCM
Hebu niambie, wewe una kifaa chako, ni mali yako, kwa mfano nguo, au jembe. Si utavitumia kadri unavyoona wewe inafaa?
Lakini nisikuache na dukuduku kuhusu ufafanuzi wangu huu. Inanibidi nifafanue tena hiyo CCM na viongozi waliopo huko kutoweza kujibu swali lako pia.
Ni hivi: CCM ni chama cha unafiki. Ndani ya CCM hakuna anayeweza kumwambia mwenzie ukweli, hata kama ukweli huo uko wazi.
Muundo wa CCM ulivyo, tazama CC (Central Committee), wajumbe wake, na hata Halmashauri Kuu ya Chama hicho uwiano wa wajumbe wake, toka Tanganyika na Zanzibar.
Hawa wajumbe wa Tanganyika, hata siku moja utasikia wakiwagomea chochote wale wa Zanzibar; hasa katika maswala yanayohusu Zanzibar. Kwa hiyo maamuzi yanayochukuliwa kuhusu Zanzibar, ni uamzi wa wajumbe toka Zanzibar.
Asikudanganye mtu kwamba mambo ya Zanzibar yanaamuliwa na watu wa Tanganyika. Hao akina Jumbe kuachishwa uRais, ni waZanzibari ndani ya CCM ndio walikomaria swala hilo, na kuungwa mkono na akina Mwalimu Nyerere, kwa vile Jumbe alikuwa anashindana kulegeza muungano, ambao uliasisiwa na akina Mwalimu. Mwalimu asingekubali kuona juhudi zake zikisambaratika.
Kuna hizi stori za viongozi wa Zanzibar kuchaguliwa Dodoma. Huu ni uongo. CCM Zanzibar ndio huchagua viongozi hao, na kutegemea wenzao wa Bara kuhakikisha chaguo lao linapita kwa njia yoyote, hata kwa kumwaga damu.
Looo, nitatiririka hadi wapi sasa. Natumaini umenielewa mkuu 'Rabbon', pamoja na wasomaji na wachangiaji wa mada yako hii.