Ni neno gani baba yako alitamka ambalo unaliishi mpaka Leo!

Ni neno gani baba yako alitamka ambalo unaliishi mpaka Leo!

Ikiwa Leo ni siku ya baba duniani?
Nakumbuka mzee wangu aliwahi kusema "hakuna mkamilifu asilimia kwa Mia kwa mia na hakuna mbovu asilimia mia kwa Mia kila mtu ukimtumia vizuri kuna fursa atakupa"

Lakini aliniambia usioe kwa kuangalia umbo bali
"Angalia ni mchezaji gani unayemtaka unaamini ukimsajili katika timu yako Ataleta matokeo unayotaka"

Vipi kwa upande wenu wanajamvi
Ni maneno gani ambayo baba yako alitamka mpaka Leo unalikumbuka na kuliishi?

Karibuni kwa michango 🤝
Usiwe na mazoea ya kwenda kazini kumtembelea mkeo, nakujuwa mwanangu ulivyo na hasira, kwani unaweza kwenda huko ukakuta kapakatwa na mtu mwingine akakuambia walikuwa wanataniana tu.
 
Dingi "Aim high Your Failure will be a Success"

My BIG bro akakazia " urithi wetu sisi ni ELIMU"

naishi navyo hii leo
 
Ikiwa Leo ni siku ya baba duniani?
Nakumbuka mzee wangu aliwahi kusema "hakuna mkamilifu asilimia kwa Mia kwa mia na hakuna mbovu asilimia mia kwa Mia kila mtu ukimtumia vizuri kuna fursa atakupa"

Lakini aliniambia usioe kwa kuangalia umbo bali
"Angalia ni mchezaji gani unayemtaka unaamini ukimsajili katika timu yako Ataleta matokeo unayotaka"

Vipi kwa upande wenu wanajamvi
Ni maneno gani ambayo baba yako alitamka mpaka Leo unalikumbuka na kuliishi?

Karibuni kwa michango 🤝
Usiendekeze mwanamke asiye na muda nawe, atakupotezea muda
 
".. nilisoma mpaka nikakuta kibao no more school.. elimu niliyonayo hakuna atakaeifikia hata mmoja.."
Na mwaka huu narudi darasan OUT nifanye masters mpaka nionyeshwe kibao alichoonyeshwa yule mzee.
 
mzee wangu aliniambia usingizi ni mali ila haujawahi mfanya mtu atoke sehemu moja kwenda nyingine kwenye maisha yake......... nimekua nikijifunza watu wengi wasiopiga hatua ukichunguza vizuri usingizi na kulala lala ndio chanzo kikuu cha wao kuwa chini.......

alikua ananimbia huwezi kuwa binadamu kamili unalala ndege wanawahi kuamka wanajaza mtumbo yao ww bado umelala...... R.I.P MZEE WANGU.
Unaamka unaenda wapi huna kazi
 
Mzee ni hadhi anayopewa mtu yeyote mwenye umri mkubwa bila kujali uhusiano baina yenu lkn kwa baadhi ya jamii za Afrika Mashariki zinatafasiri neno Mzee na hutumiwa na wanawake kwa maana ya kuwatambulisha waume zao kwa badala ya kusema huyu ni mme wangu basi wao husema huyu ni MZEE WANGU.

Kwani ukesema BABA ungeliulizwa tofauti ya umri wenu au ilikuwakuwaje akawa baba yako?
Huna hoja unataka tu ubishani
 
Baba yangu aliniambia mtu ukipotezana nae kwa miaka 2 mkija kukutana huyo ni mtu mpya kwako humjui maana anakuwa amebadilika .
Mama yangu yeye alinikataza kabisa kuomba especially hela anasema shida yoyote jizuie lakini hakuna kuomba hata kwa ndugu, pia nisiwe na tabia ya kukopa kama nahitaji kufanya kitu nijiwekee akiba nikizidiwa sana nikope kwa ndugu wa karibu tu nayo nilipe kwa wakati kama tunavyokubaliana.... Mama yangu alikuwa mtu muadilifu mnoo mimi pia nimekuwa muadilifu sana kupitia yeye
 
Natamani ningesikia neno toka kwa Baba lakini alifariki na kutuacha wanaye tukiwa wadogo sana.
Mungu Mwema, tuko tunaendelea kupambana na maisha
 
Back
Top Bottom