Ni neno gani baba yako alitamka ambalo unaliishi mpaka Leo!

Usiwe na mazoea ya kwenda kazini kumtembelea mkeo, nakujuwa mwanangu ulivyo na hasira, kwani unaweza kwenda huko ukakuta kapakatwa na mtu mwingine akakuambia walikuwa wanataniana tu.
 
Dingi "Aim high Your Failure will be a Success"

My BIG bro akakazia " urithi wetu sisi ni ELIMU"

naishi navyo hii leo
 
Usiendekeze mwanamke asiye na muda nawe, atakupotezea muda
 
".. nilisoma mpaka nikakuta kibao no more school.. elimu niliyonayo hakuna atakaeifikia hata mmoja.."
Na mwaka huu narudi darasan OUT nifanye masters mpaka nionyeshwe kibao alichoonyeshwa yule mzee.
 
Unaamka unaenda wapi huna kazi
 
Huna hoja unataka tu ubishani
 
Baba yangu aliniambia mtu ukipotezana nae kwa miaka 2 mkija kukutana huyo ni mtu mpya kwako humjui maana anakuwa amebadilika .
Mama yangu yeye alinikataza kabisa kuomba especially hela anasema shida yoyote jizuie lakini hakuna kuomba hata kwa ndugu, pia nisiwe na tabia ya kukopa kama nahitaji kufanya kitu nijiwekee akiba nikizidiwa sana nikope kwa ndugu wa karibu tu nayo nilipe kwa wakati kama tunavyokubaliana.... Mama yangu alikuwa mtu muadilifu mnoo mimi pia nimekuwa muadilifu sana kupitia yeye
 
Natamani ningesikia neno toka kwa Baba lakini alifariki na kutuacha wanaye tukiwa wadogo sana.
Mungu Mwema, tuko tunaendelea kupambana na maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…