Ni rahisi sana Afrika (Tanzania) kurudi utumwani

Si waisraeli pekee wanao ongoza kwa IQ,

Hata wazungu wana IQ na maarifa yaliyo pelekea wawe na teknolojia bora na za kisasa kwenye kila nyanja za maisha.

Sasa naku uliza hivi,

Waafrika wemebarikiwa IQ gani?
Mungu aliumba WANADAMU wote wakiwa na 1. Akili 2. Hisia 3. Uwezo wa kufanya maamuzi.

1. Sie waafrika tumebarikiwa na Kila kitu, Nchi zetu ni za joto ndomana hatukutaka hata kujihangaisha kutengeza nguo, ambapo mzungu Kwa baridi alilonalo lazima aumize KICHWA Ili kupata mavazi ya kumkinga baridi asife.

Mwarabu Hana maji, Wala chakula, naye kabarikiwa mafuta Ili ayatumie kusurvive.

Wazungu kadhalika, wamenyimwa raslimali, hivyo kuishi lazima waumize KICHWA sana.

Wote Waafrica, Wazungu, Waarabu tunazo akili, lakini tunatofautiana maamuzi ya kutumia akili zetu.

Maana imeandikwa, Awazavyo mtu ndivyo alivyo.

Mungu aliyetuumba na kumweka Mzungu Nchi mbaya baridi, Akamweka Mwarabu jangwani na kumpa mafuta, akamwumba mwafrica na kumpa Kila kitu, akitaka tuishi Kwa kidaidiana, tufikie WIN WIN SITUATION.

Narudia kusema,

Kumcha Mungu ndicho chanzo Cha AKILI, HEKIMA, MAARIFA na UFAHAMU.
 
Je mikataba iko sawa na atakavyofanya hapa?
 
Sasa unafikiri mzungu, Mchina, Mhindi atakubali kukosa access ya hivi vitu muhimu kwenye magari ya umeme, mobile phone, all computers, vitu muhimu kwa ustawi wao na cuvilization yao.

Hapo muhimu ni Afrika kuungana itakuwa na sauti kubwa, equal patner with USA, EU, China, India etc. Kwahiyo itaweza ku- negotiate bei nzuri na masharti, vigezo muhimu kuhusu assets zake.
 
Adui wa Mwafrika ni Mwafrika mwenzake na Sio Magharibi.
Kupigana wenyewe kama ni wanyama ni matokeo ya laana,hao Magharibi wanapakaziwa bure hawahusiki na hili
 
Mama wa kambo kama chief mangungo
 
Je mikataba iko sawa na atakavyofanya hapa?
Mikataba ya kibiashara itakuwa imeandikwa kisasa na yenye kulinda maslahi ya wafanya biashara wazalendo.

Tunautazama mkataba wa IGA kule bungeni kama ndio kila kitu wakati ule ni ufupisho tu wa biashara nzima itakavyofanyika.
 
Bora ya wakoloni kuliko wawekezaji.
Wawekezaji ni wezi mkoloni alikuja kuijenga Africa,sema tu kiherehere Cha wapigania Uhuru waliangalia maslai Yao binafsi na Sio ya waafrika wote
 
Adui wa Mwafrika ni Mwafrika mwenzake na Sio Magharibi.
Kupigana wenyewe kama ni wanyama ni matokeo ya laana,hao Magharibi wanapakaziwa bure hawahusiki na hili
Una Elimu Gani?

Hapo congo wanapigana bila mkono wa wageni?

Mwafrica Hana viwanda vya silaha, nani analeta silaha kama karanga Ili wapigane wao wakitorosha raslimali?

Halafu Leo Eli tueasifie wazungu Eti Wana akili Kwa kupora Mali zetu na kuua ndugu zetu!!
 
Bora ya wakoloni kuliko wawekezaji.
Wawekezaji ni wezi mkoloni alikuja kuijenga Africa,sema tu kiherehere Cha wapigania Uhuru waliangalia maslai Yao binafsi na Sio ya waafrika wote
Wawekezaji ndio hao hao wakoloni, wamebadili tu namna ya kuiba!!
 
inasikitisha sana,,ukimwangalia mtu km Samia na ungedere anaoufanya...inatamani angepigwa mawe mpaka afe mbele ya Kadamnasi...Wako wapi kina Ibrahim Traore,Asimi Goita katika Majeshi yetu...Hakuna uzalendo Jeshini kusema sasa ni basi???je wanajeshi wetu hawana Elimu ya kuongoza hii nchi,kwa nini wasiichukue??
 
Nikiwaza jinsi Magufuli alivyokuwa akisakamwa naona bora turudishieni utumwani dawa iingie
 
Bora maisha ya Mwafrika zama za ukoloni kuliko baada ya uhuru.
Uhakika wa ajira,kujiajiri,uhakika wa soko la mazao, elimu, matibabu,kwenda Ulaya ulikuwepo
 
Inashangaza kuna jeshi la kulinda amani DRC miaka 30 sasa ila hakuna Amani. Wanalinda nini?

Waasi wana silaha hatari sana kama ilvyokuwa Msumbiji, Angola (UNITA), Zimbabwe, South Afrika.

Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia Ulaya yote ilikuwa hoi, Ujerumani, Japan, France, Italy, UK na zingine zilikuwa na magofu bila ajira, basic nessesities of life.

Chini ya miaka 15 wakapiga hatua kubwa sana kurudi kwenye ubora wao. Sisi miaka 62 tunaongelea yale yale basic stuffs maji, umeme, elimu miundombinu. Akili ipo wapi?
 
Kama Wasomi wataendelea kujitenga na Siasa za Nchi zao basi tutegemee hayo kutokea.

Haiwezekani eti Kigezo cha Kuwa Mbunge eti Kujua kusoma na kuandika.

Alafu hao hao tutegemee watunge sheria za kulinda rasilimali zetu🙆‍♂️

Kutawaliwa hakuepukiki kwa mtindo huo
 
Mimi si mmoja wao.
Laana ni matokeo ya kutoukubali uafrika wako
Umeukubali uafrika umeukubali upumbavu sasa tafuta njia bora ya kuuondoa huo upumbavu ili wewe na kizazi chako kisiumizwe na huo upumbavu(uafrika)
 
Sawa.

Utumwa ulifanywa na mwarabu pekee ?
 
Mikataba ya kibiashara itakuwa imeandikwa kisasa na yenye kulinda maslahi ya wafanya biashara wazalendo.

Tunautazama mkataba wa IGA kule bungeni kama ndio kila kitu wakati ule ni ufupisho tu wa biashara nzima itakavyofanyika.
Dear Steven, nadhani tuache kuumauma, mkataba wowote lazima uwe na maslahi kwa wote. Meanwhile mwekezaji ni lazima alindwe, nasi pia tunapaswa kulindwa bila kuathiri biashara ya mwekezaji.

Je mkataba huu unatulinda sisi? Umetoa mfano DP wapo England na kwingineko, Je, mikataba yao ni ya aina hii ya kwetu? Katika nchi za dunia ya I na II ni wapi DP wana mikataba ya aina hii kama Tanzania? Tupe mifano tafadhali.
 
Laana ili hali wageni wanakuja na bag tupu wanaondoka na mabulungutu.
Wanasema Africa njoo na akili tu pesa na mtaji utavipatia Africa.
Kupitia ardhi hii hii wanapata mkopo bank wanazalisha wanachota pesa wanapeleka kwao
Kama sio laana hiyo ni nini Sasa?!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…