Ni sehemu gani ya nchi, mji au Kijiji ulifika mpaka ukajiuliza watu waishio huko walifuata nini?

Nilipanda mlima uluguru nikakuta waluguru huko juu Tena wanavijiji vyao Hali ya hewa ilikuwa nzuri ila huduma za kijamii Hadi uteremke mlima, binafsi nilishuka miguu inatetemeka na maumivu makali mno. Mpaka Leo nawashangaa watu Kule wanavyoishi
Mongwe au wapi
 
Nilikua singida kijiji kimoja hiv kule ziwani kuna milima ina nyoka wakubwa usiku wanashuka sasa bwana siku nasikia milio kama ya bata usiku nikakutana na mijoka mikubwa inatafuta maji saa saba na nyumba za nyas juu zina uwaz daaaah
Usingizi ulikuja kweli kesho yake aukuondoka?
 
kuna jamaa yangu mchaga kabisa pure ukoo wa kileo ila cha kushangaza kila X mass anaenda kula kwao ila kwao sio moshi ni ngorongoro hili swala nimelitafakari hadi nimechoka mchaga na ngorongoro na ndio kwao baba mchaga mama mchanga babu mchaga ukoo wa kichaga 😂😂
 
Ikawaje? Hujamalizia kuelezea umeishia katikati
Ilikua ukwen inabid uoneshe udume nikakomaa siku saba maana kuna maajabu mlima ule kuna wakat upepo ukivuma unasikia kelele za watu wanashangilia kama goli la mpira kijiji cha mingera singida karibu na misri
Singida kuna ziwa?
Ndio mr sijui ziwa ziwa mto maana wanavua masamak makubwa makambale na perege had mamba wapo ukigoogle kuna ziwa singidani ila kuna mto mkubwa sanaaa shelui kule kwenyw mgod kwa mbeleee kabisaa wenyeji kama wapo watakuelekeza
 
Asee pole mzee😂
 
Shelui Uelekeo Wa Chini Kwenye Milima Wanasema Bwawa Lina Kamongo Wengi Sana
 
Aisee
 
Bora hata mpanda, kuna mahali panaitwa MAJIMOTO aisee huko nilipoenda nilijiuliza qatu wamefuata nini, na wengi wao ni wasukuma kule...Ajabu ni kwamba they are making money ile hatari. Ni matajiri wa kutupwa kutokana na kilimo ufugaji na madini.
masimoto usevya kuzuri mbona kuna wasukuma wapo vizuri kweli pale
 
Kondoa vp
 
Mikoa mingi iko hivyo mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…