Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo mmoja unaimba dunguru dunguru du Basupa wa wenge musica, naombeni jina lake please.
 
Mwenzenu nimekumbwa na kimbunga
Si kimbunga cha upepo Bali kimbunga
Cha mapenzi mama
Toka siku ile ya kwanza nilipomuona
Msichana mrembo jully nilishindwa kujizuia nikamweleza wangu ukweli yakua
Nimpenda nae akanijibu jully asante kwakunipenda.dah wakuu hii ngoma hatari aliimba Bob ludara jina silijui nisaidieni niupate
 

Attachments

wa,dau kina nyimbo alikuwa anaitumia gadna g abassh kama back ground akiwa anaongea, ktk jahazi enzi zile, anajejua anitumie, sikumbuki jina
 
Mwenye wimbo Wa wachuja nafaka uitwao 'ya Leo kali' anisaidie pliz nmeutafuta mwaka Wa pili huu cjaupata
 
Natafuta saaana nyimbo ambazo mara nyingi zilikuwa zikipigwa kwny kipindi cha *mtaa wa mangoma* pale radio one na mzee mzima deogratius rweyunga
 
Kuna wimbo wa mr blue wa kwanza kabisa unaitwa blue blue. Sijawahi kuupata
 
Kuna nyimbo ya kuabudu inaitwa Hosana ndie Mungu wetu ameimba chidumule kama sikosei, mwenyenayo please
 
Ninaoutafuta ni wa zamani kidogo, nakumbuka nikiwa Dodoma kwenye Mwaka 1981 walikuja Marquiz Du Zaire wakapafomu kwenye uwanja wa Jamhuri, moja ya wimbo ulionigusa sana unaitwa CCM. Mimi sio mpenzi wa ccm, lakini naupenda huo wimbo nimeutafuta kwenye mtandao sijafanikiwa kuupata. Naongolea Marquiz ya Ogelea Piga Mbizi ikiwa na King Kiki, Supreme Ndala Kasheba na Nguza
 

Attachments

Back
Top Bottom