Nikiwaona Vijana wanaograduate, Nawahurumia sana

Nikiwaona Vijana wanaograduate, Nawahurumia sana

Nakumbuka graduation pekee niliyowahi fanya ni ya chekechea. Nna allergy na hayo matukio.

Kuna binti amegraduate diploma ya ualimu DUCE, hii wiki yote anapost mapicha yake ya mahafali kwa status whatsapp.

Kubwa kuliko leo kapost status kaweka caption, "Kama nawakera na nyie mkasome [emoji3][emoji3]" asilolifaham ni kwamba kuna graduates wa course yake tangu 2015 na hawana kazi.
 
Wakuu leo katika pita pita zangu nimepita njia ambazo zina vyuo,
Mabibo(NIT) na Uhasibu (TIA).

Na leo kwenye vyuo hivi kuna Mahafali.

Watu ni wengi sana kwenye hayo maeneo.

Nimejikuta nawaonea sana huruma vijana hawa waliovyaa majoho yao na wamejipamba vizuri sana sura zao hasa wadada.

Nimereflect tu hali ya kitaa ilivyo. Nikawahurumia tena.

Hivi kuna ulazima sana?

Natamani wafanye kimya kimya.

Anyway Mungu awasaidie.

Tuwaombee Vijana.
kila mtu ana bahati yake mkuu, amini kwamba uliemuacha chuoni anaweza kupata fursa ya ajira kabla yako
 
Nakumbuka graduation pekee niliyowahi fanya ni ya chekechea. Nna allergy na hayo matukio.

Kuna binti amegraduate diploma ya ualimu DUCE, hii wiki yote anapost mapicha yake ya mahafali kwa status whatsapp.

Kubwa kuliko leo kapost status kaweka caption, "Kama nawakera na nyie mkasome [emoji3][emoji3]" asilolifaham ni kwamba kuna graduates wa course yake tangu 2015 na hawana kazi.
🥹 Namhurumia sana!!
 
Maisha lazima yaendelee na kila mtu ana mipango yake,

Ajali za Ndege zinatokea ila watu hawaachi kusafiri,Ndoa zina matatizo ila watu hawajaacha kuoa au kuolewa Ajali za Magari kila siku ila kila siku watu wananunua Magari,

Maisha lazima yaendelee,kila mtu angekua na mawazo kama yako basi hakuna kitu kingekua kinafanyika hapa Duniani coz kila kitu kina faida na hasara zake.
Moja ya comment bora sana.
 
Taasisi za fedha zipo nyingi sana zinawahitaji ila wawe na uvumilivu katika kipindi chote cha kupata ajira. Kuhitimu taaluma hiiyo si lazima waajiriwe wote, wengine watalazimika kufanya shughuli ambazo hawakuzisomea, wajiandae kisaikolojia kuwa na altenative way kufanikiwa maishani mwao
......wengine watalazimika kufanya shughuli ambazo hawakuzisomea......

(Part of Thinking And Be Able To align Yourself Out Of The Box)
 
RC ahitimu ni wengi, fulsa ni chache, na hii sio bahati mbaya,au, imetokea tu, kwanini China, UK, USA, hakuna shida ya, ajira! Kwanini ni Afrika/bongo tu?
Kenge waliopo madarskani, wanachoona cha maana ni kuweka bajeti ya kununua magari kila mwaka! Na, kutengeneza maataasisi mengi yasio na tija! Wakavunja Sumatra, wakazaa latra,na zote zinafanya kazi zile zile,
Mambo ya k upuuzi ya nchi hii,
Hatuna haja ya kuwa na wabunge 350+! Unaweza ukaishi kyelwa, au, murongo boda, au, nanyumbu mtambaswala, na changamoto zako zikajulikana Dar!
Hatuhitaji wilaya tano dar, zilishawahi, kuwa tatu, ziliongezwa kisiasa, tu!
Dar, pwani, morogoro, unaweka RC mmoja, futa baadhi, ya mikoa, unganisha,
Kopesha, sekta binafsi ijenge viwanda! Ukitembea Afrika, miradi mikubwa inafanywa na mchina! Kwanini, sio, wazawa! Hv ukienda china, au, UK, unaweza ukaona daraja, linajengwa na wanaijeria?
Punguza wizara,punguza magari seriaklini, mawaziri, wakuu wa, mikoa, DC, polisi,ma DeD, Rac, wote hawa watumie usafiri binafsi!
Msafara wa raisi, atumie gari mbili tu! Fukuza madereva wote, kila mmoja ajiendeshe, hawezi aache kazi, uza ttcl,air tz, na iweke TBC chini ya management ya sekta binafsi, Azam au ipp media.
 
Watakavyoliwa rushwa ya ngono sasa inatia huruma sana, wahitimu wangepunguzwa maana hadi degree imeshuka thamani kama dollar ya Zimbabwe.
Zisipunguwe Ila Kila taaluma iwe na professional body ambayo itatunga Mitihani migumu ya Kupata ithibati kama nbaa, na bila kufaulu hiyo Mitihani hupati ajira.
 
Back
Top Bottom