Nikiwaona Vijana wanaograduate, Nawahurumia sana

Nikiwaona Vijana wanaograduate, Nawahurumia sana

Ndogo kwako ww ila kwa sisi wasaka tonge ni kubwa ....ndo maana nkimpa graduate 50k anafurahi lkn nkikupa ww 500k unaona ndogo
Akikua atakuacha 50k ngoja aje mtaani . Mtu mwenye kudumu nawewe atakufungulia kitu ujiendeleze atakusupport for a few months ukijiweza anakuwa anatoa pale umekwama
 
Kuna haja gani ya kupoteza mamilioni kusomesha WAUZA CHIPS?? 😝😝

Nilikuwa naangalia takwimu za HESLB, ni MABILIONI yanateketea vyuoni kulipa ada ya MABODABODA WATARAJIWA 🤣

As an experienced investor, i would call this a Business with no commercial value.

Ni upumbafu, unachota mabilioni unayamwaga hewani PWAAAH halafu unakenua.

Hayo MABILIONI YA MIKOPO bora wangewapa wafungue biashara kuliko kupoteza muda kwenye SIFURI.
Hv umeshawahi kukanyaga darasani kweli!?

Watu wanasoma ili kutanua ubongo/ kuongeza maarifa
 
Binafsi sipendi mtu hana one alafu anasoma chuo kikuu... Watu walitakiwa wakasome cookery pale zoom college leo hii wapo pale udsm wanasoma sheria...
Siku hizi madogo wanapata division 4, wana D zao za masomo ya sayansi. Wanaenda kusoma diploma ya utabibu vyuo vya private.

Wanafaulishwa na kutoka na GPA nzuri baadae unawakuta wanaenda kujiendeleza kusoma degree ya udaktari na wanaajiliwa. Mwisho wa siku wananchi wanalalamika huduma za afya mbovu [emoji3]. Ndipo tunapoelekea kama taifa!
 
Hii picha imesema yote
255621183362_status_4ea119a57992493d85f72fec488a3d2c.jpg
 
Siku hizi madogo wanapata division 4, wana D zao za masomo ya sayansi. Wanaenda kusoma diploma ya utabibu vyuo vya private.

Wanafaulishwa na kutoka na GPA nzuri baadae unawakuta wanaenda kujiendeleza kusoma degree ya udaktari na wanaajiliwa. Mwisho wa siku wananchi wanalalamika huduma za afya mbovu [emoji3]. Ndipo tunapoelekea kama taifa!
Niseme ukweli huu ni uongo hakuna mtu anajiriwa kama hajapitia field na kama hukuelewa darasanj hushindwi kujiendeleza kimaarifa ukiwa field na hupewi kazi kama kazi kama hujui unachofanya
 
The problem ni hii hatuna tena vichwa vinavyoitwa wasomi kama zamani! Kulikuwa na magenus aisee! Watu wabunifu, watu wenye maono! Sio wezi!
Sasa hivi hakuna tena wasomi labda tunao waliofuta ujinga tu kwa maana ya kujua kusoma na kuandika! ila kusema wanesoma hakuna! Huko serikalini kuna bunifu zipi mpya na wanaajiri wasomi kila kukicha!!? Umeshaona kwenye TV hata siku moja hakuna afisa anakagua mradi asiagize ocd kuwa kamata weka ndani!!? Kisa wameiba! Yaani ukweli nashauri serikali ianzishe kuajiri kwa kupima uwezo wa ubunifu na uaminifu! Otherwise wizi as usual! Hata wakiwa wanachagua vyuo utawasikia, “ Daahh yaaani hii course ukipata shavu serikalini yaani ndani ya mwaka kama hujajenga ghorofa utakuwa fala”
I dont trust anyone who said nimesoma nchi hii otherwise aniambie amefuta ujinga tu!
Wanaibaje hawa wasio ajiriwa. Wezi ni hao wasomi wazamani ndio mafisadi wqkubwa kuanzia wabunge, mpka wasimamizi wa miradi yote. Vijana hawa husiki usiwasingizie
 
Mnapewa cheti kabla ya gradu?

Basi nimekukosa, nilitaka nije 😂🙈🙈

Graduu tamu ukiwa na uhakika wa ajira. Hapo utacheza sebene na kukata mauno ya hela yote mixer kutikisa wowowo kimgandisho.

Sio unagraduate kwenda kuuza chips, hata mood inakata ,😂😂
ni transcript, cheti kama cheti ni baada ya graduu
 
Niseme ukweli huu ni uongo hakuna mtu anajiriwa kama hajapitia field na kama hukuelewa darasanj hushindwi kujiendeleza kimaarifa ukiwa field na hupewi kazi kama kazi kama hujui unachofanya
Kwa nyongeza!
Vyuo vyote, both private na public vinasimamiwa katika mfumo mmoja wa NACTEVET
 
Mmoja Facebook kasema atapost mfululizo picha za ku graduate mpaka tuseme.
Siku kwao wakimchoka na ajira akikosa nadhani ataacha kupost
 
Kwahyo watu wasiende tena vyuo.?? Vyuo vifungwe watu wasielimike siyo.?? Unakosea sana mkuu wacha wafurahie kumaliza chuo nayo ni mafanikio pia,, hayo mengine watajua wao wenyewe suala la ajira ni gumu dunia nzima sasa due to high population growth na resource za uzalishaji bado zipo chini.. Ila all in all siyo wote wanaograduate wanakuja kuteseka kitaani kuna wengne washatengenezewa mifumo na kuna wajanja wengine walijitengenezea wenyew mifumo wakiwa vyuoni huko...
 
Maisha lazima yaendelee na kila mtu ana mipango yake,

Ajali za Ndege zinatokea ila watu hawaachi kusafiri,Ndoa zina matatizo ila watu hawajaacha kuoa au kuolewa Ajali za Magari kila siku ila kila siku watu wananunua Magari,

Maisha lazima yaendelee,kila mtu angekua na mawazo kama yako basi hakuna kitu kingekua kinafanyika hapa Duniani coz kila kitu kina faida na hasara zake.
Kabisa mkuu, acha vijana wafurahie maana ni haki yao, kugraduate sio kitu kidogo. Kila mtu aliyefikia kiwango hicho bila shaka alipitia hali hiyo pia( kusherehekea). Sio kosa maana kusherehekea ni jambo lingine na kupata kazi either ya kujiajiri/kuajiriwa ni jambo lingine pia. Kila jambo lina nafasi yake na wakati wake pia.

Japo kiuhalisia ana point!
 
Back
Top Bottom