Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Nilichojifunza Nanenane: Kufanya Kazi Halmashauri ni kupoteza muda na kukaribisha umasikini tu

Maonyesho yoyote yanatafuna Sana hela. Ningekuwa kiongozi ( jambo ambalo siwezi) ningefuta maonyesho yote na semina na warsha zote zifanyike online with zero cost. Watu wanasafiri, wanalipwa nights, wanaandaa mabanda ya gharama, wanahamisha VIFAA vya ofisi mwishowe wanayavunja mabanda hayo utafikiri ni zile nyumba za udongo za watoto.
Kasome "multiplier effect" kwenye uchumi.

#YNWA
 
Basi ni wewe tu na hiyo Halmashauri yako unayotoka ndio mma njaa. Mbona wengine wamelala sehemu nzuri tu ma tumekuwa rate ya 220,000. Mbona rate za sasa zinafanana kwenye taasisi zote zinaanzia 100,000- 250,000 per day. Muonekano wa Mabanda unategemea na maandalizi ya Halmashauri ila usi generalize.
Kwa mwaka wangu wa 20 kufanya kazi Halmashauri, Halmashauri sio kubaya ila inategemea na wewe unajishughulishaje baada ya kazi. Kama baada ya kazi unapiga masanga huku kuitegemea Posho na mshahara au mipigo utaendelea kuwa maskini na mlalamikaji ila ukijishughulisha nje ya kazi, mambo bum bum.

Sijaongelea mapato nje ya kazi.
Kwa mapato nje ya kazi kila mtu ana akili zake na wizi wake.

Naongelea ile Equality mbele ya serikali ya CCM.

Mbele ya serikali ya CCM watumishi wa TAMISEMI ni makapuku, ndio maana mwenye bachelor kama yako ana mshahara mara mbili kuliko ule uupatao halmashauri.

Achana na side hustle za watu (kila mtu na akili zake)

Nazungumzia kipato cha kazini.

#YNWA
 
Kwanini usijiajiri mkuu? Naamini mishahara kwa watumishi wa umma imepishana kidogo kwa kada husika,labda uwe mwanasiasa ndio utapiga pesa.

Lakini katika ajira za kutumikia umma wote tupo katika mtumbwi mmoja

Hapana hayupo wote mtumbwi mmoja.
Mfano:-
Wewe na Mimi wote tuna degree ya uchumi kutoka chuo kimoja.
Tukaajiriwa serikalini.
1. Aliye ajiriwa TAMISEMI (halmashauri = Afisa mipango) mshahara ni TGS D (745K - 780K)
2. Aliye ajiriwa BRELA (Taasisi = Registration officer) mshahara ni 1.6Mil - 1.8mil

Ni mtumbwi mmoja gani huo usemao?

#YNWA
 
Tatizo huko Tamisemi ajira zake zinapatikana kiurahisi, hakuna cha kutazama wenye GPA kubwa, hakuna cha kufanyiwa interview, yaani mnazolewa wote kama kumbikumbi.
Hujui usemalo
Mimi niliajiriwa halmashauri kwa interview za written na oral.
Ukiwa unaandika uwe Unafanya kwanza uchunguzi.

#YNWA
 
Hakuna asiyetaka maisha mazuri.
Juzi nimelalia Mbeya pazuri.
Nikiwa Niko full na Castle lite zangu kichwani nikamropokea mkurugenzi wangu ""Uchaguzi wa 2025 hauwezi kunikuta kwenye halmashauri yako" yaani Mimi na li-masters langu nifie kijijini. HAIWEZEKANIII

Aliniangaliaaa akanijibu "Pombe hizo" [emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji2960]

#YNWA
Mpaka madereva wanatushinda kwa posho
 
Ukifanya kazi Halmashauri,halafu ikawa Halmashauri ya vijiji mchoko, Kama Kilimanjaro unakuwa mtumishi daraja la mwisho kabisa.
Kwani Halmashauri za Kilimanjaro ni choka mbaya sanaa?

#YNWA
 
Back
Top Bottom