Nilikamatwa Morogoro stesheni ya SGR nikituhumiwa kusafirisha chupa ya mil.500 ya maji ya kunywa!

mkuu sheria ni mbaya ndio ila usilete siasa kila mahali,
Hata nchi tukiwapa Chadema haitakuwa unafanya kila unachotaka, na hio sheria haitafutwa hata kije chama gani
Mkuu kwani siasa ni marufuku au ni jambo exclusive kwa sehemu au watu fulani tu? Maisha na matendo yetu yote yanaongozwa na siasa. Jambo ambalo watawala wa CCM wameweza kuwaghilibu watanzania ni kuwaaminisha kuwa siasa haiwahusu au siasa haina uhusiano na kila kitu wanachofanya. Hiyo sheria ni matokeo ya uongozi mbovu wa nchi na uongozi ni siasa.
 
Mkuu, hizo ni sheria kwenye biashara, hata kwenye ndege hupandi na maji, uwe ulaya au bongo,
Na huko ni CCM ?
Kwenye ndege ni kwa sababu maalum, kwa huzijui niambie nikuelimishe. Halafu kwa taarifa yako hawakazi maji per se!
 
Dunia nzima ipo sheria hiyo,si kwenye train tu hata kwenye ndege uruhusiwi kuingia na chupa ya maji,siku yake nenda hata pale kwa mkapa stadium kata tiketi halafu uende getini na chupa yako ya maji kama utaruhusiwa
 
Pole sana, ndani ya mabehewa wanauza maji yao, ulitaka kuwakosesha pesa[emoji2][emoji2]
 
Mimi nisingeyaacha mezani kwa afande ila ningemwaga yote au kunywa yote palepale
1. Hivi mle ndani ya SGR kuna vyoo?

2. Ukishikwa na haja ndogo au tumbo la kuhara inakuwaje?(swali hili litakuwa valid endapo swali la kwanza ni HAPANA)
 
hiyo hiyo chupa ya afya 500ml wanakuuzia elfu moja huko ndani. Yaani kuongozwa na watu wasiokuwa na akili kunahitaji moyo wa uvumilivu mkuu. Pole sana...watu wanatumia minguvu badala ya akili
 
Fuata masharti hutapungukiwa chochote, labda walichokosea kukutreat kama muhalifu!
Niliwahi acha lotion Songwe Airport iliniuma sana basi tu!
 
Tujifunze kufuata sheria. Kama sheria hairuhusu maji hata kama ni ya sh mia hayaruhusiwi. Hivyo tukijifunza kufuata sheria wala hatutakuwa na malalamiko na tutaishi maisha ya furaha. Kama sheria inasema maji hyaruhusiwi na wameweza kuisimamia nawapongeza sana. Leo tutaruhusu maji ya miatano, kesho ndoo ya samaki, keshokutwa ulanzi mwisho wa siku watu wanaanza kupanda na kuku, mbuzi ng'ombe .

Tuulinde huu mradi kwa wivu mkubwa. Hata ukiona jirani yako anafanya vitu visivyo sawa toa taarifa.
Mungu ibariki tanzania, Mungu ibariki TRC
 
Wanakataza watu kupanda maji lakini hawajali wakipanda na kunguni mwitu
 
Dunia nzima ipo sheria hiyo,si kwenye train tu hata kwenye ndege uruhusiwi kuingia na chupa ya maji,siku yake nenda hata pale kwa mkapa stadium kata tiketi halafu uende getini na chupa yako ya maji kama utaruhusiwa
Dunia gani umetembea wewe? Nmefika mabara yote lakini sijakutana na ujinga wa kunyima watu kuingia na maji kwenye treni. Unasema uwanja wa Mkapa, hili linaeleweka, ni uwanja wa mpira. Unachanganya madawa.
 
Mkuu kwenye flight, tunaruhusiwa kuingia na chakula vinywaji na kuvitumia humohumo kwenye flight?.

Na sgr ndio iko hivyo kama flight, zimetumika pesa zenu za Kodi na tozo, kuweni na huruma jamani na pesa za serikali.

Hatuwezi kuruhusu watu waje na vitumbua, bagiya, mayai ya kuchemsha, wali wa maharage, humo ndani ya sgr itakuwaje, ?
 
Lalamiko la msingi bei ya vyakula humo kwenye treni haiendani na huku kitaa, huko kwenye ndege misosi wanatoa free

Sasa mtu unamzuia kuingia na chakula au kinywaji chake halafu unamuuzia kwa bei kubwa haileti mantiki yoyote zaidi ya kuhalalisha wizi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…