Nilitumia miaka mitano ya kujenga nyumba ya ndoto yangu, inawezekana vijana tusilale

Hakuna nilipojisifia Bali naeleza uhalisia wa maisha yangu na bahati mbaya kabisa hunifahamu na ndio maana humu wengi tunatumia fake Id kwa sababu Kama hizo.
Vumilia kidogo maana ntakuja kueleza pia kilimo Cha papai nilichofanya kwenye shamba la ekari 20 bagamoyo, ardhi ilikuwa hairuhusu papai lakini nili-force na ikawezekana, Vuta subira ntaeleza na utajua nilipata kiasi gani
wewe ni kiduku lilo uliepooza
 
[emoji23][emoji23][emoji23]basi mama njoo kwangu na begi me ntakupokea, achana na huyo ambaye hataki uende kwake na begi.
Wala mm vya kuja navyo ninavyo vingi tu ila kiualisia sivileti coz mm mwanaume ninaekuwa nae nilivyo navyo lazima awe navyo i mean kwa age yangu.
Sana sana kwa mwanaume nabeba nguo kidogoo, vyeti vyangu, simu yangu na bichwa langu.😂 i mean akili zangu.

Lazima tuishi kwenye nyumba ya mwanaume. Hii ni sheria.
 
Leo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.

Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.

Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.

Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.

Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.

Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.

Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.

Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.

Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.

Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)
Enzi za mwendazake ungestahili kutiwa mikononi mwa vyombo vya dola na kufanyiwa uchunguzi baada ya hapo kesi ni muhujumu uchumi mkubwa.
 
Binafsi mtoa mada nimemwelewa, lengo la uzi wake ni kuinspire kundi la vijana wanaoona majumba mazuri na magari mazuri watu wanayasukuma wakaona kama yanamililiwa na aliens

Savings ndo kitu cha kwanza kabisa ili uweze kumiliki kitu cha ndoto yako

Yeye amesema anaweza kusave 1.8 kwa mwezi , sio msahafu wewe save hata elfu kumi tu kwa mwezi ,

Vijana tupende kusikia habari kama hizi zinasaidia kututoa usingizini , sio kila siku tunapenda kusikia story za wakina Gigy na ambaruti
Sijui Amonaizi

Pia me kwa experience yangu ya ujenzi pesa kubwa niliyoitafuta kwa mpigo ilikuwa kununua uwanja na kupaua lakini mengine kila nikipata pesa nanunua vifaa namuita fundi anajenga pesa ikiisha natafuta nyingine.

Usidharau pesa unaiyoipata ,kama unaina 350,000 ni ndogo hata milioni 10 utaiona ndogo coz utaishi kulingana na kipato chako
 
Tujiulize tu haya magari tunayoyaona road kwan wanaishi sayari ya 6? Nashangaa watu wanapenda kubisha bisha tu
 
Hapana kwa hapa sikuungi mkono..kila.mtunana dream.house yake..kumbuka hapa kajenga zaidi ya miaka 8 nyuma mkuu...kwanza nyumba ni finishing mkuu...hapa unakosea mno
Kabisaaaaa hlf hajajitangazaa ni ametoa km motivation kwa wengneee pyuuuuu yaani binadamuuuu utadhan wao wanavyoletaga nyuzi humu waga wanajitangazaaaa
 
Tena wanakuj kwa force balaa...ugumu wa maisha huo..
 
Tujiulize tu haya magari tunayoyaona road kwan wanaishi sayari ya 6? Nashangaa watu wanapenda kubisha bisha tu

Tujifunze kuwa positive , hizi pesa ndogo unazipata zinaweza kufanya vitu vikubwa hadi ukashangaa , tupunguze gharama unnecessary hasa mademu, kuvaa nguo za gharama ,mastarehe yasio kuwa ya lazima,kumiliki masimu ya gharama ,ishi sehemu inayoendana na kipato chako
 
Ukiweza hayo kwakweli lazima utapanda tu
 
kwani lengo lako kuleta uzi lilikuwa baya kiasi hicho!!!kwanini unapewa mrejesho unawaka!!!!

1.8ml kwa mwezi hiyo siyo ya kufungulia uzi hapa jf,utaonekana unatukana watu.sijui utasema ni mawazo ya kimasikini au vipi whatever.

ila wacha nikichanganue uone uko nafasi ipi maishani hapa.

kama ni reserved balance hiyo means una zaidi ya kipato cha 3mln/month.

sijui ni biashara ama ni muajiriwa,ila kama ni biashara imesha mature kabisa maana yake imekula muda mrefu zaidi kwa uwekezaji kabla ya kufika hapo,kama ni muajiriwa basi umeshafikia post za juu tu ofisini kwenu.kitu ambacho ni ukakasi kwa kundi kubwa la watanzania,viwanja vywa watz wengi wa ndoto ni 3mln-1.5 mln,wewe unatuletea story za 18ml bro[emoji15][emoji15].

hatukatai kutiana moyo,ila iwe ni kutiana moyo kweli,mambo ya nilianza na kuku mmoja wa mayai ndani ya mwaka nalisha mikoa sita,yanachanganya.

1.8 ml kwa mwezi ni pesa nyingi sana,kuiweka kwenye mfano,hata kama ulikuwa nayo,ungeipunguza kujishusha ili ukae kwenye kundi kubwa la watu.

utaenda halafu uje useme uliezeka paa kwa 17mln[emoji1787][emoji1787],halafu unasema unawapa watu moyo,ah kuweni serious bana.
Kwahiyo ajishusheee kisa kufurahishaa kundi kubwa la watuuuu,hayaaaa nayo ni maajabu ya jf ni upuuuziiii
 
Kwa Comment za watu humu inaonesha kusevu 2M kwa mwezi pesa nyingi mpaka wanaogopa...mimi mbona naiona kama pesa ndogo au ndio rahisi kuandika.
Wanamalalamiko sanaa ninabiashara iko sehemu nzuri tu kwa mwezi nasave hiyo na hapo nimeshalipa vijana wangu wawili mshahara na kod ya pango nk.
 
Safi sana bora mjitokeze mtoe shuhuda...inawezekana ukiwa smart...
 
Mmmmh huyo jamaa huwa ana tambo nyingi sana hujui hata ushike lipi au uache lipi...juzi Kati kasema kakamatia 12m, mahela yamejaa kibao kitaa, mara 1.8m kwa mwezi anasevu[emoji16][emoji16]
Ila.kama anadanganya basi atakuwa ana shida sehem..kwanza anaitesa nafsi
 
Ndoto za mchana hizi bhana
images%20(53).jpg
 
Leo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.

Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.

Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.

Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.

Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.

Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.

Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.

Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.

Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.

Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)
Huu uzi hauna maana kama licha hamna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom