moto wa maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2016
- 4,174
- 3,007
Positive minds always success....hongera sana mkuu ngoja niwe natunza hata hamsini tu
Wengine tujenge vitambiPoint.
Sasa kila mtu ajenge nyumba za jupanga atakaa nani?
Tugawane, wengine wajenge nyumba wwngine tujenge fremu.
Hongera sanaLeo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.
Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.
Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.
Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.
Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.
Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.
Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.
Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.
Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.
Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)
Mkuu acha hizo. Unawakatisha tamaa vijana.Hahahahaa dah sijui tufanyeje. Si wengine tutafia kwenye kupanga sijui.
nimerudiarudia sana kusoma hiyo bajeti ya mwezi nikidhani labda nikiwango alichokuwa akitenga kwa kila mwaka, nahisi amekuja kutudhihaki tuu!!Kila mwezi kuweka Mil 1.8 wewe sio mwenzetu aisee.
Kwamba hata angekuwa nayo aishushe ili akae kwenye kundi la wengi? Kuna ubaya gani mtu kuwa na hela? Kila mara humu JF watu wanaleta Stori za kuchukia umaskini mbona mtu akileta habari kinyume na umaskini watu wanawaka?kwani lengo lako kuleta uzi lilikuwa baya kiasi hicho!!!kwanini unapewa mrejesho unawaka!!!!
1.8ml kwa mwezi hiyo siyo ya kufungulia uzi hapa jf,utaonekana unatukana watu.sijui utasema ni mawazo ya kimasikini au vipi whatever.
ila wacha nikichanganue uone uko nafasi ipi maishani hapa.
kama ni reserved balance hiyo means una zaidi ya kipato cha 3mln/month.
sijui ni biashara ama ni muajiriwa,ila kama ni biashara imesha mature kabisa maana yake imekula muda mrefu zaidi kwa uwekezaji kabla ya kufika hapo,kama ni muajiriwa basi umeshafikia post za juu tu ofisini kwenu.kitu ambacho ni ukakasi kwa kundi kubwa la watanzania,viwanja vywa watz wengi wa ndoto ni 3mln-1.5 mln,wewe unatuletea story za 18ml bro[emoji15][emoji15].
hatukatai kutiana moyo,ila iwe ni kutiana moyo kweli,mambo ya nilianza na kuku mmoja wa mayai ndani ya mwaka nalisha mikoa sita,yanachanganya.
1.8 ml kwa mwezi ni pesa nyingi sana,kuiweka kwenye mfano,hata kama ulikuwa nayo,ungeipunguza kujishusha ili ukae kwenye kundi kubwa la watu.
utaenda halafu uje useme uliezeka paa kwa 17mln[emoji1787][emoji1787],halafu unasema unawapa watu moyo,ah kuweni serious bana.
Kila mtu ana dream yake. Kwake hio ni dream house. Kuna mtu anatamani awe na kwake tu itakuwa huyu mwenye nyumba ya 70m?Mimi wala silalami sioni cha ajabu ulichofanya! Na siwezi jenga ka nyumba cha 70M nije kutangaza hapa kama mwehu bila kuulizwa. Nyumba ya milioni 70 yenye fence na finishing ni nyumba ndogo ya kawaida kabisa haishtui.
21M umepaua, umechimba choo, umeweka grill na makorokoro kibao na bati ni za versatile that means hako kanyumba ni kadogo cha kawaida mno hakafai kuitwa dream hse. Nyumba ya maana upaue kwa versatile ama romantiles hakuna namna itapungua 20M.
Punguza maringo kijana bado sana hujafika popote.
JMT!!! Kazi iendeleee!!!!
Bro nimeshangaa watu kuona mil 1.8 kwa mwezi ni pesa nyingi. nachojiuliza hadi wale.wafanyabiashara kkoo hawapo humu? Maana kwao ukisema unasave mil 1.8 unaonekana bado upo chini Sana, bado najiuliza Ina maana watu huku hawana ndugu au marafiki wanaofanya biashara na kupata faida ya mil 5, 10 au 15 kwa mwezi?Kwamba hata angekuwa nayo aishushe ili akae kwenye kundi la wengi? Kuna ubaya gani mtu kuwa na hela? Kila mara humu JF watu wanaleta Stori za kuchukia umaskini mbona mtu akileta habari kinyume na umaskini watu wanawaka?
1.8m kwa mwezi nyingi Kwa mantiki gani? Nyingi kwa nani? Ukiangalia kiundani unaweza kukuta wanaosema nyingi bill zao kwenye pombe,kuhonga, na matumizi yasiyo muhimu inazidi hio 1.8m!
Hapa ndio uone tatzo lilipo, huyu mama Samia kazi anayo.Kila mtu ana dream yake. Kwake hio ni dream house. Kuna mtu anatamani awe na kwake tu itakuwa huyu mwenye nyumba ya 70m?
Guys hivi mil 1.8 kwa mfanyabiashara ni pesa nyingi kweli? Mil 1.8??? Humu Kuna watu wa aina gan? Mbona Kuna watu wa kawaida tu Wana make Hadi mil 10 kwa mwezinimerudiarudia sana kusoma hiyo bajeti ya mwezi nikidhani labda nikiwango alichokuwa akitenga kwa kila mwaka, nahisi amekuja kutudhihaki tuu!!
Wewe dada shida ni nini? Nina biashara zaidi ya 3 , mil 12 kwa project moja mbona ni pesa ya kawaida? Tatizo nini humu?Mmmmh huyo jamaa huwa ana tambo nyingi sana hujui hata ushike lipi au uache lipi...juzi Kati kasema kakamatia 12m, mahela yamejaa kibao kitaa, mara 1.8m kwa mwezi anasevu[emoji16][emoji16]
Bado nashindwa kuelewa hii mil 1.8 mbona ni pesa ndogo Sana kwenye biashara? Humu Ina maana hakuna wafanyabiashara kabisa? Mama Samia kazi anayoIla.kama anadanganya basi atakuwa ana shida sehem..kwanza anaitesa nafsi
Nimeshangazwa kweli watu kuogopa mil 1.8 kwa mwezi, Kuna watu nawafahamu wanapata faida Hadi mil 10 kwa mwezi tena ukiwaona huwezi amini. Watu humu wapojeKwa Comment za watu humu inaonesha kusevu 2M kwa mwezi pesa nyingi mpaka wanaogopa...mimi mbona naiona kama pesa ndogo au ndio rahisi kuandika.
Wewe sio mgeni humu JF. Ukileta Stori kama hii tegemea povu. Hapa lete thread Una siku mbili hujala,umefukuzwa kwenu uhame, huna Kodi utaona iyakavyochangiwa kwa furaha.Bro nimeshangaa watu kuona mil 1.8 kwa mwezi ni pesa nyingi. nachojiuliza hadi wale.wafanyabiashara kkoo hawapo humu? Maana kwao ukisema unasave mil 1.8 unaonekana bado upo chini Sana, bado najiuliza Ina maana watu huku hawana ndugu au marafiki wanaofanya biashara na kupata faida ya mil 5, 10 au 15 kwa mwezi?
Sikuwahi nilitegemea hili humu, mil 1.8 watu wanatoa povu na matusi? Kweli?
Nilikuwa sijawajua vizuri watu humu, Ila kwenye hili naanza kupata wasiwasi.Wewe sio mgeni humu JF. Ukileta Stori kama hii tegemea povu. Hapa lete thread Una siku mbili hujala,umefukuzwa kwenu uhame, huna Kodi utaona iyakavyochangiwa kwa furaha.
Angalia watu wanvyoshangilia wanaotumbuliwa na mama Samiha as if mtu akifukuzwa kazi yeye kipato kinakuwa.
Advice...Leo Kuna jambo ningependa kuwaeleza, lengo ni vijana kutokata tamaa magumu ni sehemu ya maisha. Kikubwa tuweke malengo na tupambane.
Angalizo: Kama una husda na wivu hii post usisome maana utashindwa kula leo.
Nilianza pilika za maisha mwaka 2011 soon after kugraduate, mambo yalikuwa mengi Sana Ila yalikuwa poa.
Ilipofika 2014 mwezi wa 3, nikanunua kiwanja goba njia nne kwa mil 18, ni kizuri na kikubwa. Hivyo jukumu lililokuwa mbele yangu ni kuanza kufikiria kujenga, japo pia nilikuwa na wazo la kuwa na hardware hukohuko goba kwa kuwa ujenzi kule ulikuwa na Kasi Sana.
Nilichofanya ni kuhakikishia kila mwezi naweka mil 1.8 ili mwisho wa mwaka nianze kidogo, na mwaka unaofuata mwishoni niendelee.
Mwaka wa kwanza yaani 2015 mwishoni nilikuwa nimekusanya jumla mil 21 hivyo nikaanza na foundation na kunyanyua boma. Nikalitelekeza.
Mwaka unaofuata 2016 nikaendelea na plan zangu zilezile na ilipofika December nikakusanya tena mil 21, hapa nikapiga bati kipindi hiki bati zile aina ya versatile zilishika chati jumla zilikuwa 145(zilibaki 6), pia niliiweka grills, mashimo ya choo, plumbing na wiring pesa yote ikaishia hapo.
Mwaka unaofuata 2017, vilevile nikakusanya mil 21 sikuacha lengo langu. Safari hii kazi ilikuwa kuzungusha ukuta, kupiga plasta, kununua gypsum, na tiles nikaziacha ndani humo.
Mwaka 2018 ulikuwa ni kwa ajili ya finishing, bahati mbaya sikufanikiwa kumaliza finishing Ila nikaapa 2019 lazima nimalizie.
Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mwisho na ilipofika mwezi wa 7, kila kitu kilikuwa tayari na nikahakia hapo rasmi. Jumla ilitumika mil 78.
Kuhusu hardware, Sasa hivi ni moja ya inayofanya vizuri goba kwa kuwa nilitumia ujanja wa kupita sites na kuongea na wenye nyumba na mafundi, nawapunguzia Bei kidogo wananipa kazi. SoMo kubwa usipende Sana faida kubwa, watu watakuja kwako.
Wito kile unachofanya fanya zaidi na zaidi, weka plan zako.vizuri, na Kama bado mambo hayajakaa sawa tafuta zaidi weka pembeni kidogo starehe.
Naogopa picha kwa kuwa pale najulikana sababu ya biashara zangu(gen supplies, kampuni ya mfukoni ya construction na hardware)
Hebu fafanua mkuu cjakupata hati fungani ndo nn na kuna utaratibu gani kuzipataAdvice...
Ukitumia njia hii, siyo vfibaya ila siyo wise kama unaweza kusave 1.8M a month.
Based on your explanation, hela ulikuwa either unaiweka kwenye kibubu au checking account benki na utunzaji wako haujaonyesha au haujaleta faida.
Ukitunza hela benki ni kama umewapa watu hela bure. Hayo ni mambo ya 70s, kwanini udundulize hela yako?? Ni upotevu wa hela kutunza hela kwenye kibubu au checking account.
Benki haziweki hela benki. Sasa kwanini unaweka hela benki with such disposable income? Benki zinanunua hatifungani za Benki kuu, ukiweza na wewe nunua.
Milioni 21.6 za mwaka 2014 zingekupatia coupoun ya 3.3 milioni mwaka 2015 kama ungenunua Bond ya miaka 20. baada ya miaka 5 ungekua na yearly coupons za milioni 16 na bado milioni 21.6 yako ipo palepale. Na hiyo milioni 21.6 bado unaweza kuiweka kama collateral bank ingawa kwa kipato chako huna haja.
Milioni 21.6 za mwaka 2015 ungeingiza milioni 13 baada ya miaka minne (4). Za mwaka 2016 ungeingiza milioni 10 baada ya miaka mitatu. Za mwaka 2017 ungeingiza milioni 7 Kwa hiyo, mwaka 2019 ungekuwa umeingiza faida ya milioni 45 na kuanza ujenzi, by 2020 ungekuwa na milioni yako 21 jumlisha yearly coupons za bonds 3 totalling 10 million jumla ungejenga nyumba yako ya 75million na bado una treasury bonds zenye thamani ya milioni 65 zinazokuingizia faida ya milioni 10 kwa mwaka.
Just a brotherly advice. .... might be off for a couple of millions.
Ukiwa na disposable income ya 2 million a month kwa Tanzania, usiweke hela Benki na kamwe usiweke hela kwenye simu. Benki zitakubembeleza zikupe mikopo zikijua upo financially smart na unaweza kunegotiate a very good interest na ukiona benki zinaongea na wewe, ujue unaingia next level easily. Kazi yako ni kutafuta proposal ya nguvu na kutake off.