Niliwahi kumwambia Hayati Magufuli, leo narudia kwa Rais Samia ili asipoteze muda wake

Maendeleo ya vitu yanachagiza yale ya watu.

Huwezi kukejeli uwepo wa ndege zenye kuongeza watalii wanaoongeza pato linalokwenda kuongeza madawa na kujenga madawati ya kisasa.

Huwezi kukejeli fly overs zinazoondoa muda wa kukaa njiani unaoongoza ufanisi wa mtu mmoja mmoja.

JPM alipambana ili tuachane na utamaduni wa kufanya kazi kwa mbwembwe nyingi za kujieleza mbele ya camera halafu tija inakuwa ni kama haipo.

JPM alikosea kwenye approach yake katika masuala kadhaa lakini lengo lake lilieleweka kwa mamilioni ya watanzania.

Mama Samia aende kitaasisi zaidi akiwa mkali kwa mawaziri wake lakini muungwana kwa watanzania.

Mama Samia aendelee kujenga hoja bila ya kuifokea jamii anayoiongoza.
 
Sahihi kabisa
 
Ili uweze kuwa kwenye Deep State unatakiwa uwe na vigezo gani?

Deep State inaundwa na watu wagapi?

Mfumo wa kiuongozi wa Deep State ukoje ukoje?

Je Deep state ina nguvu kuliko TISS?

Je Deep State inaushawishi mkubwa kuliko kamati kuu ya Ccm?
Kiongozi naomba sana sana unielimishe juu ya hayo. Asante sana sana
 
Deep state iliitaka Kumkomoa lowasa na chadema
 
Kitakacho kera zaidi kwa utawala huu ni kuendeleza chaguzi za kibabe, kutekana, watu kuumizwa, kufa na hakuna hatua zinazochukuliwa.
 
Hapa nakataa mkuu. Jpm alikua anataka fair business kati ya tanzania na nchi nyingine. Alitaka wananchi wawe na thamani sawa na foreigners. Na kutoa dhana ya cheap labour.

Hao wazungu wako wangapi hapa nchini hadi atake fair business na wao?
 

Naam Mkuu
 
Kabisa asee
 
Lakini naye toka siku hiyo hakuwahi kuonekana tena
 
Maza amechemka kabla hata ya siku 100 za mwanzo
 
Mimi nilimwambia kuwa kizazi cha sasa kinaongozwa kwa akili, ujanja, maarifa na mambo yote yahusuyo akili. Ubabe ungeweza kutumika machungani kwenye mbuzi, ng'ombe, na kondoo ambao hawana utashi kama binadamu.
 

Nawaza nao wazungu wangesema msipelekee misaada wale nyani wa africa maana wao ni mabeberu jpm aliwaita na wao wangemuita nyani daaa
 
In
Kabla ya daraja la sasa hivi, kuna ndugu yangu mmoja aliwahi kupoteza mtoto katika foleni ya ubungo wakati akiwa anampeleka hospitali.

Jamaa ana pesa nzuri tu (maendeleo ya watu) lakini miundombinu mibovu (maendeleo ya vitu) ilifanya apoteze mtoto.
Infantry uko juu wanaoelewa wataelewa wenzangu na mimi watakusamehe.
 
Angekuwa hawapendi wazungu, angewafukuza mabalozi basi mkuu. JPM alikuwa anataka fair play kati ya Tanzania na nchi zingine.
Mmmmh! Asingeweza kuwafukuza maana ingeleta diplomatic problem. Kila siku alikuwa anawaimba mabeberu mabeberu!!! Huo wimbo mpaka leo kuna watu wanauimba hasas kwenye taarifa ya wataalamu wa kumshauri raisi kuhusu covid 19. Wanasema wametumwa na mabeberu hao madaktari! Na hii mi naona ni sumu kaiacha mwendazake!!!! Na sumu hii itatutafuna sana. Hata hivi tunavyochat ni wazungu. Sasa tunawaonaje wabaya? Kila kitu chetu tunachofanya kama alivyosema mwandishi ni wazungu. Na tutaendelea na vya wazungu tu!!!!
 
sijasoma yote, nimesoma kidogo.. "WATU WENYE AKILI"... nakuunga mkono 100% uwekezaji kwenye vichwa vya watu aka maarifa ndio jambo la kwanza la maana kufanyika...Watanzania wengi sio smart kuweza kuleta hayo maendeleo tunayoyataka...
 
. Magufuli aliwekeza zaidi kwenye matamko kuliko kuweka mfumo imara ili hata yeye akiondoka mambo yatajiendesha vyema.
Niliwahi mwambia kuwa One manshow ni kama mbio za sakafuni ambazo lazima ziishie ukingoni. Nilimwambia anapoteza muda wake
Na kweli alipoteza sana muda ktk hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…