Nimeacha pombe na sigara lakini napata taabu sana, sipati usingizi hadi usiku wa manane

Umefanya uamuzi sahihi
 
tafuta mbegu za maboga hata kilo moja mix na aidha mtama au mahindi yani tengeneza kama lishe halafu saga, uwe unapika uji unakunywa kwa siku asubuhi na jioni fanya hivyo kwa mwezi mmoja utaona usingizi unavyoanza kukuvagaa, vitu vyengine kwasasa usiku usipende kukaa na mwanga wakati wakulala yani kama ukiwa unaenda kulala vitu vya mwanga zima, pia penda kuchosha akili aidha kwa kutafakari ama kusoma makala zakufikirisha ama hadithi zakufikirisha hii huufanya ubongo uanze kujilazimisha kupumzika!, so utakuwa unashangaa tu gari limezima!.
 
Asante mkuu ntazidi kupambana kila njia mpaka nishinde
 
Kila jambo lina ugumu wake binafsi nilijotaidi kuacha mishangazi ulipita mwaka ivi mwanzo ilikuwa ngumu. Lkn mwishoe nilizoea kabisa ila isivyo bahati nimerudia tena mwaka huu.ko ushauri wangu kwa sasa pumzika tu kwa mda mkuu.
 
Sawa mkuu japo sijaoa ntajitahid kuwakanda hivo hivo
 
Daah hii mada yako imenigusa sana nimeachana na madem zangu kadhaa kisa sigara nilianza nikiwa chuo japo sio mraibu wa pombe ila fegi ilikuwa hunambii kitu japo nina muda wa miaka 3 hv tangu navuta. Lkn no one noticed zaidi ya wale watu wangu wa karibu sana Nashukuru hata wazazi wangu hawajawahi kujua kama navuta
Lakini tangu tarehe 1 mwezi wa kwanza niliamua rasmi kuacha sigara kwa hiyo niko sober mwezi 1 sasa,Japo haijawa rahisi kuna muda misuli inakaza sana au napata maumivu ya kichwa kwa sababu damu inahitahi nicotine
Kuna kazi naifanya ya kuzunguka mikoani na shirika moja la Dini inanifanya niwe busy sana....kingine jitahidi sana kunywa maziwa fresh na matunda aina ya matango na tikiti vinasaidia sana pia kunywa maji mengi sana
Jitahidi usiishie njiani wataalamu wanasema ukijitahidi miezi 3 tuu tyr umeshaacha...
Nimejitahidi sana japo kuna siku uvumilivu ulinishinda nikaenda pembeni nikasmoke zangu wee ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Tuoambane man fegi sio issue kabisa ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿ’”
 
Anavyokosa usingizi maana yake hajaacha pombe..bado anashawishika kugida.

Labda tuambie ulikuwa unapiga bia au vikali
 

Pole sana na hongera kwa kuchukua hatua ya kuacha pombe na sigara.

Kwa sababu mwili ulishazoea vitu hivyo (pombe na sigara) kwa muda mrefu ukiacha kutumia kuna dalili utaziona (withdrawal symptoms) kama hiyo kukosa usingizi nk.

Hizo dalili (withdrawal symptoms) ndizo husababisha wale wanaojaribu kuepuka matumizi ya pombe na sigara nk kurudi tena kuvitumia.

Kwa hiyo ni muhimu ukaonana na daktari ili akusaidie katika namna ya kukabiliana na hizo dalili (withdrawal symptoms).

Kuna vituo/hospital wanatoa hiyo huduma kuacha pombe (detoxification...) hivyo watafute kwa msaada zaidi.

Utashinda.

Kila la kheri.
 
Ukiamua acha mkuu pigaba na hela yote mm imebaki usingizi ndio changamoto mwili kutetemeka uliacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ