Nimeacha pombe na sigara lakini napata taabu sana, sipati usingizi hadi usiku wa manane

Nimeacha pombe na sigara lakini napata taabu sana, sipati usingizi hadi usiku wa manane

Hongera hakuna kitu kinashindikana kuacha ukijizatiti na kuwa na msimamo.
 
Pole sana na hongera kwa kuchukua hatua ya kuacha pombe na sigara.

Kwa sababu mwili ulishazoea vitu hivyo (pombe na sigara) kwa muda mrefu ukiacha kutumia kuna dalili utaziona (withdrawal symptoms) kama hiyo kukosa usingizi nk.

Hizo dalili (withdrawal symptoms) ndizo husababisha wale wanaojaribu kuepuka matumizi ya pombe na sigara nk kurudi tena kuvitumia.

Kwa hiyo ni muhimu ukaonana na daktari ili akusaidie katika namna ya kukabiliana na hizo dalili (withdrawal symptoms).

Kuna vituo/hospital wanatoa hiyo huduma kuacha pombe (detoxification...) hivyo watafute kwa msaada zaidi.

Utashinda.

Kila la kheri.
Amen mkuu sitak artificial medication mkuu watanipa methadon hao🤣🤣 sema ntatoboa
 
Hapana mkuu nilishindwa kuacha taratibu nilikua nikivuta muda tu unaenda huku nikijiapiza kuacha na kulaumu nikilud tena
Sema utaacha tu kwa sababu ushaweka Nia. Kikubwa kua serious na jitahidi kuyapitia Mara kwa Mara madhara yanayosababishwa na sigara pamoja na pombe hiyo pia itakupa msukumo wa kuacha.
 
Sema utaacha tu kwa sababu ushaweka Nia. Kikubwa kua serious na jitahidi kuyapitia Mara kwa Mara madhara yanayosababishwa na sigara pamoja na pombe hiyo pia itakupa msukumo wa kuacha.
Amen mkuu
 
Daah hii mada yako imenigusa sana nimeachana na madem zangu kadhaa kisa sigara nilianza nikiwa chuo japo sio mraibu wa pombe ila fegi ilikuwa hunambii kitu japo nina muda wa miaka 3 hv tangu navuta. Lkn no one noticed zaidi ya wale watu wangu wa karibu sana Nashukuru hata wazazi wangu hawajawahi kujua kama navuta
Lakini tangu tarehe 1 mwezi wa kwanza niliamua rasmi kuacha sigara kwa hiyo niko sober mwezi 1 sasa,Japo haijawa rahisi kuna muda misuli inakaza sana au napata maumivu ya kichwa kwa sababu damu inahitahi nicotine
Kuna kazi naifanya ya kuzunguka mikoani na shirika moja la Dini inanifanya niwe busy sana....kingine jitahidi sana kunywa maziwa fresh na matunda aina ya matango na tikiti vinasaidia sana pia kunywa maji mengi sana
Jitahidi usiishie njiani wataalamu wanasema ukijitahidi miezi 3 tuu tyr umeshaacha...
Nimejitahidi sana japo kuna siku uvumilivu ulinishinda nikaenda pembeni nikasmoke zangu wee 🤣🤣
Tuoambane man fegi sio issue kabisa 🚮🚮💔
Amina mkuu miez 3 itaisha tu na hakika na kuendelea ntafanya yote uliyo niambia
 
Nilijitahidi kuacha pombe lkn nashindwa.

Nilianza kuacha kunywea bar. Nimeshinda sasa nanywea home.

Home nilijitahidi kuacha kwa kuanz kunywa bia chache hadi moja, bado ninehamia kula sprit. Yaani kwa sasa nakuwa kama popo.

Ushauri wa kwenda kwa daktari nikafanyiwe detoxification napata ubaridi maana niknikama kwend kufanyiwa ile kusFisha figo
 
Back
Top Bottom